Vip kile kipindi cha Pro.Shivji pale ITV kuhusu katiba mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vip kile kipindi cha Pro.Shivji pale ITV kuhusu katiba mpya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwenyenguvu, Aug 18, 2012.

 1. mwenyenguvu

  mwenyenguvu Senior Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mimi nilikuwa ni miungoni mwa wasilikizaji wakubwa katika ile shule aliyokuo akiitoa pro pale itv,na mada zake zote nilizilekodili ili zinisaidie katika kuandika na kutoa maoni juu ya katiba mpya mara tu tume itakapokuwa hapa dar.Sasa najiuliza,mbone kile kipindi kimepotea ghafla?
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Prof. Shivji anahangaika na kombora alilorushiwa kwamba alisema Muungano uvunjwe!
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  ..mimi nahisi Prof amehongwa na CCM.

  ..kauli zake za hivi karibuni ni tofauti kabisa na maandiko yake ya muda mrefu.

  ..Prof ameandika vitabu vingi sana akiukandia muungano, lakini majuzi amegeuka anadai kwamba anaunga mkono muungano, tena anataka serikali 2.

  ..hata Ahmed Rajab, yule mwandishi wa ki-Zanzibari mwenye chuki kali na wa-Tanganyika, ameandika makala akimshangaa Prof.Shivji kuhusu kubadilika kwa msimamo wake.
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Pengine ameambiwa Watawala wanachunguza kama yeye ni Raia ama la, hivyo amelazimika kurudisha majeshi nyuma...
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  huyu hana lolote lile la maana. ni anti christian, anti semite na anti west wa kutupwa.
   
 6. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mmmm hata user name yako ina sadiki ukisemacho.
   
 7. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,026
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  wengi wa wasomi wa tanzania wanaongonzwa na matumbo yao....kitumbua kikitisshiwa kuwekewa mchanga wanafyata mikia....
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,625
  Trophy Points: 280
  Vile vipindi vilikuwa ni six series, yaani ni vipindi 6 tuu ndivyo vilivyopangwa tangu mwanzo na viliisha rasmi na havikukatizwa!.

  Japo zile series zimeisha, hoja nyingi bado zinahitaji ufafanuzi, labda tiombe ITV iendeleze zile series!.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,625
  Trophy Points: 280
  Mkuu Joka Kuu, mimi ni mwanafunzi na mfuasi wa Prof. Shivji, ni kweli ameandika na kutoa mihadhari kibao kuhusu muungano, ila hajawahi kusema muungano uvunjwe!, japo ameuzungumzia kuwa muungano haukuwahi kupata uhalali wa kisheria toka pande zote za muungano, lakini matendo ya utekelezaji wa muungano toka pande zote, yauhalalisha rasmi muungano wetu!.

  Muungano ni kama ndoa, japo ilikosa uhalali wa kisheria, lakini baada ya kuwa "consumated", then ni muungano halali!.

  Muungano wa Ndoa halali, huingiwa kwa ridhaa ya wana ndoa, baada ya ndoa kufungwa, ndoa hiyo haiwi halali mpaka baada ya ndoa hiyo kuwa "consumated". Endapo ndoa itafungwa bila ridhaa ya mmoja wa wanandoa husika, hivyo kugoma kuisaini hati ya ndoa, lakini hatimaye mwanadoa huyo akakubali kui "consumate" ile ndoa, ndoa hiyo inakuwa halali licha ya mwana ndoa mmoja kutosign ile hati ya ndoa hivyo kuwa na ndoa halali yenye hati iliyokosa uhalali wa kisheria!. Hii huitwa "voidable marriage", kule kukosekana uhalali, kumerekebishika kwa kuitimiza ndoa hiyo!.

  Ziko ndoa nyingi ambazo ni ndoa halali lakini hazina hati ya ndoa kuzihalalisha mbele ya macho ya sheria. Vivyo hivyo zipo ndoa, ambazo hati za ndoa zimesainiwa vizuri na wanandoa wote wawili, na mashahidi wote wawili, kisha ikafuatia sherehe kubwa ya ndoa, lakini kufika chumbani, mwan`andoa mmoja akagoma kui "consumate" hiyo ndoa!, ndoa hiyo inakwa sio ndoa tena bali ni ndoa batili ambayo haukuwahi kuwepo, japo hati za ndoa hiyo ni hati halali. Hii huitwa "void marriage" na kuivunja hakuhitaji hata talaka kwa sababu hajakuwepo hata hiyo ndoa yenyewe kilichopo ni hati tuu!.

  Alichosema na alicho tufundisha Prof. Shivji, ni kuwa zile hati za muungano hazikufanyiwa "ratification" kwa upande wa Zanzibar, hivyo kukosa uhalali wa kisheria kwa zile hati, lakini utekelezaji wa vipengele vya muungano kwa pande zote, kumeuhalalisha rasmi muungano huo, licha ya zile hati kukosa uhalali wa kisheria na kamwe hakuwahi kusema muungano sio halili wala kutaka kuuvunja muungano japo process ya kuungana ilikosa uhalali wa kisheria!.

