Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Wengi wanaomtazama msichana mja mzito kama vile katenda kosa ambalo halistahili kufanywa na yeye, hapa naongelea mitazamo yetu ya kiafrika.
Mpaka mwanafunzi anafikia hatua ya kwenda kujifungua, tayari kisaikolojia keshajichukulia kana kwamba kazaliwa ili asifanye lolote maishani.
Lakini katika dunia ya sasa ya selfie, dunia ya mtu kumiliki simu za mkononi tangu akiwa mdogo, inawezekana vipi kwa mwanafunzi huyu kubakia salama, akawa mbali na vishawishi vya ngono?.
Nadhani vita ya muhimu ili kupunguza kama sio kuondokana kabisa na suala la mimba za wanafunzi wa sekondari na shule ya msingi, kwanza msukumo uwe ni katika kuhakikisha simu za mikononi zinakuwa mbali nao.
Ikishindikana basi angalau mzazi amruhusu binti yake kuwa karibu na simu katika siku za mwishoni mwa wiki tu.
Simu zinao msaada wa kurahisisha maisha, hasa mawasiliano lakini kuna upande wa urahisi wa msichana kuweza kuingia kwenye vishawishi vya ngono.
Wizara ya elimu inayo wajibu wa kutengeneza tangazo la kwenye radio au kwenye TV linalohamisha wazazi kuwa karibu na simu za watoto wao ambao ni wanafunzi.
Zamani wakati wa simu za mezani, wavulana walikuwa wakifika nje ya nyumba ya msichana wanaotaka kumtongoza walikuwa wakipiga miluzi au hata kupiga jiwe pipa la jalalani lililo karibu na nyumba.
Siku hizi hakuna tena matumizi ya "code" za mawasiliano, msichana anaongea moja kwa moja na kidume kwa kutumia smartphone yake.
Ni maendeleo kuwa na simu kwa dunia inakuwa ndogo lakini kwa wasichana wa sekondari na shule ya msingi, kwa kweli ni mtego mwingine wa uja uzito usiotarajiwa.