Vipi kuhusu hili suala Mahakama kuwa na biashara ya choo cha kulipia?

viva666

Senior Member
Oct 11, 2016
111
116
Habari wapendwa JF.

Kwa huzuni na mshangao mkubwa leo nimeshuhudia kwa macho, akili, masikio yangu nikidaiwa hela baada ya kuingia choo cha mahakamani kuu Mwanza.

Ipo hivi: Leo Jji la Miamba, Rock City (Mwanza) lilipata neema ya mvua kuanzia mapema saa 12 asubuhi mpaka mida ya mapema saa tisa alasiri.

Kama ilivyo ada, mahakama haipangiwi nilifika pale mahakamani mapema licha ya mvua kunyesha, wakati nasubiri taratibu zingine zifuate lahaula nikabanwa haja ndogo kwelikweli basi nikaangaza huku na kule maeneo ya mahakama nikakiona choo maeneo ya mahakama karibu na canteen ya mahakama basi nikaona isiwe taabu mimi nikaingia kwa kasi mule ndani kumaliza shida zangu.

Basi ile natoka tu msalani naitwa na sauti ya mdada mmoja hivi wa makamu, nikaitika wito kwa kumsogelea karibu nijue shida nini!? Cha kuhamaki nafika hapo ananambia hela nadaiwa.Ya nini? Nikauliza, akasema si umetoka chooni.

Ilibidi tuanze kubishana sasa nikiwa na hoja zifuatazo:

1. Mbona hapo hakuna bango elekezi ni choo cha kulipia.

2. Itakuaje kama taasisi zote kama TMDA, PCCB, TANESCO, DAWASCO, hospitali, shule, TCRA hawatozi tozo kwa vyoo vilivyopo kwenye taasisi sembuse taasisi nyeti kama mahakama iweje initoze choo chake.

3. Hakuna bei elekezi wala bango kuonesha unapaswa kulipia.

4. Mtoza pesa kajibanza sehemu hivi na hakuambii kuna malipo mpaka utoke msalani.

5. Je, watu wakitoka kula canteen watabidi walipie choo nao.

Hitimisho: Tulisumbuana sana mpaka mwisho akaona aniache tu.

Mamlaka husika chukueni hatua kwa hawa watu waliogeuza choo cha taasisi ama mhimili kuwa mradi wao binafsi. Huu ni uhuni mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo haya bhana
nafikiri ni tamaa ya hela tu iyo

Sasa sijui hizo hela zinazotolewa na serikali katika idara mbali mbali zinafanyiwa nini maana kulipia choo ni ishara kuwa kunawatu wanalipwa hapo Hasa wafanya usafi ambao katika logic serikali ndio huwalipa hao
Sasa hayo mapato yanaenda wapi wakiyapata

Maana kama ni ujenzi ni wa serikali apo

Uvivu na umaskini ndio tatizo

MUNGU tusaidie
 
Back
Top Bottom