Vipele vinavyotokana na kunyoa nywele Kichwani (Karibu na Shingo) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipele vinavyotokana na kunyoa nywele Kichwani (Karibu na Shingo)

Discussion in 'JF Doctor' started by MyTanzania, Oct 21, 2008.

1. MyTanzania

MyTanzania Senior Member

#1
Oct 21, 2008
Joined: Sep 9, 2008
Messages: 107
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Ndugu zangu ndani ya JF habari zenu.

Mimi nina matatizo ya vipele mwisho wa nywele za kichwani upande wa kisogoni ambavyo vinatokana na kunyoa.

Nimepata ushauri kwa madaktari mbalimbali juu ya dawa za kutumia bila mafanikio.Kama kuna mtu anajua ni namna gani naweza kutibu na pia kuzuia visitokee tena naomba tuwasiliane humu JF.

Nimeona watu wengi hivi karibuni wamekuwa na hali hiyo ambapo baadhi inapelekea kuota nyama kubwa baadaye.Naomba anayejua asaidie,maana najua watu wengi wanahangaika sana kuutibu ugonjwa huo sasa.

Nitashukuru kwa mtu yeyote aliye tayari kutoa msaada wa ushauri na hata kama kuna dawa aiandike humu niitafute.

Asante.
2. Steve Dii

Steve Dii JF-Expert Member

#2
Oct 21, 2008
Joined: Jun 25, 2007
Messages: 6,417
Likes Received: 49
Trophy Points: 145
Pole sana ndugu kwa tatizo hilo linalokusumbua.
Napenda kuuliza je ukiacha bila kunyoa muda mrefu vipele hivyo bado vinajitokeza, au ni pale tu unaponyoa?

3. Yo Yo

Yo Yo JF-Expert Member

#3
Oct 21, 2008
Joined: May 31, 2008
Messages: 11,254
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Wembe zinaleta vipele jaribu kutumia mashine ya kwako peke yako......

4. Steve Dii

Steve Dii JF-Expert Member

#4
Oct 22, 2008
Joined: Jun 25, 2007
Messages: 6,417
Likes Received: 49
Trophy Points: 145
Kweli kabisa, miye situmii nyembe hata kidogo.... na kwa ma barbers ndiyo kabisa usipoangalia unaweza jikuta unarudi na magonjwa ya kila aina ya ngozi.

Naona hajapata chance ya kujibu swali langu nililomuuliza hapo mwanzo...

Nilitaka ku-suggest ajaribu pia njia nyingine abstract; afuge rasta. Huwezi jua, kunaweza kumsaidia.

5. MyTanzania

MyTanzania Senior Member

#5
Oct 22, 2008
Joined: Sep 9, 2008
Messages: 107
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Nashukuru Steve D na YO Yo kwa kuonyesha concern.Nisiponyoa muda mrefu haviendelei kuota,ila sasa shughuli ninayofanya hainiruhusu kufuga rasta,ningekuwa nina shughuli yangu mwenyewe ningefuga,kwani hili tatizo limekuwa kero sana kwangu.
Nimenunua mashine yangu mwenyewe lakini nadhani tatizo liko pale pale kwenye nyembe.Ila kuna mtu kanishauri nitumie mkasi kunyoa lakini sijapata mtaalamu wa hiyo nyenzo maana vinyozi wengi siku hizi wamesahau kutumia kifaa hicho ambacho tulitumia zamani.
Asanteni sana,bado nasubiri ushauri zaidi.

6. Steve Dii

Steve Dii JF-Expert Member

#6
Oct 22, 2008
Joined: Jun 25, 2007
Messages: 6,417
Likes Received: 49
Trophy Points: 145
MyTanzania, samahani natoka nje kidogo ya mada, kwanini lakini rasta hawaruhusu sehemu unayofanyia kazi?!

7. M

Muha New Member

#7
Oct 22, 2008
Joined: Sep 2, 2008
Messages: 2
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Pole sana kwa tatizo la vipele. Jaribu kutumia maji ya moto sana kila baada ya kunyoa kujikanda kwenye hizo sehemu. Nilipata huo ushauri toka kwa rafiki yangu nikaujaribu kwa mtu ukakubali. Hata kama unapata hilo tatizo ukinyoa ndevu, jaribu kutumia maji ya moto sana kila unaponyoa unajikanda na tatizo litakwisha. Ukifanikiwa saidia na wengine.

8. K

Kipanga JF-Expert Member

#8
Oct 22, 2008
Joined: Apr 24, 2008
Messages: 680
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
My Tanzania,

Tatizo unalozungumzia limeshawakumba watu wengi na hasa wale wanaopenda kunyoa nywele zote kichwani (kipara). Kitu ninachoweza kukushauri unapokwenda kunyoa salon punguza nywele kwa kiasi cha kutumia kitana kidogo kabisa ambacho nadhani ndio size ya mwisho kuchania. Pia mwambie kinyozi kuwa asikuchonge sehemu ya nyuma ya kichwa na hasa hayo maeneo zinapoishia nywele kuna uwezekano mkubwa ukaepukana na hili tatizo. Kuna siku nilihama salon baada ya kukuta mtu ananyolewa na ana vipele mwisho wa nywele then kinyozi akapitisha mashine pale ni damu kwa kweli nilistuka sana na hapo nami nikapata wazo la kununua mashine yangu mwenyewe!!!

