Vipi kama hawa watu walipandikizwa?

mtimawachi

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
1,208
2,000
Katika watu wanaouharibu ulimwengu ni wanasiasa,

Unaweza mkajikuta mpo watu kumi Chadema, mkidhani mna nia moja kumbe nane kati yenu ni makada wa CCM. Baadae unasikia tu wameunga juhudi halafu mnaanza kuwalaumu eti wamenunuliwa hao wamerudi kwao.

Unadhani serikali ni jinga mpaka imteue nassari, au 'juakali' waongoze wilaya/mkoa. Yaani mtu atoke upinzani vuup! Afikie kuula CCM/Serikalini? Kama uliwaza hivyo ulikosea.

Mkae mkijua baada ya shetani anafuata mwanasiasa.
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,369
2,000
Siasa za Maji Taka za Tanzania Awamu ya 5 kwanini Wakati wa Mwinyi ,Mkapa na Kikwete hakukuwa na Siasa hizo ina maana kupandikiza kumeanza Awamu ya 5 Siasa za Chuki za Awamu ya 5 za kutaka Kuufuta Upinzani ndio zilizopelekea Wanasiasa Kununuliwa na hizo Teuzi ni Mikataba Waliyokubaliana wakati wa Hiyo Biashara Haramu ya Mwendazake.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061

Upo sahihi mkuu
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,764
2,000
Katika watu wanaouharibu ulimwengu ni wanasiasa,

Unaweza mkajikuta mpo watu kumi chadema,mkidhani mna nia moja kumbe nane kati yenu ni makada wa ccm. Baadae unasikia tu wameunga juhudi halafu mnaanza kuwalaumu eti wamenunuliwa hao wamerudi kwao.

Unadhani serikali ni jinga mpaka imteue nassari,au 'juakali' waongoze wilaya/mkoa. Yaani mtu atoke upinzani vuup! Afikie kuula ccm/serikalini!? Kama uliwaza hivyo ulikosea.

Mkae mkijua baada ya shetani anafuata mwanasiasa.
The snare was set to meet that objective by late Magufuli and as such hungry and unscrupulous individuals from the opposition camp got trapped.
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,312
2,000
Politics yes,ILA wote hawa ni Watanzania hakuna aliye mkimbizi na wanastahili kuitumikia nchi yetu regardless imani zao za kiitikadi,mara ngapi tunashuhudia USA president (Democrats)akamteua ex president (Republican)kuiwakilisha nchi ?historia inatufunza sana,kuna kipindi Madiba aliishangaza South Africa kwa kumwachia madaraka ya Urais Mangustu Buthelezi(from opposition)na nchi ikaendelea na cha ajabu kwenye kipindi hiki cha kuachiwa nchi aliamurisha majeshi ya South Africa kuvamia Lesotho!!!
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,608
2,000
Katika watu wanaouharibu ulimwengu ni wanasiasa,

Unaweza mkajikuta mpo watu kumi chadema,mkidhani mna nia moja kumbe nane kati yenu ni makada wa ccm. Baadae unasikia tu wameunga juhudi halafu mnaanza kuwalaumu eti wamenunuliwa hao wamerudi kwao.

Unadhani serikali ni jinga mpaka imteue nassari,au 'juakali' waongoze wilaya/mkoa. Yaani mtu atoke upinzani vuup! Afikie kuula ccm/serikalini!? Kama uliwaza hivyo ulikosea.

Mkae mkijua baada ya shetani anafuata mwanasiasa.

