Vioo vya Samsung kuanzia S6 Edge ni vya hovyo sana

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
9,672
2,000
Pomoja na Tech nzuri ya Super Amoled, vyenye mwanga mng'aavu, Vioo vya hizi simu ni mtihani sana kwa watumiaji.

Yaani kuanzia toleo hilo na kuendelea vioo vinaweka mistari bila sababu ya msingi kama TCL.

vipo so delicate, weka liquid protector ongezana Glasi protector lazima vikutafutie sababu ya kukutia hasara.

pia vinaweka Vidoa vya wino kwenye vioo.

sasa kaulize bei ya kioo, bora ununue simu nyingine.

Nina Sunsung 3 kabatini sida ni vioo tu. najua madon watakuja na kusema nanunua simu za bei rahisi, well mbina Infinix, Techno, Huawei na Iphone hawana hili tatizo kwa kiasi hiki?

Ngoja nihamie OPPO A92 nione.

ONA HAPA BEI YA KIOO TU
UCScreenshot20210109132453.png
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
24,035
2,000
Pomoja na Tech nzuri ya Super Amoled, vyenye mwanga mng'aavu, Vioo vya hizi simu ni mtihani sana kwa watumiaji..
Sio simu za bei rahisi Bali refurbished.

Huo wino ilishatoa toka huko ughaibuni wajanja wakacheza nayo ukaja kupigwa wewe huku.

Kama ulinunua mpya na warranty ya miaka 2 ya Samsung Africa peleka kwa wakala wao itatengenezwa Bure tu.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,034

Hivi kaka katika simu ubora wa kioo huwa unapimwaje?Yaani kwenye specifics za simu kuna sehemu huwa wanazungumzia kuwa kioo kina ubora fulani?Au kwa maana nyingine mfano nitajuaje kuwa samsung A50 ina kioo bora kuliko Mi A2 lite?
 
gwankaja

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,577
2,000
Vioo vya samsung ni delicate sana, nina J7 pro kioo kimevunjika mara 3, hii mara ya mwisho nilibahatika kiliweka cracke tu..nimeacha ikija kufa ndo bas siwez badilisha tena.

Ila nina Iphone haina hata screen protector ila hakuna hata mkwaruzo
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
24,035
2,000
Hivi kaka katika simu ubora wa kioo huwa unapimwaje?Yaani kwenye specifics za simu kuna sehemu huwa wanazungumzia kuwa kioo kina ubora fulani?Au kwa maana nyingine mfano nitajuaje kuwa samsung A50 ina kioo bora kuliko Mi A2 lite?
1. Unaangalia resolution aka idadi ya pixel. Jinsi display inavyokuwa na pixel nyingi ndio jinsi Picha inakuwa angavu na nzuri. Kwa kuangalia A2 lite na A50 zote zina resolution moja.

2. Una angalia technology iliotengeneza kioo kama ni oled, lcd, ips lcd, Amoled, Sema zinazotumika kwa wingi ni
-Amoled/oled ambayo sifa yake ikionesha rangi nyeusi inazima kabisa pixel Hivyo inakuwa na rangi nyeusi iliokolea kabisa kila pixel hujiwasha yenyewe sababu hii hupelekea kuwa na mwanga mdogo mzuri hata usiku bila kuiwasha taa haiumizi sana macho.

Tatizo kubwa la Amoled sababu pixel zinajiwasha zenyewe huwa na Tabia ya kuungua ikionesha Picha moja muda mrefu.

-lcd yenyewe inakuwa na mwanga mkali sababu kunakuwa na Taa nyuma ya kioo, hii pixel zake haziungui kama Amoled na ikionesha nyeusi inakua kama kijivu ilioiva.

Yapo mambo mengine kama calibration ya display, vitu kama Color accuracy etc
Mfano kuna display zinaweza kuonesha rangi milioni 16, nyengine rangi billioni 1 etc.

Pia kuna standard hizi mpya za Hdr10 na Dolby vision ambazo zote zinaashiria kioo kinaweza onesha mabilioni ya Rangi, kwa mwanga mkubwa sana na mdogo sana kuileta ile feeling kama ya real life.

Na mwisho wa siku mkuu specs tu hazitoshi, review muhimu, unaweza kuta ikawa Amoled ikawa mbaya na lcd ikawa nzuri kutegemea na Nani katengeneza na katumia nini.

Ukitaka kununua kifaa angalia reviews za kutosha.
 
Kwani kaka haya uliyoyazungumzia yana uhusiano na ugumu wa kioo cha simu?(Durability).Mimi nilikuwa nataka kukuuliza juu ya ugumu(durability) ya kioo cha simu,mfano nikidondosha simu kioo kisipasuke kwa urahisi.

Yaani swali langu lilijikita kwenye hilo.Mfano nategemea simu aina fulani nikiidondosha kwenye sakafu katika umbali fulani kioo chake kisipasuke lakini simu ya aina fulani nyingine nikiidondosha katika umbali huohuo basi kioo chake kinapasuka.Sasa haya yanapimwaje?
 
Hili hupimwa na protection ya juu iliotumika.

Display inakuwa na layer nyingi, ndani kabisa ndio zinakaa hizo Amoled na lcd, juu kuzilinda hizo display wanaweka protection.

Maarufu zaidi ni gorilla glass na hizi zipo version nyingi 2, 3, 5 etc.

Sema ugumu wa glass tu hautoshi, bezell nazo husaidia, simu yenye bezell kubwa husaidia kulinda kioo, ndio maana unaona watu hulalamikia simu zenye edge maana zina bezell ndogo.

Simu za kizamani nyingi zilikuwa Ngumu kuvunjika kioo sababu ya Bezell
 
Shukrani sana mkuu hili ndiyo nilitaka kufahamu!Lakini kaka mbona sasa kwenye specification huwa hawazungumzii haya mambo ya bezell na gorilla glass?Sasa nitajuaje kuwa simu aina fulani ina aina ipi ya bezell?
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
24,035
2,000
Shukrani sana mkuu hili ndiyo nilitaka kufahamu!Lakini kaka mbona sasa kwenye specification huwa hawazungumzii haya mambo ya bezell na gorilla glass?Sasa nitajuaje kuwa simu aina fulani ina aina ipi ya bezell?
Mkuu bezel ni ile nafasi toka kioo kinapoishia mpaka pembe za simu. Mfano wa simu yenye bezell kubwa na ndogo ni kama huu.
5a3014480b0f279e268b4763

Hivyo kwa macho unaona bezell

Kuhusu gorilla glass huwa inaandikwa kwenye specs. Mfano Gsmarena huwa wanaandika.

Na Kuna baadhi ya simu pia zina plastic display, hizi ukidondosha hazipasuki Sema zikiungua na joto kubwa zinayeyuka. Samsung active series na baadhi ya Motorola zina display za hivi.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,034
2,000
Mkuu bezel ni ile nafasi toka kioo kinapoishia mpaka pembe za simu. Mfano wa simu yenye bezell kubwa na ndogo ni kama huu.
5a3014480b0f279e268b4763

Hivyo kwa macho unaona bezell

Kuhusu gorilla glass huwa inaandikwa kwenye specs. Mfano Gsmarena huwa wanaandika.

Na Kuna baadhi ya simu pia zina plastic display, hizi ukidondosha hazipasuki Sema zikiungua na joto kubwa zinayeyuka. Samsung active series na baadhi ya Motorola zina display za hivi.
Shukrani mkuu!🙏🙏🙏
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom