Vipi kuhusu ajira za TRA wa walioajiriwa serikalini.

Gooodwin

Member
Sep 22, 2016
77
66
Habari Wapiganaji, mimi ni muajiriwa wa serikalini, nipo local government nimeliona tangazo la kazi la TRA nafasi 400 zimenivutia, na vile vvile nina ndoto ya kuhama local government.

kwa bahati nzuri nimelisoma hili tangazo vizuri, nikakutana na kipengele kinasema mtumishi aliyeajiriwa aitishe barua kwa mwajiri nami bila kuchelewa nikaandika barua na kwenda kwa DED, DED akaniabia niende kwa HR, Baada ya kufika kwa Hr kagoma katu katu kunipitishia barua yangu.

Sasa wadau swali langu ni kwamba je niombe hivyo hivyo bila kupitisha kwa DED?
Na je ikitokea nikapata kazi TRA, check number haiwezi ku double click.

Wazoefu, maafisa utumishi naombeni ushauri wenu.
 
Kama wewe ni mtumishi wa umma (Isipokua mashirika ya umma) kiomba bila kupitishia barua yako ya maombi kwa mwajiri wako hutaitwa kwenye usaili kwa sababu utakua umedanganya.

Waajiriwa wote wa serikali kuu, serikali za mitaa, taasisi zilizo chini ya serikali kuu au wizara isipokua mashirika ya umma taarifa zao zinahifaziwa kwenye mfumo wa ajira unaoitwa Lauson.

Hivyo kama ikitokea ukaajiriwa kwa mara ya pili sehemu nyingine ndani ya serikali kuu au serikali za mitaa au taasisi zilizo chini ya serikali kuu, watakapoanza kukuingiza katika mfumo huo wa ajira huo mfumo utakukataa maana tayari una taarifa zako. Hii ni kuepuka wewe kulipwa mishahara miwili ndani ya mfumo mmoja wa ajira.

Hivyo wanataka upate kibali toka kwa mwajiri wako ili iwapo utafaulu usaili iwe ni kukubadilishia mwajiri kutoka DED kwenda kamishina au mwajiri mwingine ila taarifa zako ni zile zile.

Wale wa mashirika ya umma wao wanaomba tu bila kupitia kwa mwajiri maana wao sio watumishi wa umma ila ni watumishi katika mashirika ya umma na pia hawako katika mfumo wa ajira wa Lauson, ndio maana unaona hata ajira zao wanatangaza wenyewe. Mashirika ya umma ni yale yenye magari ya SU( SOMA ULE).

Nadhani itakusaidia kuelewa mantiki.
 
Aisee.

Wakizingua tulia ulinde kibarua chako ulichokuwa nacho
 
Habari Wapiganaji, Mimi ni Muajiriwa wa serikalini, nipo local government. nimeliona Tangazo la kazi la TRA nafasi 400 zimenivutia, na vile vvile nina ndoto ya kuhama local government. kwa bahati nzuri nimelisoma hili tangazo vizuri, nikakutana na kipengele kinasema mtumishi aliyeajiriwa aitishe barua kwa mwajiri. nami bila kuchelewa nikaandika barua na kwenda kwa DED, DED akaniabia niende kwa HR, Baada ya kufika kwa Hr kagoma katu katu kunipitishia barua yangu.

sasa wadau swali langu ni kwamba je niombe hivyo hivyo bila kupitisha kwa DED?
Na je ikitokea nikapata kazi TRA, check number haiwezi ku double click.

WAZOEFU, MAAFISA UTUMISHI NAOMBENI USHAURI WENU.

Ni ruhusa kuapply sema barua yako ya kuapply iwe ina muhuri wa mwajiri wako..yaani iwe na U.F.S... na imepigwa Muhuri na Signature ya Bosi wako..tena DED ndo aipitishe..bila hivyo halafu wewe ni mwajiriwa wa serikali hutakubaliwa hiyo app yako...pia ukipata ajira wewe utahama na si utaanza upya...
 
Sasa anagoma kusain kwan yy ndio anakulipa mshahara?? Ndio ajue mazingira ya kazi yake cio mazuri aongeze mshahara cio akatae kusain.
Kuna hiyo tabia kwa watu wengi tu unaeza enda omba kazi akakwambia hakuna wkt bosi wake hajawahi ht kusema lolote.mkomalie uende ukajaribu
 
Kama wewe ni mtumishi wa umma (Isipokua mashirika ya umma) kiomba bila kupitishia barua yako ya maombi kwa mwajiri wako hutaitwa kwenye usaili kwa sababu utakua umedanganya.

Waajiriwa wote wa serikali kuu, serikali za mitaa, taasisi zilizo chini ya serikali kuu au wizara isipokua mashirika ya umma taarifa zao zinahifaziwa kwenye mfumo wa ajira unaoitwa Lauson.