9. MyTanzania

MyTanzania Senior Member

#9
Oct 22, 2008
Joined: Sep 9, 2008
Messages: 107
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Steve D
Tatizo la mabepari hilo inabidi tukubali tu kwakuwa tunataka cha uvunguni otherwise tunatakiwa kuwa watu huru.
MUHA
Nashukuru pia kwa ushauri wako,leo ninaanza kuutumia na ukinisaidia nitasaidia wengine pia.Asante saaaaaaaaana
KIPANGA
Nashukuru kwa ushauri wako,nitaanza kunyoa nabakisha nywele kwa kutumia mashine yangu mwenyewe.
Asanteni sana nikifanikiwa nitalirudisha humu JF ili wengine nao wafaidike na ushauri mlionipa.

10. u

uporoto01 JF-Expert Member

#10
Oct 25, 2008
Joined: May 23, 2008
Messages: 4,742
Likes Received: 13
Trophy Points: 135
Kuna jiwe linaitwa shabu kama chumvi ya mawe hili linaondoa tatizo kabisa,unachovya kwenye maji na kupaka baada ya kunyoa.Saloon za wahindi mjini zote hutumia.

11. KakaJambazi

KakaJambazi JF-Expert Member

#11
Jan 11, 2011
Joined: Jun 5, 2009
Messages: 13,531
Likes Received: 1,765
Trophy Points: 280
Mi huwa natoka vipele kisogoni. Nomba mnisaidie jinsi ya kutibu.

12. Humphnicky

Humphnicky JF-Expert Member

#12
Jan 11, 2011
Joined: Dec 1, 2010
Messages: 1,619
Likes Received: 355
Trophy Points: 180
acha kukwangua ukienda saluni kunyoa.
wewe una alergy na metal

13. b

blackgold New Member

#13
Aug 25, 2011
Joined: Aug 25, 2011
Messages: 2
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Wadau kuna hivi vipele sugu nyuma ya kisogo,,vinasumbua sana kwa mda sasa,,ipi dawa yake na wapi naweza kutibiwa?

14. Brooklyn

Brooklyn JF-Expert Member

#14
Sep 4, 2011
Joined: Mar 17, 2009
Messages: 1,452
Likes Received: 25
Trophy Points: 135
Wakuu naombeni msaada, nina sumbuliwa sana na vipele vya chini ya kisogo, yaani vinaniwasha mpaka nakosa raha. Mwanzoni nilifikiri vinatokea kwa sababu ya kushare mashine za kunyolea salon na nikaamua kununua mashine yangu lakini vipele bado havijaisha.

Naombeni ushauri wakuu nitumie dawa gani ili niweze kuondokana na vijipele hivi? Maana siwezi acha kunyoa nywele moja kwa moja.

Natanguliza shukrani.

15. NEW NOEL

NEW NOEL JF-Expert Member

#15
Sep 4, 2011
Joined: May 21, 2011
Messages: 816
Likes Received: 82
Trophy Points: 45
Kwa ushauri wangu,ningekushauri uwe unanyoa katika saloon moja au mbili yaani usiwe unanyoa katika saloon nyingi sana. Na ili vipungue kuna sabuni inaitwa ''Kopacabana black spot soap'' ni nzuri. Inauzwa katika maduka ya cosmetics(vipodozi). Ni sabuni nzuri unatakiwa uwe unaitumia kunawa nayo kila asubuhi na jioni. Jambo jingine muhimu ni kuacha kuchonga nyuma.
Ila kwa ushauri zaidi waone madaktari bingwa wa ngozi.

16. Brooklyn

Brooklyn JF-Expert Member

#16
Sep 4, 2011
Joined: Mar 17, 2009
Messages: 1,452
Likes Received: 25
Trophy Points: 135

Asante kwa ushauri wako mkuu, ngoja nifanye mpango wa kuonana na madaktari wa ngozi. Kuhusu kuchonga nyuma, huwa sichongi kabisa.

17. J

Juma. W Senior Member

#17
Sep 4, 2011
Joined: Mar 28, 2011
Messages: 131
Likes Received: 0
Trophy Points: 33

pole mshikaji. Mimi pia nina tatizo hilo ila kuna epidem cream imenisaidia sana. Pia kuna coaltar moja nadhan inaitwa polycoaltar ipo kwenye phamasi. Pole sana

18. Chimunguru

Chimunguru JF-Expert Member

#18
Sep 4, 2011
Joined: May 3, 2009
Messages: 9,826
Likes Received: 216
Trophy Points: 160
Jaribu Candiderm nayo nzuri sana

19. HAZOLE

HAZOLE JF-Expert Member

#19
Sep 4, 2011
Joined: Feb 25, 2011
Messages: 1,318
Likes Received: 45
Trophy Points: 145
see the dr

20. Brooklyn

Brooklyn JF-Expert Member

#20
Sep 4, 2011
Joined: Mar 17, 2009
Messages: 1,452
Likes Received: 25
Trophy Points: 135

mkuu hizi epidem cream si nasikia zinafanya uwe mweupe? Hebu nipe uzoefu wako mkuu, wewe haijabadilisha rangi ya ngozi yako?

Loading...