Mkuu kwa uelewa wangu, kazi ya serikali ni kujenga mazingira mazuri mfano miundo mbinu, miradi ya kilimo, sera mbalimbali nk na kinachofuata ni mtu mmoja mmoja kutumia hizo fursa kujiletea maendeleo. Mfano, ndege zitaleta wageni, Liganga italeta wawekezaji, ajira nk ujenzi wa reli utarahisisha usafirishaji kwa bei nafuu, cement ambayo inauzwa kigoma mf 20,000 ikiletwa na kwa reli cement hiyohiyo usishangae ikauzwa kwa sh 15,000/= Maana yake ni nini ? ni kuwa kwa kutumia fursa hizi na ww upambane ujikwamue, ujenge nyumba nzuri, upate tiba na madawa, usafirishe mazao yako toka huko kijijini kwenda mjini, hayo ndio maendeleo, au nikuulize ww unadhani unapoambiwa maisha yatabadilika unategemea kuona mabadiliko gani ?Wa ndugu naleta kwenu vipaumbele vya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 ambavyo vimetajwa na waziri wa fedha. Vipaumbele hivyo ni.
1.Ujenzi wa Reli
2.Kuhuisha ATCL
3.Ununuzi wa ndege
4.Mradi wa Liganga
5.Kuhamia Dodoma
6.Kuanzisha kanda maalumu za kiuchumi.
Je kwa vipaumbele hivi maisha ya mtanzania yatabadilika ukilinganisha na hali ilivyo sasa??!