Hamna cha kupandikizwa Mkuu, kwa kawaida kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani. Ifahamike kuwa kwenye upinzani hasa wenye nguvu kunataka kujitoa muhanga, sio wote wanaweza, wengine kwa uoga, tamaa ya mali na mambo kama hayo, hutumiwa na chama tawala kupunguza nguvu ya upinzani. Ni kweli kuna wanaopandikizwa, ila sio kwa hao wasaka tonge.
 
mtimawachi

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
1,208
2,000
Siasa za Maji Taka za Tanzania Awamu ya 5 kwanini Wakati wa Mwinyi ,Mkapa na Kikwete hakukuwa na Siasa hizo ina maana kupandikiza kumeanza Awamu ya 5 Siasa za Chuki za Awamu ya 5 za kutaka Kuufuta Upinzani ndio zilizopelekea Wanasiasa Kununuliwa na hizo Teuzi ni Mikataba Waliyokubaliana wakati wa Hiyo Biashara Haramu ya Mwendazake.
Wanaweza kukupandikizia hata tangu yupo chuo na usihisi
Zito kakulia chadema lakini usikute ccm nao walimlea akiwa hukohuko
Unaweza usivione vitu hivi wakati MKAPA,KIKWETE,kumbe ndio kipindi hichohicho ndio walikuwa wanaandaliwa
 
mtimawachi

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
1,208
2,000
Hamna cha kupandikizwa Mkuu, kwa kawaida kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani. Ifahamike kuwa kwenye upinzani hasa wenye nguvu kunataka kujitoa muhanga, sio wote wanaweza, wengine kwa uoga, tamaa ya mali na mambo kama hayo, hutumiwa na chama tawala kupunguza nguvu ya upinzani. Ni kweli kuna wanaopandikizwa, ila sio kwa hao wasaka tonge.
CCM kwenye hili ni mabingwa,ila sikukatalii WASAKATONGE kuwa hawapo.
Ninachomaanisha ni kwamba SAMIA asionekane kama AMEKURUPUKA.
Siasa ni taaluma mkuu
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,608
2,000
CCM kwenye hili ni mabingwa,ila sikukatalii WASAKATONGE kuwa hawapo.
Ninachomaanisha ni kwamba SAMIA asionekane kama AMEKURUPUKA.
Siasa ni taaluma mkuu

Ccm hawana ubingwa wowote kwenye hili, wanachofanya sio kupandikiza watu, bali hupeleka ushawishi kwa wapinzani kwa ahadi za vyeo, ama wakati mwingine hufanya hujuma kwa shughuli za kumuingizia kipato mpinzani wamtakaye, na wakifanikiwa kumpata mpinzani mdhaifu ndio hufanya yao. Hilo la kwamba wanapandikiza sio kweli, maana sio wazuri kwenye intelijensia zaidi ya kutumia mabavu.
 
Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,748

Mbona na mimi ninanafasi kubwa kwenye kundi lenu??
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,234
2,000
Hata mwenyekiti wa chama fulan cha upinzani ni pandikizi la chama tawala. Ndio maana kila unapofika uchaguzi ambao unaonekana kutishia uhai wa chama tawala kubaki madarakan, anachukua wale wale pandikizi wengine wa chama tawala kuja kugombea nafasi za juu kwenye uchaguzi na baadae kukisambaratisha chama chake anachokiongoza kwa makusudi kabisa. Hapa namaanisha huyo mwenyekiti na wanatoka chama tawala kuja kugombea upinzani lengo lao huwa ni moja tu.
 
Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,029
2,000
Unajua no sawa na Ile 2015 ya lowasa ametoka CCM akaja akapewa kuwa mgombea wakati akina Silaa na wengine wamepigania chadema kwa nguvu zote Hadi kuwekwa jela , kupigwa mabomu, kuitwa vibaraka nk.

No wonder Slaa akaamua kutoka zake maana unapigania chama ili nawe chama kikupe fadhila at last anakuja mtu from nowhere ambae hajakisimamia chama anakuja na maslahi yake halafu anapewa shavu. Inauma sana kiukweli.

Hao vijana wa CCM lazima waumie maana wengi walipambana kusimamia maslahi ya chama, wakilala nje, walitumia pesa zao mfukoni wakati mwingine halafu anakuja mtu wa upinzani aliyekuwa anawafanya wasilale kuhakikisha wanaeneza Sera za chama Chao then anapewa shavu, it totally unfair and inconsiderate act.

Lakini wakome kuishangilia CCM. Mama haieleweki keshaanza kupaka henna na kushinda mitandaoni tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom