Vipi endapo kiwango cha madini baada ya uchenjuaji nchini kutoendana na taarifa na. 1 ya makinikia?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,515
2,000
Kati ya mapendekezo ya taarifa ya pili ya makinikia ni kujengwa kwa kiwanda cha kuchenjua makinikia ndani ya nchi. Na inasemekana Barrick/ Acacia wamekubali kufanya hivyo. Ila viwango vya kwenye taarifa hiyo vimepingwa kuwa na chumvi mno. Sasa endapo kiwanda kikianza kazi na uzalishaji wa dhahabu na madini mengine ukawa tofauti na viwango vya kwenye taarifa ya kwanza ya makinikia hasa kwa kushuka, mambo yatakuwaje ingawaje itategemea na mkataba na mwekezaji?

Na endapo Barrick/ Acacia atakuwa amelipa madai ya Tanzania, je itabidi arudishiwe fedha yake?

Halafu, hawa jamaa ni wavumilivu sana, na wana kawaida ya kurudisha kilicho chao hata baada ya miaka mingi. Mfano, waliitwaa NBC Tanzania ambayo ilikuwa Barclays kabla ya utaifishaji mwaka 1967 kwa njia ambayo mtu wa kawaida sio rahisi kuelewa, na pia serikali ilijitahidi kuona hilo na kukwepa lakini mwisho wakapigwa bao. Je, vita hii ya uchumi waliotangaza tena leo hii awamu ya tano watashinda kwa kuangalia muda mrefu (long term)?

Mchezo ulikuwa hivi, NBC ilipigwa mnada, siku ya mnada Barclays - Uingereza na Absa - South Africa wakanyoosha mikono na Barclays kushinda lakini zengwe likapigwa kuwa wanataka kuchukua chao, hivyo akapewa Absa. Barclays akaenda kumnunua Absa hivyo akawa ameitwaa NBC Tanzania. Halafu pendekezo lao la Machi 2016 (sijui kama limepita) ni kuunganisha NBC Tanzania na Baclays Tanzania na kumaliza kabisa mechi (soma notes kutoka Wikipedia hapo chini).

NBC Tanzania 'About Us' page (angalia paragraph ya kwanza juu ya muda wa uzoefu wa benki hii) National Bank of Commerce - About NBC

Absa bank 'About Us' page Absa | Learn more about Absa Bank Limited

History[edit]
The bank traces its origins to 1967 when the Tanzanian Government nationalized financial institutions, including banks. In 1991, the banking industry was deregulated. Six years later, in 1997, the institution then known as "NBC" was split into three separate entities: (a) NBC Holding Corporation (b) National Microfinance Bank (NMB) and (c) NBC (1997) Limited. In 2000, the South African banking group Barclays Africa Group, at that time known as Absa Group Limited, acquired a majority stake in NBC (1997) Limited. The Government of Tanzania retained a 30% shareholding and the International Finance Corporation (IFC), a member of the World Bank Group took up 15% shareholding in the bank. The new entity became known as National Bank of Commerce (Tanzania) Limited.[4]

Merger[edit]
As at March 2016, Barclays Bank Plc. is seeking regulatory approval in Tanzania to merge this bank with Barclays Bank Tanzania in which Barclays maintains a controlling interest.[5]
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,220
2,000
Mkuu hapo ni kuunda tume nyingine ili kuweza kuichunguza ile TUME YA KWANZA
 

Joto Balaa

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,142
2,000
Kwa sasa tuache kupiga ramli. Walichofanya Barrick ni kuzuia kelele kuhusu makinikia ili kulinda heshima yao Kimataifa.
Hatua inayofuata ni mazungumzo ambayo naamini hayatakuwa nje ya kile kilichomo kwenye mkataba. Tusuburi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom