Vipi hatma ya wito wa kutumia kikoa cha .com Tanzania?

ndotoyangu

Senior Member
Nov 7, 2020
101
250
Mwaka jana (2020) mwezi wa kwanza TCRA ilitoa wito ya watu wote kutumia .co.tz na ukitumia .com ni kosa ambalo unaweza kulipishwa faili au kifungo.

Swali langu ni je, mpaka sasa sheria hiyo ipo? na kama bado ipo kwa nini baadhi ya watu wanaendelea kutumia .com? naomba ufafanuzi kwa wanaofahamu swala hili.

Asanteni
 

Erasto Jr

New Member
May 29, 2020
4
45
Nahisi wamejichanganya kidogo kikoa kinategemea na kitu unachofanya.

Commercial we use .com

Education .edu

wanaideal na issues za bongo kama mwananchi, global na wengine .co.tz lkn wakurungwa wanaoweka .com hawajatarget maswala ya bongo hapa
 

ndotoyangu

Senior Member
Nov 7, 2020
101
250
Nahisi wamejichanganya kidogo kikoa kinategemea na kitu unachofanya
Commercial we use .com
Education .edu
wanaideal na issues za bongo kama mwananchi, global na wengine .co.tz lkn wakurungwa wanaoweka .com hawajatarget maswala ya bongo hapa
Ahsante sana
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
33,263
2,000
Watu wanaendelea kutumia .com kama kawaida kwa sababu uhuru wa habari siyo mapenzi,hisani,kudra wala takwa la Rais wala taasisi yoyote ile bali ni takwa la kikatiba.Kuzuia matumizi ya .com Tanzania ni kuminya uhuru wa habari pamoja na uhuru wa kujieleza ambao ndiyo msingi wa katiba yetu.Sheria kandamizi kama hizi zinapaswa kupingwa hadi na mawe ambayo hata uhai hayana.

Suala la uhuru wa habari na haki za kujieleza ni haki yetu kikatiba.

Haki huwa haiombwi wala huwa haitolewi bure kama unavyodhania bwana mleta uzi bali haki huchukuliwa kwa nguvu na ndiyo maana watu wanaendelea kutumia .com bila wasiwasi wowote ule.

Rais na taasisi zozote zile hazina wajibu wala haki wala nguvu wala amri ya kuzuia au kuruhusu watu kutumia .com na pia hatuna haja wala wajibu wa kumuomba Rais wala taasisi yoyote ile iruhusu matumizi ya .com Tanzania bali ni haki yetu na mtu yoyote yule ikiwa ni pamoja na Rais au taasisi yoyote ile ikituzuia tuna wajibu kikatiba wa kuchukua haki hiyo kwa nguvu kwa sababu uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi katika katiba yetu.

Rais na taasisi zozote zile zitake zisitake suala la kutumia .com Tanzania ni haki yetu kikatiba wala siyo mapenzi yao na wasipotaka tuna wajibu kikatiba wa kuwalazimisha.

Umeelewa mleta mada?
 

Super Assassin

JF-Expert Member
Jul 12, 2018
409
500
Nahisi wamejichanganya kidogo kikoa kinategemea na kitu unachofanya.

Commercial we use .com

Education .edu

wanaideal na issues za bongo kama mwananchi, global na wengine .co.tz lkn wakurungwa wanaoweka .com hawajatarget maswala ya bongo hapa

Kwahyo Commercial purpose si tunatumia .com maana hizo sheria sasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom