Vipi kuhusu mtego wa smartphones kwa wanafunzi wa kike?

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Wengi wanaomtazama msichana mja mzito kama vile katenda kosa ambalo halistahili kufanywa na yeye, hapa naongelea mitazamo yetu ya kiafrika.

Mpaka mwanafunzi anafikia hatua ya kwenda kujifungua, tayari kisaikolojia keshajichukulia kana kwamba kazaliwa ili asifanye lolote maishani.

Lakini katika dunia ya sasa ya selfie, dunia ya mtu kumiliki simu za mkononi tangu akiwa mdogo, inawezekana vipi kwa mwanafunzi huyu kubakia salama, akawa mbali na vishawishi vya ngono?.

Nadhani vita ya muhimu ili kupunguza kama sio kuondokana kabisa na suala la mimba za wanafunzi wa sekondari na shule ya msingi, kwanza msukumo uwe ni katika kuhakikisha simu za mikononi zinakuwa mbali nao.

Ikishindikana basi angalau mzazi amruhusu binti yake kuwa karibu na simu katika siku za mwishoni mwa wiki tu.

Simu zinao msaada wa kurahisisha maisha, hasa mawasiliano lakini kuna upande wa urahisi wa msichana kuweza kuingia kwenye vishawishi vya ngono.

Wizara ya elimu inayo wajibu wa kutengeneza tangazo la kwenye radio au kwenye TV linalohamisha wazazi kuwa karibu na simu za watoto wao ambao ni wanafunzi.

Zamani wakati wa simu za mezani, wavulana walikuwa wakifika nje ya nyumba ya msichana wanaotaka kumtongoza walikuwa wakipiga miluzi au hata kupiga jiwe pipa la jalalani lililo karibu na nyumba.

Siku hizi hakuna tena matumizi ya "code" za mawasiliano, msichana anaongea moja kwa moja na kidume kwa kutumia smartphone yake.

Ni maendeleo kuwa na simu kwa dunia inakuwa ndogo lakini kwa wasichana wa sekondari na shule ya msingi, kwa kweli ni mtego mwingine wa uja uzito usiotarajiwa.
 
Mkuu watoto wa siku hizi wanaweza kuwa na simu na mzazi asijue.Pia wanaweza pata simu hizi bila msaada wa wazazi.Kumbuka kuna wadau mkuu
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Hizi smartphone za Mzungu tunazisingizia kwa sababu kwa asili, Afrika lazima atafute wa kumsukumia matatizo yake!!!

Mwafrika ameanza kuhusudu ngono hata kabla simu za kukoroga hazijaingia let alone smart phone!!!

Hizo simu zina-catalyse tu hulka yetu ya kupenda kuvuana chupi lakini wala sio msingi wenyewe!!!

Ukitaka kuijua akili ya Mwafrika; nenda vijijini! Mtu ana bonge la eneo lakini choo hana! Gogo likimbana, anakimbilia vichakani... akili za wapi hizi!!!
 
Duh kaka chige umeua....
 
Wengi wanaomtazama msichana mja mzito kama vile katenda kosa ambalo halistahili kufanywa na yeye, hapa naongelea mitazamo yetu ya kiafrika.

Mpaka mwanafunzi anafikia hatua ya kwenda kujifungua, tayari kisaikolojia keshajichukulia kana kwamba kazaliwa ili asifanye lolote maishani.

Lakini katika dunia ya sasa ya selfie, dunia ya mtu kumiliki simu za mkononi tangu akiwa mdogo, inawezekana vipi kwa mwanafunzi huyu kubakia salama, akawa mbali na vishawishi vya ngono?.

Nadhani vita ya muhimu ili kupunguza kama sio kuondokana kabisa na suala la mimba za wanafunzi wa sekondari na shule ya msingi, kwanza msukumo uwe ni katika kuhakikisha simu za mikononi zinakuwa mbali nao.

Ikishindikana basi angalau mzazi amruhusu binti yake kuwa karibu na simu katika siku za mwishoni mwa wiki tu.

Simu zinao msaada wa kurahisisha maisha, hasa mawasiliano lakini kuna upande wa urahisi wa msichana kuweza kuingia kwenye vishawishi vya ngono.

Wizara ya elimu inayo wajibu wa kutengeneza tangazo la kwenye radio au kwenye TV linalohamisha wazazi kuwa karibu na simu za watoto wao ambao ni wanafunzi.

Zamani wakati wa simu za mezani, wavulana walikuwa wakifika nje ya nyumba ya msichana wanaotaka kumtongoza walikuwa wakipiga miluzi au hata kupiga jiwe pipa la jalalani lililo karibu na nyumba.

Siku hizi hakuna tena matumizi ya "code" za mawasiliano, msichana anaongea moja kwa moja na kidume kwa kutumia smartphone yake.

Ni maendeleo kuwa na simu kwa dunia inakuwa ndogo lakini kwa wasichana wa sekondari na shule ya msingi, kwa kweli ni mtego mwingine wa uja uzito usiotarajiwa.
Tuache kusingizia smart phone---Wazazi tumeproof failure kwenye malezi ya mabinti wetu.Tunawapa uhuru wa kuvaa mavazi ya kuonyesha maumbo yao kipindi cha likizo. Mzazi unatoka na bent yako--kavaa kiskini tight, maziwa nje nk.alafu unalalamika kapewa mimba.
 
hivyo hivyo na hivi vitoto viache kuvaa viskini tight, na kuachia matiti nje--viache matangazo ya miili yao.
Wavae mavazi yanayowasitiri maumbo yao kikweli kweli.Viskini tight watavikuta tu wakimaliza.Namuunga mko Mheshimiwa Magu--FUKUZA TU !!!
Mimi naunga mkono hii ya kutorudi shule....
 
Sio kila mtoto mwenye simu shule basi mzazi wake anajua...........mimi nimeshawahi kutumia cm kuanzia form 2 mpk namaliza bila wazazi kufahamu pale nyumbani tena sikua na simu moja.......kwa hilo la simu lisimfike mzazi moja kwa moja
 
Sasa ndio unajisifu, na kuwafundisha wadogo zako wafiche simu au??? Hapa tunataka kuwasaidia wanafunzi ili wasiishie kulea watoto.Ulikuwa unaificha wapi hiyo simu sasa---huko chini au? Sema ili nao zapatee maujanja.
 
Huyu utandawazi mbona kila kitu anasingiziwa yeye jamani, sidhani kama shida ni teknolojia na utandawazi shida ni sisi watumiaji wa hivyo vitu.
 
Back
Top Bottom