Hivyo kama ikitokea ukaajiriwa kwa mara ya pili sehemu nyingine ndani ya serikali kuu au serikali za mitaa au taasisi zilizo chini ya serikali kuu, watakapoanza kukuingiza katika mfumo huo wa ajira huo mfumo utakukataa maana tayari una taarifa zako. Hii ni kuepuka wewe kulipwa mishahara miwili ndani ya mfumo mmoja wa ajira.

Hivyo wanataka upate kibali toka kwa mwajiri wako ili iwapo utafaulu usaili iwe ni kukubadilishia mwajiri kutoka DED kwenda kamishina au mwajiri mwingine ila taarifa zako ni zile zile.

Wale wa mashirika ya umma wao wanaomba tu bila kupitia kwa mwajiri maana wao sio watumishi wa umma ila ni watumishi katika mashirika ya umma na pia hawako katika mfumo wa ajira wa Lauson, ndio maana unaona hata ajira zao wanatangaza wenyewe. Mashirika ya umma ni yale yenye magari ya SU( SOMA ULE).

Nadhani itakusaidia kuelewa mantiki.

Nashukuru kwa ushauri. imeeleweka vyema.
 
Ni ruhusa kuapply sema barua yako ya kuapply iwe ina muhuri wa mwajiri wako..yaani iwe na U.F.S... na imepigwa Muhuri na Signature ya Bosi wako..tena DED ndo aipitishe..bila hivyo halafu wewe ni mwajiriwa wa serikali hutakubaliwa hiyo app yako...pia ukipata ajira wewe utahama na si utaanza upya...

Aisee.

Wakizingua tulia ulinde kibarua chako ulichokuwa nacho

Acha tu, hapa ujanja sina.
 
Kama wewe ni mtumishi wa umma (Isipokua mashirika ya umma) kiomba bila kupitishia barua yako ya maombi kwa mwajiri wako hutaitwa kwenye usaili kwa sababu utakua umedanganya.

Waajiriwa wote wa serikali kuu, serikali za mitaa, taasisi zilizo chini ya serikali kuu au wizara isipokua mashirika ya umma taarifa zao zinahifaziwa kwenye mfumo wa ajira unaoitwa Lauson.

Hivyo kama ikitokea ukaajiriwa kwa mara ya pili sehemu nyingine ndani ya serikali kuu au serikali za mitaa au taasisi zilizo chini ya serikali kuu, watakapoanza kukuingiza katika mfumo huo wa ajira huo mfumo utakukataa maana tayari una taarifa zako. Hii ni kuepuka wewe kulipwa mishahara miwili ndani ya mfumo mmoja wa ajira.

Hivyo wanataka upate kibali toka kwa mwajiri wako ili iwapo utafaulu usaili iwe ni kukubadilishia mwajiri kutoka DED kwenda kamishina au mwajiri mwingine ila taarifa zako ni zile zile.

Wale wa mashirika ya umma wao wanaomba tu bila kupitia kwa mwajiri maana wao sio watumishi wa umma ila ni watumishi katika mashirika ya umma na pia hawako katika mfumo wa ajira wa Lauson, ndio maana unaona hata ajira zao wanatangaza wenyewe. Mashirika ya umma ni yale yenye magari ya SU( SOMA ULE).

Nadhani itakusaidia kuelewa mantiki.
Mfumo huu wa Lawson unatambua mtumishi kwa no IPI ni check number ya mtumishi au index number ya kidato cha NNE ya mtumishi? Naomba unifafanulie kama una uelewa wa hii system
 
Na mimi swali langu ni kama lako
Huu mfumo unatambua taarifa zako za kidato cha nne na sita au chuo. Maana namba yako ya cheti cha chuo ni yako peke yako, sasa ikitokea kua namba hiyo inaonekana kuingizwa upya mfumo utakataa kua hii namba ipo.

Kwa vyovyote kama unafanya kazi hizo idara za seikali na mfumo wa Lauson una taarifa zako, ikitokea ukaacha kazi kukuingiza tena upya unakataa, hivyo ukipata kazi mpya ndani ya serikali kinachofanyika ni kukuhamisha kutoka mwajiri mmoja kwenda mwingine, mfano kutoka mkuu wa TMAA kwenda DED na kinyume chake.

Hii pia inaepusha mtumishi mmoja kua na cheki namba 2 na kupelekea kuzalisha watumishi hewa.

Zamani ma HR wa serikalini walikua wanachakachua kwa kuingiza taarifa za uongo za watumishi ambao hawapo na kujilipa hiyo mishahara. Ila zama hizi za Magufuri huo mchezo umekufa.
 
Back
Top Bottom