VIP makanisani.....

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Wadau, hivyi mnajua kuna makanisa yametenga siti maalum kwa watu (VIP) fulani n ukikaa hizo siti lazima utanyanyuliwa. Ukiuliza sababu unaambiwa wewe utaweza kulipa 250,000 kila jumapili kama sadaka? hivyi dini ndiyo imekuwa biashara kiasi hicho?
 
kanisa gani hilo wana tabia chafu namna hii?

hebu litaje kwanza
 
Ukishaona hivyo basi ujue hapo kanisani kwenu faith imeshakua compromised!
 
Jameni Bible inasema msipende kukaa viti vya mbele ambapo waweza kuja kuondoshwa hili waheshimiwa wakae, kwani ukikaa nyuma husikii neno?
 
Hiyo ni tabia ya kanisa ulilokwenda wewe, hivyo usihalalishe kwamba hiyo ni tabia ya Makanisa.
 
Hiyo ni tabia ya kanisa ulilokwenda wewe, hivyo usihalalishe kwamba hiyo ni tabia ya Makanisa.
Na ndiyo maana nikasema "KUNA MAKANISA" kauli hiyo pekee inaonesha c yote....
 
Umeambiwa taja basi mfano wa makanisa hayo, nina uhakika kila kanisa hapa tz lina member wa jf!...epuka majungu!
 
naomba niyataje hayo makanisa na VIP seats.

1.AZANIA FRONT

EDWARD LOWASA HUYU ALIPEWA KITI CHA MBELE KUSHOTO

2.SAINT JOSEPH CATHEDRAL NA SOME TIMES SAINT PETERS OYSTERBAY.

BENNY MKAPA MBELE KULIA
 
naomba niyataje hayo makanisa na VIP seats.

1.AZANIA FRONT

EDWARD LOWASA HUYU ALIPEWA KITI CHA MBELE KUSHOTO

2.SAINT JOSEPH CATHEDRAL NA SOME TIMES SAINT PETERS OYSTERBAY.

BENNY MKAPA MBELE KULIA


Mwongo wa kutupwa Benny anasali St Imakulata - Upanga :D
 
Mkuu ushahidi si huo amekutajia hayo makanisa na siti zake!
Sasa wewe jaribu kwenda na kukaa kwenye hizo siti, then tuone kama utanyanyuliwa au la.


Ndiba Benny tuko nae upanga ukimwona st joseph au peter`s kuna ibada maaluum
sasa aseme hapa upanga kiti chake ni kipi?
 
Mada hii haina mashiko...ina mtazamo-shoto zaidi kuliko kujenga.
Bible inasema kwamba Viongozi wa Serikali na waheshimiwe, maana wasingepata madaraka hayo kama yasingelitoka juu!
Kama kanisa linapata taarifa kwamba VIP fulani anakuja kusali kanisani kwao, ni lazima wajue atakaa wapi, si kitu cha ajabu aisee!
Wewe mwenyewe ukipata habari za ujio wa mtu muhimu kwako lazima kuna maandalizi unafanya bana...usipime watu hapa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom