Vipeperushi Vyasambazwa Pemba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipeperushi Vyasambazwa Pemba.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 20, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WATU wasiojulikana wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbali mbali kisiwani Pemba vyenye ujumbe wa kuwataka watu wenye kuweka vikwazo kwa wananchi kujiandikisha wajitayarishe mwaka 2010 utakuwa ni wenye mateso kwao ikiwa wataendelea kuwapinga watu wanaotaka vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
  Afisa Tawala wa Wilaya ya Wete, Khamis Juma Silima alisema tayari wamepokea taarifa za kuwepo kwa kundi hilo lenye kusambaza vipeperushi ambapo vyombo vinavyohusika vinalifanyia kazi suala hilo.
  Alisema kwamba uchunguzi wa kina unafanyika kuhusiana na kundi hilo kabla ya hatua kuchukuliwa na watakaopatikana na hatia watachukuliwa sheria kali dhidi yao kwa kuendesha vitisho dhidi ya wananchi ambapo lengo alisema ni masheha.
  Afisa huyo alisema kwamba kundi hilo limeundwa kwa dhamira ya kufanya vitendo vya hujuma ambapo tayari wameanza kuwatisha baaadhi ya Masheha kutokana na msimamo wa viongozi hao katika kusimamia sheria ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
  Amesema Afisa Tawala huyo alisema kuwa kundi hilo ndilo linalohusishwa na kumwagia tindikali Sheha Mussa Kombo Omar ambaye ilibidi apelekwe kwa matibabu zaidi Unguja.
  Mbali ya hatua hiyo, kundi hilo linahusishwa na kufanya vitendo vya kutaka kuhujumu kazi ya usajili na utoaji vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na hivi karibuni limetoa vitisho kwa kumwandikia vipeperushi Sheha wa Shehia ya Kambini, Ali Said Ali.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Saleh Bugi alisema kwamba Polisi inatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi kinachotaka kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na kwamba wanafuatilia suala hilo.
  Kamanda Bugi alisema wamefanikiwa kupata moja wapo ya kipeperushi kilichosambazwa kwa Sheha wa Shehia ya Gando wakimtishia maisha.
  “Ole wako tukupate, tutakuua wejifiche, lakini 2010 ufikapo utaona” Alikariri Kamanda Bugi sehemu ya ujumbe kwenye kipeperushi alichotumiwa Sheha wa Gando.
  “Vipeperushi hivyo amekabidhiwa Mkuu wa Wilaya na anavifanyia kazi kwa sasa,”aliongeza Afisa Tawala Khamis.
  Bugi alisema uchunguzi dhidi ya kundi hilo linalojiita ‘kundi la kuhujumu masheha’ liliandika vipeperushi vya kumtisha sheha huyo na kwamba: “Usipokubaliana na mahitaji yetu kitakachokukuta usitulaumu.”
  Katika suala zima la usajili na utoaji wa vitambulisho katika wilaya ya Wete ambayo awali liliripotiwa kuwa na vurugu, kazi hiyo tangu Jumatatu iliyopita ilikuwa ikiendelea vizuri.
  Wakati huo huo watu wanane wakazi wa Kijiji cha Kiuyu Minungwini Mkoa wa Kaskazini Pemba jana wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na fomu za kughushi za Idara ya usajili Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kisiwani hapa.
  Watu hao walifikishwa Mahakamani mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Kaskazini Pemba, Makame Khamis wakituhumiwa kujipatia usajili huo kinyume na kifungu 312 cha sheria ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 2004.
  Mwendesha mashtaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Abdallah Issa Mgongo ameiambia Mahakama kwamba watuhumiwa hao Agosti 18 wakiwa katika Afisi ya Usajili wa Vitambulisho ya Wilaya ya Wete waliwasilisha fomu za kughushi kwa nia ya kutaka kupewa kitambulisho.
  Walioshitakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Bakar Hamad Ali (20), Fatma Ali Nassor(20), Bakar Khamis Haji(18), Saada Ali Pandu (22), Fatma Mohammed Ali(18), Sophia Said Salum(18), Fatma Malik Bakar(20) na Shamte Hamad (19).
  Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande hadi Septemba 2 wakati kesi hiyo itakapotajwa tena ambapo Mahakama itazingatia pia ombi la upande wa utetezi la kutaka watuhumiwa hao kupewa dhamana kwa mujibu wa sheria.
  Wakili wa washtakiwa, Ussi Khamis aliambia Mahakama kwamba wateja wake ni watoto wadogo na ambao ni wanafunzi hivyo, aliomba wapewe dhamana kwani kosa lenyewe sio kubwa kiasi cha kutopewa dhamana.
  Licha ya ombi hilo, Hakimu Makame Khamis alisisitiza kwamba Mahakama yake itazingatia na kutoa uamuzi wa ombi la dhamana Septemba 2, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
  Watuhumiwa hao ni wanafunzi wa Shule mbali mbali katika Jimbo la Ole, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  HII IMETOKEA LEO BAADA YA SALA YA IJUMAA, WATANGANYIKA KAZI KWENU

