TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Muda umepita sasa tangu zisambae taarifa za Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi taifa, Mhandisi James Mbatia kupelekwa nchini India kutibiwa matatizo ya Mguu yanayomsumbua.
Zilipotolewa taarifa za aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Samwel Sitta(R.I.P) kupelekwa nchini ujerumani kutibiwa tatizo la mguu, maneno mengi yalisemwa hasa kutoka kwa Wapinzani wakihoji tatizo la mguu tu kumpeleka mtu nje ya nchi kwa matibabu.
Tuyaache hayo ya wanasiasa. Basi tujulishwe hali ya Ndugu yetu James Mbatia, vipi hali ya mguu wake unaendeleaje huko aliko?