Vipaumbele vyetu ni nini…Nyumba ya Gavana (HAPANA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipaumbele vyetu ni nini…Nyumba ya Gavana (HAPANA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkongo, Dec 26, 2009.

 1. mkongo

  mkongo Member

  #1
  Dec 26, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikiangalia baadhi ya habari na imenisikitisha sana Uamuzi wa Gavana wa Tanzania kutumia fedha nyingi kukarabati/kujenga nyumba ya kuishi YEYE. Yaani kupewa tu nafasi hiyo anataka aishi nyumba ya kifahari. Je alikuwa wanaishi kwenye nyumba ya kifahari kabla ya kupewa cheo hicho? Ingekuwa fedha hizo zinatoka mifukoni mwake angejenga nyumba hiyo ya kifahari? Hakuna mtu asiyependa maendeleo lakini tuwe na huruma, hivi wewe GAVANA hujaishi maisha ya mtanzania ya kijijini? Huoni shida wanazopata wananchi wa kijijini? Na sio tu kijiji mijini pia kuna shida pia ambazo Serikali inasikilizia kutatua. Inaweza kuwa Benki Kuu labda haihusiki moja kwa moja na kutatua matatizo ya mwananchi basi Vipaumbele vya Benki kuu nini? Kujenga nyumba ya Gavana? (Jibu langu ni HAPANA lakini la Prof.Ndulu ni NDIYO). Waliomweka huyu Prof. Ndulu madarakani wanasemaje kuhusu suala hili? Tumekaa kimya tunawasubiri waseme… wanatakiwa kuwajibika kwetu kwa hiyo tunawasubiri. Tanzania ni nchi ya ajabu baadhi wa watu wachache (Viongozi) wenye madaraka na nguvu wameamua kujifanya wenyewe sio sehemu ya Matatizo ya Watanzania. Angalia

  1.Tatizo la barabara mbovu (Wanajinunulia mashangigi). Mwananchi wa kawaida shauri yako

  2.Uduni wa shule zetu (Wanasomesha watoto nje ya nchi). Mwananchi wa kawaida shauri yako

  3.Uduni wa mahospitali na huduma za afya (Wanaenda nchi za nje kutibiwa) Mwananchi wa kawaida shauri yako

  4.Umeme unakatikakatika (Wana majenereta au haukatwi sehemu wanazoishi). Mwananchi wa kawaida shauri yako

  5.Orodha inaendelea

  Ewe Kiongozi wa Tanzania ACHA UBINAFSI na yule aliye kijiji au anayepata hizo shida ni Mtanzania/binadamu kama wewe. Ulichaguliwa au kupewa hayo madaraka kumtatulia shida zake na sio shida zako. Ni hayo kwa leo wajameni.
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ubinadamu kazi ndugu yangu.
  Tuendelee kumuomba MWENYEZI MUNGU ATUPE MOYO WA UJASIRI WA KUWAELEZA VIONGOZI WETU PIA NAO VIONGOZI WAONE NA KUJALI SHIDA ZETU
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi hizi nyumba zitajengwa ngapi? Akija kila gavana mpya anajengewa nyumba mpya?
   
 4. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu kimoja kinanichanganya hapa. Hivi hicho kiasi cha fedha ndio amepewa contractor kama down payment afanye hayo marekebisho au ndio gharama za project nzima? Maana kama nimeona mahali kuwa hicho ni kianzio tu.
   
 5. e

  echonza Senior Member

  #5
  Dec 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vyovyote itakavyokuwa bado si halali kutumia kiasi hicho cha shilingi bilioni 1 kujenga nyumba ya familia moja tu wakati watanzania wengine wanakufa na njaa vijijini. Uchoyo gani huu Ngulu ameuonyesha? Mimi nafikiri utaalamu wake wa uchumi angetusaidia kupunguza pengo kati ya wasio nacho na wenye nacho, lakini yeye ndiyo kabisa amefaya liongezeke kadri siku zinavyozidi kwenda. Tangu aingie BOT:
  1. masikini wanaumia na mfumko wa bei;
  2. amepitisha wafanyakazi wa BOT pekee yake wapate mikopo nafuu (madhara ya hili ni kwamba, pamoja na kwamba wao pia ni watumishi wa umma, kutokuwa na pengo kubwa kati ya wao na watumishi wengine wa umma kiuchumi);
  3. ameruhusu matumizi hayo makubwa ya fedha kujenga nyumba ya kuishi yeye pekee kiasi kisichopungua bilioni 1.

  Mtu wa namna hii ni hatari sana kwa nchi inayofikiria kujikwamua kutoka kwenye umasikini unaoongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kutoka Tanganyika ilipopata uhuru wake.