  [​IMG]
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kimesambazwa na baadhi ya watu leo baada ya sala ya Ijumaa Malindi
   
 4. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ?????
   
 5. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mambo yamekuwa mambo, fujo hiyooooooo iko njiani.
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  tehe tehe tehe nimeipenda hii "umoja wa wazalendo unapenda kuwakumbukusha wazanzibari na waislamu kwa ujumla....

  alafu mwisho akamalizia na hii .....umoja wa wazalendo unawaomba.....wazidishe juhudi katika kuunganisha umma wa kizanzibari ili tuwe wamoja......
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mbogela unaugonjwa wa macho nini mbona wenzio wanasoma vizuri tu.
  Naona huku visiwani moto umesambazwa.
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nina Hakika Zanziber pamoja na nia waliyo nayo ya kujitenga .... Hawatabaki salama. Wataendeleea kugawanyika.

  Siamini Tanganyika na WAKOLONI kwa Zanziber. Mtizamo huu sio stahili kabisa.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivyo vikaratasi vinasemaje mbona ni jambo la kawaida tu kutokea kwa vikaratasi huko uzenjini au vina ujumbe mkali ,hebu weka sawa tuangalie kwenye data zetu kama zinalingana na habari hizo.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wazanzibar wanaichukulia Bara ambayo ni Tanganyika kama wakoloni weusi. Hii dhambi ya kuanza kubaguana kama hivi ikisha ingia damni sijui tutaelekea wapi? Wengine tunatarajia kuchumbia znz.
   
 11. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ujumbe kama unavyosomeka mazee, au niuite waraka may be
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ni chembechembe za udini hizi
   
 13. K

  Kelelee Senior Member

  #13
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .....confusion at it's best
   
 14. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ..............sijawaelewa wataka nn hawa au ni........
  `kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji`
   
 15. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  si wajaribu tuone, hawa wazanzibar/waislam wana matatizo sana huwa wanapenda sana kufanya fujo mara wanapotoka misikitini, huwa najiuliza bila majibu huko huwa wanaenda kuswali au kupanga mikakati ya kufanya fujo
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  He, vereje???
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Naona hii ni kazi ya mtu mmoja; tena mwanasiasa aliyrchoka. Mtu yeyote anaweza kuandika na kutoa nakala kadhaa kisha kusambaza.
   
 18. K

  Koba JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...waachieni nchi yao,kushindwa kwa CUF miaka yote ni matokeo ya siasa za mafisadi wa CCM bara wakishirikiana na wenzao wa visiwani,nina uhakika majority ya hawa watu wanataka nchi yao na hawataki muungano na bara,sijui tatizo ni nini...isije ikawa vurugu kama Ethiopia/Asmara then after 40yrs and death of millions ndio asmara wakapewa nchi yao,kuna umuhimu gani wa haya matatizo?
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Haya akili kichwani mwenu. Kwani siku zote viongozi wa juu wa Znz wanachaguliwa Dodoma, hata raisi wa awamu ya pili mzee wetu Aboud Jumbe alipojaribu alizimwa Dodoma.

  Sasa muwe makini ni ukoloni mkongwe.
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Na mimi napenda kuwakumbusha Watanzania na wananchi wote kwa ujumla kwamba lengo la genge hili linalojiita Umoja wa wazalendo, Zanzibar, ni kutugawa Watanzania. Tujihadhari sana na kikundi hiki.
   
Loading...