Viongozi ya ualimu mnajisikiaje kwa hili la madaktari

CHEMPO

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
368
59
Hakuna kada yenye viongozi dhaifu kama ya ualimu..mishahara ya wanaowaongoza iko chini ila wao hawana shida wamelala fofofo
angalia viongozi wa kada ya afya pamoja ya kuwa mishahara ya wanaowaongoza ni yakuridhisha ila bado wanapambana kuendana na mfumuko wa bei..(mfano mwl cheti 244,000 afya chet 476000)
viongozi wa waalimu amkeni
 
Waalimu viongozi wenu ni DHAIFU sana! Wanahongwa laki mbili, wanawauza waalimu wote. Wanasahau kuwa na watoto wao watakuwa waalimu wauridhi umaskini ( Mwana wa msana husana, asiposana hufukuta.) Halafu eti wakisikia daktari anadai wanasema mbona hata sisi tunalipwa kidogo.
Halafu cha kusikitisha, ni kuwa waalimu wamegoma karibu mwaka wa kumi sasa lakini hawasemi. Ukitaka kuhakikisha hilo, angalia matokeo ya wanafunzi Mfano mwaka jana form four Division I-III= 9.7%. Division 4 na ziro 90.3%. Darasa la saba ndo usiseme, mwaka jana wanafunzi elfu tano walipasishwa kwenda sekondari bila kujua kusoma wala kuandika. Hii inakuingia akilini kuwa eti kuna mwalimu anafundisha????!!!!
 
Waache kwanza tunajipanga tuko chuo kwa ajili ya viongozi hao tunakisafisha kwanza chama cha walimu kisha tuingie kwa serikali kudai haki. Naamini walimu wenzangu mtaniunga mkono. Tuanze kuifuta CWT kwa mapinduzi afu tupambane. Wailimu safiiiiiiii!!
 
Back
Top Bottom