Tatizo la vipele vinavyotokana na kunyoa nywele kichwani chini ya kisogo (Acne Keloidalis Nuchae)

Kuna dawa inaitwa gentriderm iko kitube kidogo hivi inauzwa 2000 mpaka 3000 pharmacy, jaribu hiyo ...na usiache hospital kwenda .. na pia kama itawezekana nunua mashine yako ya nywele ukienda salun nenda nayo kuepuka kutumia zao na kubeba maambukizi..
 
kaka asante kwa ushauri wa tiba, sasa hiyo tiba dozi yake ipoje? namaanisha nioshe kwa siku mara ngapi na kwa muda wa siku ngapi??? asanate sana MziziMkavu

Dr, mchanganyiko unatakiwa uweje i.e uwiano wa maji na swaumu? Na upakaji ni kwa muda gan mkuu? MziziMkavu.
Kitunguu saumu kiwe kimoja kizima maji ya kuweza kuosha sehemu yenye hivyo vipele na uwe unatumia Asubhi na jioni mpaka hapo utakapo pona.
 
Ukinyoa nywele Usichonge maeneo hayo yaliyo na vipele,zipunguze tu. Huu uwe utaratibu wako muda wote unyoapo nywele. Taratibu vitaanza kupungua na hatimae kutoweka. Mimi nilikuwa navyo lakini baada ya kufwata njia hii vilitoweka kabisa,sikutumia dawa yoyote!
 
habari wadau..
Katika kunyoa nywele kichwani imenitokea nimeota vijipele nyuma ya kichwa karibu na shingo. sasa kila nikienda pharmacy na dispensary wananipa dawa ambazo zimeshindwa kunisaidia. Hali hii imekuwa ikinikosesha raha sana, nimepanga kwenda hospitali kubwa lakini nimeona kabla sijaenda huko inawezekana kuna mtu akanipa ufumbuzi rahisi wa kuweza kutatua tatizo hili. Kwa yeyote mwenye ufumbuzi wa kuondoa vijipele hivyo naomba anisaidie.

Wasalaam
Ndugu yangu huu ugonjwa usije ukauchekea. Hivi vipele ni ugonjwa mkubwa na unajitaji matibabu ya madaktari wazuri hizi phamacy watakumalizia prsa yako bure na ninachokuomba ni wewe kuwahi kuutibu huu ugonjwa usje ukachelewa kwani hivyo vipele vinasambaa.
 
Mcheki Dr IZACK wa Clouds aliwai kuizungumzia hii ishu,tatizo la ujaaji wa nyama
 
kuwa makini na saluni sikuhizi kuna spirit za kutengeneza mtaani na nyingi ndizo zachangia hayo madhara
 
Kuna uzembe wa hii serikali yetu,tangu mambo za mashine za umeme za kunyolea zimeanza hili tatizo limesha wakumba watu wengi sana,lakini sijawahi kusikia tamko la wizara ya afya kuhusiana na maradhi haya ambayo bado yanaendelea kuwakumba watu wengi.Ni tatizo na lipo lakini hakuna tahadhari yoyote inayotolewa kwa wateja wa hizo salon.Mimi nilishawahi kupata hivyo vipele lakini kwakuwa ni muoga wa kuumwa nilivipasua vyote na vilipoanza kukauka nikapaka Betacort-N mpaka vilipopotea,mpaka leo takribani miaka 4 havijanirudia tena na ninachofanya nikienda kunyoa sichongi nywele nyuma ya kichwa kwa mashine zao,badala yake huwa natumia nyembe za disposable za kunyolea ndevu zinazouzwa 1000/- only.TRY THIS.
 
Dah huo ugonjwa mm mwenyewe unanisumbua huu ni mwaka wa tatu sasa na nimetumia madawa kibao wala hauonyeshii dalili ya kuisha na vinakua jaman cjui hata nifanyejee
 
Me Nina tatizo la vipele kichwani nimetumia Dawa Nyingi sana bila mafanikio Kwa hyo kuvifubaza huwa natumia Gentresone tatizo ni takribani miaka sita sasa naomba kama kuna Dawa inaweza nisaidia nijulishwe.
 
mkuu kuna dawa inaitwa gentlemen after shave ina maliza hilo tatizo kabisa vinatoa damu au usaha
 
Back
Top Bottom