Vipaumbele vya bajeti mwaka wa fedha 2017/2018 vitabadilisha maisha ya Watanzania?

Tuna Mavi-ongozi yanayoamini kwamba maendeleo ni kwenye vitu na siyo kwenye human security and development! Twafaaaaaaa,, na wachumi-a-tumbo wetu wanamwogopa mkulu kama ukoma! Naamini hata akiyaangalia usoni huwa yanainamisha vichwa!
Hahahahahahaha....hilo neno la juu kabisa limekua ni mbadala wa hili pia vio-ngozi
 
Wa ndugu naleta kwenu vipaumbele vya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 ambavyo vimetajwa na waziri wa fedha. Vipaumbele hivyo ni.
1.Ujenzi wa Reli
2.Kuhuisha ATCL
3.Ununuzi wa ndege
4.Mradi wa Liganga
5.Kuhamia Dodoma
6.Kuanzisha kanda maalumu za kiuchumi.
Je kwa vipaumbele hivi maisha ya mtanzania yatabadilika ukilinganisha na hali ilivyo sasa??!
Kaman mie ndiyo upeo wangu mdogo au? Kwa budget hiyo mbona kama Wizara ya Ujenzi itachukua almost more than 50% ya budget nzima? Hii haraka haraka yote ya nini jamani?

Hayo mapesa mengine si yangepelekwa wizara nyingine pia
 
Doh,
kilimo hakijapewa kipaumbele.?
Afya jee.?,
vipi kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama.?

Vipi kuhusu Makazi bora kwa raia.?

Hivi binafsi niliona kama vinapaswa kuwa vipaumbele kwa sasa.

Ingawaje kwa vipaumbele hivyo natabiriKwa mfumuko wa bei kupungua na ugumu wa maisha kwa raia wa kawaida kuongezeka mara dufu.
Siku zote huwa ni hivi vyako.....na maisha hayajawahi kubadilika.....
 
ni kweli ukilitazama moja kwa moja hauwezi kuona kama ndege zinamsaidia maskini lakini zinamsaada mkubwa sana kwake kwa njia moja au nyingine na hasa tukiangalia huko nyuma sekta ya usafiri ilikuwa inaongoza kwa uchangiaji mkubwa kwa pato la taifa.
wakati mwingine kuna vitu tunavihitaji si kwa sababu vinaumuhimu sana kwetu lakini kwa kuwa muda umefika kuwa navyo. mfano mtu wa kawaida kabisa wa kijijini haitajisana simu ya mpanguso ukilinganisha na mahitaji yake lakini ikizingatiwa hana umeme na muda wa kutumia simu kwa muda mrefu.
hivyo wacha tuwe nazo zinaweza kuchangia kukuza hata utalii siku zijazo
Unachosema kwenye ndege nnaweza kukubaliana kiasi na wewe. Ila tungekuwa na subira kidogo tukaangalia hata performance ya hizi mapanga nshaa za saa hivi. Halafu hiyo pesa wanayotaka kukimbilia kununua ndege nusu ingepelekwa wizara ya Maji na nyingine Afya maana huko ndiyo unamgusa mwanachi wa hali ya chini kabisa then budget ya mwakan wanunue walau ndege 1 afu pesa nyingine wapeleke kwenye umeme
 
nakubaliana na wewe kabisa kiukweli hii risk inayochukuliwa hapa inatisha ikifanya vizuri tunaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kugharamia hizo huduma kwa ufanisi ila ikifeli tutatafutana! kinachoonekana tajiri ananunua ndege apate hela na hela ndizo zigharamie hayo uliotaja.
nikama nilivyosema wakati mwingine tunafanya vitu ambavyo ni muhimu lakini si kwa muda wa sasa na hii inachangiwa na watu wanaotuzunguka wakoje na sisi tukoje wakati mwingine unalazimisha kufananafanana na wenzako japo unaelewa kabisa sio kweli.
mfano mzuri ni ununuzi wa magari kwa watu ambao wanajua hawawezi kumudu mafuta likini wamezungukwa na watu wote wanamagari tena wengine hawana kipato kikubwa kuzidi wao hivyo na wao wanaamua kuingia mikopo na matokeo yake bajeti ya ndani inayumba. sawa na ada za shule kwa shule za kishua! wengi zinawapa malalamiko mno! ndivyo nasi tulivyo sasa kama utakumbuka hata ununuzi wa rada ulitusumbua lakini kilichokuja nyuma yake kilituumiza sote ngoja tuone na hiki
 
ni kweli ukilitazama moja kwa moja hauwezi kuona kama ndege zinamsaidia maskini lakini zinamsaada mkubwa sana kwake kwa njia moja au nyingine na hasa tukiangalia huko nyuma sekta ya usafiri ilikuwa inaongoza kwa uchangiaji mkubwa kwa pato la taifa.
wakati mwingine kuna vitu tunavihitaji si kwa sababu vinaumuhimu sana kwetu lakini kwa kuwa muda umefika kuwa navyo. mfano mtu wa kawaida kabisa wa kijijini haitajisana simu ya mpanguso ukilinganisha na mahitaji yake lakini ikizingatiwa hana umeme na muda wa kutumia simu kwa muda mrefu.
hivyo wacha tuwe nazo zinaweza kuchangia kukuza hata utalii siku zijazo