  Kama ilivyo mkataba wa ndoa, kuna void na voidable, vivyo hivyo sheria za mikataba kuna void contracts, na voidable contracts, ule mkataba wa muungano ni voidable contract, ilikosa uhalali wa kisheria na sio void contract ambao ni mkataba usio halali!.

  Pasco.
   
 10. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hicho kiwango fulani cha uelewa ni kipi? Wewe unacho?
   
 11. B

  Beria Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Aibu ni pale mtu anapomkandia mtu kwa sababu ya uwezo wake mdogo wa kuelewa kile anachosema! Baadhi ya watu humu hawamwelewi Shivji, huwezi kusema Shivji hataki muungano. Wengine wamesoma maaandiko yake ila hawakuelewa, bahati mbaya kweli hii!
   
 12. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sasa kama unahitaji uwe na kiwango fulani cha uelewa, na wewe umesema hapo juu (kwenye hayo maandishi meusi yaliyokolea) kuwa huna hicho kiwango, iweje utufafanulie kwa lugha nyepesi na mifano rahisi ya wazi kabisa ili tuelewe ilihali umesema huna hicho kiwango cha uelewa wa kuweza kumuelewa Issa Shivji?

  You ain't all that you think you are. At best you are very average.
   
 13. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Shivji is not some super-larger than life genius and neither are you.

  You contradicted yourself and you don't even have the humility to fess up to it and instead you are resorting to throwing little mickey mouse snide comments just to make yourself feel like you are some type of an intellectual superior (when the fact of the matter you are not)

  Hubris and obduracy won't get you far. Quite possibly it could result in your ruination. Take that Mr. so called learned brother.
   
 14. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  I'm not least bit interested in your college grades. Take that juvenile stunt to your wife or whoever else that's interested. But not me.

  Verdict: Epic fail.
   
 15. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Another epic fail!!

  Unaleta vi-grade vyako vya UDSM hapa ili um-impress nani? Kubwa zima lakini utoto hujaacha. Utakua lini wewe?

  Grow up and start acting like you got some hair in your armpits and nether region.
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  So sad ...SMH
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  ..kwanza nikiri kwamba mimi siyo mwanafunzi wa Prof.Shivji, na vilevile siyo mwanasheria.

  ..katika udadisi wangu, masuala yanayohusiana na hoja za kisheria au kikatiba kama hii tunayojihusisha nayo, huwa si rahisi kwa washiriki wote kufikia conclusion ya aina moja.

  ..hoja za kisheria au kikatiba, ni tofauti kabisa hoja za mahesabu, au any other physical science. mfano, katika hisabati ikiwa utajenga hoja kwamba namba fulani inagawanyika kwa mbili, basi huna jinsi zaidi ya kufikia conclusion kwamba namba hiyo ni even.

  ..sasa nyinyi wasomi wa sheria hambanwi na kanuni kama ilivyo ktk hisabati, au science. ndiyo maana hata wakati mwingine mahakama hulazimika kuwa na majaji 3 ili kuamua shauri lililoko mbele ya mahakama. sijawahi kusikia yule jaji aliyetoa minority opinion akatupiwa vijembe na wenzake kwamba amekosa "uelewa" kama wewe ulivyofanya kwangu mimi.

  ..tukirudi kwenye hoja, Prof.Shivji ameandika makala pamoja na vitabu kwamba muungano umekosa msingi wa kisheria na kikatiba. Sasa hata nikikubaliana na madai yako kwamba Prof.Shivji hajatamka maneno "muungano uvunjwe", how do we get out of this mess??

  ..Je, ni hatua zipi tunazopaswa kupitia ili kuupa muungano wetu msingi wa kisheria na kikatiba? Je, hatupaswi kurudi kwenye bunge na baraza la wawakilishi? Je, hatupaswi kuwauliza wananchi wa pande mbili za muungano? Je, wakati tunafanya yote hayo muungano wetu utakuwa ktk state ipi? Je, utakuwa likizo, umevunjika, transition, au??

  ..Mwisho, nakubaliana na wewe kwamba Prof.Shivji anaweza kuwa hajatamka maneno "muungano uvunjwe", lakini makala na hoja zake zinatoa nafasi kwa wasomaji wake ku-conclude kwamba anachomaanisha yeye ni kwamba muungano ni batili na hivyo unapaswa kuvunjwa.

  ..Naomba nimalizie kwa kueleza masikitiko yangu kwa jinsi alivyotuponda wale tusiokuwa na mtizamo kama wako, kwamba ni watu tuliopungukiwa uelewa wa namna fulani kwasababu tu hatujapata kuhudhuria darasa la Prof.Shivji.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,625
  Trophy Points: 280
  Mkuu Joka Kuu,

  Kiukweli, nawaombeni msamaha sana, wale wote waliokwazwa na ile kauli yangu kuwa "mtu unahitaji kiwango fulani cha uelewa ili kuweza kumwelewa Prof. Shivji!.

  Nimeguswa na nimeumizwa na kauli yangu!.

  Samahani sana kwa kauli hii!.

  Much regrets.

  Pasco.
   
 19. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Phony remorse.
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  ..apology accepted.

  ..hakijaharibika kitu.

  ..tusonge mbele na mjadala wetu.
   
Loading...