Vipi Haki na Mwelekeo wa Mwanangu?

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
street%20children.jpg


Hivi kila leo tunapata ushahidi na uchungu wa matatizo jinsi gani watu wachache Tanzania wamepewa busara za kujipendelea na kujibagua kitabaka. Kinachonigusa zaidi ni huu ubilionea na umilionea wa mtoto wa kikwete, Ridhiwan. Mtoto wa kiongozi wa chama fulani na Baba yake kumpa power ya influence kubwa ya kuwa tajiri mkubwa Tanzania. Yeye mtoto wa kikwete sio peke yake katika huu utamaduni mpya wa Taifa letu, wapo watoto wa Lowassa, Nnauye, Makamba, Mkapa, Rostam, Chenge na wasisimizi wengine wa ccm. Ninacho kijua mimi mpaka sasa hakuna industries yeyote au Silicon Valley au Founder yeyote wa technology katokea Tanzania.

Alipoulizwa (Ridhiwan) mbona anaonekana akitembelea magari ya kifahari, mtoto huyo wa Rais alisema: “Hapa mjini unaweza kumuona mtu amevaa suti ukadhani ya kwake kumbe ameazima. Mimi nina marafiki wengi, huwa wananiazima magari yao nitembelee, juzijuzi hapa nilikuwa na benzi ya rafiki yangu….jamani miundombinu ya mjini si mnaijua?”
Mtoto wa Rais Kikwete aukana ubilionea

Ninachokifahamu mpaka sasa kwa kuishi kwangu Tanzania ni kwamba mtoto wangu aliechini ya miaka kumi akindelea kuishi Tanzania, hatapata miasha ya Ridhiwan, elimu bora, fedha za kulipia shule bora, huduma bora akipata maleria au kuharisha na hata akifanya vizuri shuleni hatapata kazi nzuri ya kujenga familia yake. Swali langu ni hili, mimi nibaki na kukaa kimya bila kupigania haki yake ya Kikatiba? Au niendelee na mapigano ya haki yangu ya Katiba na Wananchi wenzangu?

Aliewapa wakina Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Nnauye, Lowassa, Rostam, Chenge, Pinda, Malecela na familia zingine chache Tanzania hii Haki ya kutawala na kuongoza wanapoamua wao, kupata huu utajiri na maisha bora ni nani? Hii Haki or the Civil Rights of Tanzania iliibiwa vipi na mwanzilishi ni nani? Kwanini serikali ya Tanzania wanapewa hii nafasi ya kujificha nyuma ya pazia la udini, kutumia vyombo vya usalama na vyombo vya habari kuendelea kuwakandamiza watanzania?

Ukweli na Unafiki Gani hapa ccm kwa miaka 50?
"Ujamaa, kama demokrasi, ni moyo katika nchi ya Ujamaa kama
unataka kuhakikisha kwamba watu wanajali shida za watu wengine,
linalotakiwa ni mawazo ya Kijamaa, wala siyo kufuatisha tu utaratibu
maalum wa siasa. Shabaha ya kitabu hiki ni kufikiria tabia hiyo; wala
siyo kueleza utaratibu unaotakiwa kuendesha Ujamaa katika mataifa
ya kisasa"

http://www.ccmtz.org/nyaraka/UJAMAA.pdf

"Haki ya Kila Mtanzania kupata Elimu Bora, Huduma Bora ya Afya, Ajira na Kujua Wajibu wa Serikali Yako"

"Kukaa Kimya na Kutowaelimisha Wananchi Wenzako ni SAWA NA KUWAKANDAMIZA"
 
Bado kidogo sheria ya kumiliki silaha itakua huria...let us wait...itasaidia sana kupunguza Temper
 
Afadhali umeona kitakacho mkuta mwanao,hivi mbona vibaka wa mtaani tunawachoma moto?tunashindwa nini kupanga mawe barabarani na kuwasulubu watawala hawa mbona rahisi basi hili tumeshindwa tuwanyime kura kwa sauti ya pamoja 2015 ili kuondoa lawama hizi jamani ee inatosha tusimame basi
 
Back
Top Bottom