Mkuu Mipango ya Serikali iko wapi mpaka kila mwaka inakuja na vipaumbele vipya vikubwa? Kila mwaka serikali inabadilisha vipaumbele. Kama mtindo ni huu subiri mwakani vipaumbele vitabadilika. Kwanini serikali isiwe na comprehensive programs za kutimiza muda mrefu. Hizi program ziwe agenda za miaka mitano au kumi. Hatari iliyopo ni kwamba miradi inayoanzsishwa ni haiwezi kukamilika hata siku moja kwa sababu the government keeps on changing its priorities. Huwezi mfano kukamilisha ujenzi wa reli kwa mwaka mmoja, kufanya kampuni ya ndege kusimama kwa bajeti ya mwaka mmoja. Lack of clear vision, plans and strategies lead to waste of public resources. Kuna mifano kibao ya miradi iliyoanzishwa na kuachwa kwa kinachoitwa vipaumbele kila bajeti inapoandaliwa. Mfano unasikia nini juu ya SAGCOT kwenye Kilimo, Kilimo Kwanza imefika wapi..Hivi lile jengo la Machinjio ya kisasa pale Ruvu limefikia wapi,...nk, Hivi bandari ya kisasa ya Bagamoyo imeishia wapi...na je Katiba Mpya imeishia wapi..nk. Eti wanaanzisha tena Kanda Maalum za Kiuchumi....Je hizi ni tofauti na EPZ ambazo JK alianzisha au ni hadithi zingine?

Ningefikiri waje na clear strategies za miaka 5 au 10 ambazo kila mwaka tutazitimiza kwa bajeti. Je ajenda ya viwanda imeisha, tumeanzisha ngapi?
 
Ningefikiri waje na clear strategies za miaka 5 au 10 ambazo kila mwaka tutazitimiza kwa bajeti. Je ajenda ya viwanda imeisha, tumeanzisha ngapi?
tabu wataalamu wetu hawako tayari kutoa msaada kwa kadri ya taaluma zao wengi wamebaki kufanya kazi za mazoea hawako tayari kuaibika kwa kuang'ang'ania wanachokiamini, wamekuwa watu wakuburuzwa na wanasiasa na matokeo yake tija ya moja kwa moja haionekani kwa jamii ni kweli miundo mbinu kama reli inatakiwa ijengwe kwa muda mrefu kwa kuwa kwanza ni capital good ili tuweze kubaini mapungufu wakati wa utekelezaji wakati mjenzi akiwa anaendelea lakini kinachosumbua baba mwenye nyumba anataka kura hivyo ukimwambia miaka kumi tujenge reli na zingine tuwekeze katika kupanua ajira na kuleta tija kwa taifa hawezi elewa haraka
 
Kwan ndege sizimekwisha nunuliwaa? Au zinginee tenaa

hizo ni nyingine 4 mkuu wanaangaika na maeneleo ya vitu wanasahau watu

leo hii watu wapo mtaani miaka miwili wanasubiri ajira hawajakumbukwa wanazidi kuangaika maisha magumu

mpango wao wa elimu bure walioutangaza wameusahau leo hii shule zinahangaika kwa bajeti ndogo huku wananchi hawataki kuchangia kwani wameaminishwa elimu ni bure

kilimo kimesahaulika na tunafahamu mabadiliko ya tabia nchi duniani na hasa eneo letu la afrika mashariki bila hatua za haraka kuchukuliwa siku zijazo tutapata taabu

kwenye afya matatizo ni mengi kuliko

tz ya v-wonder
 
Kwan zile nyingine bajet yake ilipitishwa na bunge lipi?
 
Kama tulikuwa tumeachwa maili 10 na jirani zetu, tunako elekea hii nchi tutaachwa maili 1000 zaidi. Katika dunia ya sasa kuendesha nchi YOU need to be very smart, ndipo hapo unaweza kuiendeleza nchi yako.
 
Kutoa kipaumbele kwa mananuzi ya ndege za ATC kuna - defy reasoning. Hii ni kwa sababu kipindi cha ndege kurudisha uwekezaji wake ni kirefu sana. Vile vile hatujaelezwa mikakati madhubuti ya kuweza kuhakikisha hizo ndege zitapata wasafiri wa kutosha. Ikumbukwe kuwa hii biashara ina ushindani mkubwa sana na mashirika makubwa yanashusha bei ili kuuwa ushindani.
 
Hivi ni nani ananunua tv wakati hana chakula?Ni nanai ananunua begi wakati hana nguo?Njoo Tanzania uwaone tena ni wenye vyeo waliovaa suti, wanaojigamba wanaakili kuliko wengine
 
Back
Top Bottom