  Ili watanzania wawe na maisha bora (high standard of living), hatua ya kwanza kabisa ni kuwekeza katika miradi itakayochochea kukua kwa uzalishaji nchini. Na moja ya vichochezi hivyo ni kuwekeza fedha kama hizo kwenye miradi mbalimbali itakayoajiri watanzania, na kuongeza uzalishaji chakula na mazao ya biashara na siyo hili la kujenga nyumba za gharama kiasi hicho wakati nyumba ikishasimama itadai matumizi zaidi ya fedha za walipa kodi bila kutuzalishia chochote cha ziada.

  Baada ya kuongeza uzalishaji wa mazao na huduma nchini, pato la taifa liweze kugawanywa kwa usawa kabisa na ikiwezekana sehemu ambazo ziko nyuma zipate kingi zaidi ili kuweza kulingana na mikoa mingine iliyopiga hatua kimaendeleo (mikoa duni kiuchumi Kigoma, Rukwa, Tabora nk). Juhudi hizi zitakuwa za kuendelea kabisa baada ya nchi kuwa na vipaumbele vyenye kueleweka kwamba zinatatua matatizo ya watanzania walio wengi nchini.
   
 6. M

  Manji Supporter Member

  #6
  Dec 27, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  If we buy food for the hungry people, next month or next year they will be hungry again. On the other hand, the governor's house is an asset that will yield a profit for a long time. Think people don't just complain because you are jealous someone has something and you don't. You want BOT governor to live in Uswazi like you? Never. We will keep doing what we are doing and if you don't like it go jump in the ocean. Let adults run the government as they see fit.
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  mwenye shibe hamjui mwenye njaa, mtaanzisha mapambano msiyoweza kuyamudu.

  Makaburu kule SA walikuwa na uongozi mkali usio na mfano lakini vita vilivyoanzishwa na akina Mbeki kisha akina Steve Biko ilibidi wakubali kushindwa.

  Mabutu Seseseko aling'olewa madarakani kwa aibu hivi hivi, Mzee Mugabe anaishi kwa shida na taabu kwa sababu kama hizi. mifano ni mingi, hitimisho ni kwamba ufisadi, ubaguzi unaleta vuguvugu za ukombozi, uharamia na vita vya wenye kwa wenyewe. Hakuna amani ya uongozi ktk mitazamo uliyonayo.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Your name itself speaks volumes!
   
 9. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ngojeni niwaibie siri naona wengine humu mnarusha mdongo tu bila kujua!

  hiyo nyumba (na nyingine kadhaa) ni kwa ajili ya kuwakopesha viongozi wakuu wa BOT baadaye. habari imevuja baada ya ukarabati mkubwa kufanyika, lakini mpango ni kuwa zikarabatiwe na kukopeshwa watendaji wa BOT kabla hawajastaafu uli kuwawezesha kumiliki nyumba bora zianzoendana na hadhi zao na utumishi wao. huu ni sehemu ya mpango wa kuwakopesha watumishi wa taasisi hiyo nyeti nchini mikopo ya fedha taslimu kwa ajili ya kujijengea makazi kama ilivyotokea katika magazeti hivi karibuni.

  nadhani sasa imeeleweka

  japo si sahihi kutumia hela zinazolingana na vijisenti vya chenge huko UK kudai eti ni ukarabati tu, lakini hata hivyo msisahau uchaguzi umekaribia!!!!
   
 10. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sijui kitu gani kitokee kwa viongozi wa bongo manake priority ziko wazi lakini hawa majamaa wanajifanya kama hawaelewi vitu wanavyotaka watanzania nadhani tuombe sana ili hawa mabwana wakubwa wasiendelee kujenga majumba kama haya .Inasikitisha sana haya kutokea katika nchi maskini kama hii
   
 11. a

  alles JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2009
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio maana yake...kila gavana mpya nyumba mpya.Si hajabu baadae atainunua kwa 5million na kua nyumba yake binafsi.
   
 12. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Tusisahau kwamba dynamic ya Serikali yatu inatokea kwa masangoma. Hamuoni hizo nguvu za utendaji kazi wa Serikali kwa mwaka ujao zimeanza kuchochewa kutoka ofisi ya mnajimu? Nchi ina vipaumbele ila cha kushangaza havifuatwi na wananchi kwa sababu ya kunyimwa elimu ya kujitambua ndio basi tumekuwa zoba hakuna reaction. Cha kujiuliza ni je serikali haina nyumba kwa ajili ya waandamizi wake? Na kama zipo mbona basi kila kiongozi mwandamizi anapoteuliwa anajengewa nyumba tena ya kufuru? Hii ni rushwa ya kumpumbaza mteule wa rais asi tizame ufisadi unaofanywa kwenye taasisi husika. Ndulu keshapumbazwa na ndio kawakopesha wafanyakazi wa Bot mamilioni kibao kwa masharti nafuu ili nao wamnyamazie maana mate yashamdondoka na tayari keshaanza kuimega keki ya taiafa bila hata kunawa mikono. Mfumoko wa bei umefikia kiwango cha juu kabisa na ni kama haimhusu. Nasema huu uzumbukuku na ofisadi wa serikali yetu kuwajengea mahekalu na kuwanunulia magari ya kifahari watendaji wake pindi wanapoingia ofisini ukome. Kuwe na utaratibu wa kuwa na vitendea kazi ambavyo mwajiriwa atavikuta na kuviacha kwa mwingine pindi anapoiachia ofisi. Alaa!!! Umasikini gani huu wa kujitakia hadi hata mji mkuu mahala serikali inakaa kuna wanafunzi wamekosa viti wanakaa sakafuni???
   
 13. A

  August JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Muzee kuna mahali umetoroka? unajua investment property inakuwa treated namna gani na property ya matumizi ya kawaida zinakuwa treated tofauti?
  Hiyo itakuwa kwenye asset register ya BOT kama ni Nyumba ya matumizi ya Governor na kutunzwa na watu wa Administration, wakati Investment Property itakuwa kwenye Register ya Investment Portfolio ambayo itashikiliwa/kutunzwa na Investment department, sasa kwa akili yako investment gani huwa kwenye asset register ya Administration?
  Kwa maelezo zaidi wasiliana na NBAA wakueleze zaidi.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  good point mie ndio maana saa zengine siangalii jamiiforum kuna watu wanakurupuka tu kusema wakijidai wao wataalamu kumbe wazimu mtupu kama huyu Manji Supporter.
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,085
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Hiyo nyumba iliyoonyeshwa thamani yake haifiki 1.4 bio. labda kama ina ma-sink ya dhahabu ndani kama nyumba ya Marehemu Saddam Hussein huko Baghdad. CAG waende kukagua thamani halisi ya nyumba ile na TAKURURU wakae mkao wa kula!
   
 16. M

  Manji Supporter Member

  #16
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  An asset is anything that can be easily converted into cash. The governor's house is an asset and a very valuable one due to its location. If we sell the house today, taxpayers will make a profit. End of story.
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  ukirudi kwenye post yako utaona umeandika nyumba ya governor ni asset which will yield a profit, in that context hiyo ni investment, ambayo imewekwa/kununuliwa kwa objective ya ku-yield profit. na kama unataka kuzungumzia kitu kuwa an asset hata treasury bill is an asset, hata deposit is an asset tena hizi zingine ni risk free kuliko a house, maana unaweza usipate hiyo hela kama tunavyo ona kwenye kipindi cha recession.na zaidi ya hapo ikiwa construction cost zilikuwa inflated.
   
 18. mkongo

  mkongo Member

  #18
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la nyumba sio la Benki kuu peke yake. Watanzania wangapi wanapanga? Hawana uwezo wa kujenga nyumba. Na inawezekana kabisa kuna watanzania wengine wenye uwezo wa kufanya kazi Benki kuu lakini kwasababu nafasi hazitoshi na sio wote tutapata nafasi Benki kuu. Serikali ilitakiwa kuanzisha mpango wa kujenga nyumba na kuwapa wananchi na warudishe gharama za kujenga kwa kulipa kodi ya mwezi. Wanapofikisha kile kiwango kilichotumika kujenga nyumba basi wanapewa umiliki wa nyumba hiyo. Na hii iwe fursa ya mwananchi yoyote sio tu kwa wafanyakazi wa Benki kuu. Mfanyakazi wa Benki kuu analipwa hela ya kutosha... anaweza kabisa kujenga nyumba yake mwenyewe. Lakini nakumbuka ule usemi usemao aliyenacho ataongezewa. Pia nashangaa kwamba Waziri husika amekaa kimya hii inamaanisha kwamba huu ni mpango wao. Tutafika kweli? CCM kwanini umenifikisha hapa? CCM kwa nini umenikataa mimi mwananchi? CCM kwanini unanitenda?
   
 19. G

  Genda Member

  #19
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyumba yenyewe ya miktadha ya nchi za baridi...tazama hayo mawe yaliyojenga sakafu hapo nje!

  Wakati wa jua kali, mazingira yatakuwa ya moto...lakini ndani shauri ya poesa za wananchi kuna airkondishina!

  Hivi ni madawati mangapi yangetengezwa kwa ajili ya shule zetu?
   
 20. M

  Manji Supporter Member

  #20
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Who told you treasury bill and deposits are risk free? Or better yet who told you they are less risky than a buying a house in a prime area like Oysterbay?
   
Loading...