Viongozi wote wawili wa Muamsho na watu 30 wako nje hadi Juni 16, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wote wawili wa Muamsho na watu 30 wako nje hadi Juni 16,

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, May 28, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Posted on May 28, 2012 by zanzibaryetu[​IMG]Zanzibar leo hii imejikuta ikirejea kule ilipotoka baada ya matukio ya uvunjifu wa amani kujitokeza kwa mara nyengine tena ambapo wananchi na jeshi la polisi kwa pamoja wamekuwa wakifanya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Vijana wenye hasira wamechoma moto matairi barabarani na kuharibu mali za watu lakini na Polisi nao wamekuwa wakiwakamatwa vijana hao na kuwapiga kwa marungu na mateke jambo ambalo ni kinyume na haki za binaadamu ambapo Tanzania imeridhia azimio la umoja wa mataifa la kuheshimu haki hizo.

  JUMLA ya watu 30 wakiwemo wanaodaiwa kuwa viongozi wawili wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, leo walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashitaka ya uzembe, uzururaji na uvunjifu wa amani.

  Shitaka jengine walilosomewa mahakamani chini ya Hakimu Mohammed Ali Mohammed Shein hapo ni pamoja na kufanya mkusanyiko usivyo halali ambapo Mbarouk Said Khalfan (45) Mkaazi wa Taveta Meli nne na Mussa Juma Issa (57) Mkaazi wa Makadara wote wakaazi wa Mjini Zanzibar.

  Washtakiwa hao ambao walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa aman, walifikishwa mahakamani hapo wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi.
  Viongozi hao kwa pamoja walisomewa mashitaka ya kujikusanya na kufanya maandamano kinyume na sheria kifungu 55 (1)(2)(3) sheria nambari 6 ya mwaka 2004. ambapo Hakimu Shein alisema mahakamani hapo kwamba mnamo Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:30 za mchana viongozi hao walijikusanya kinyume na sheria za Zanzibar.

  Hakimu huyo alisema wananchi hao walifanya maandamano ambayo yalianzia katika uwanja wa Lumumba kupitia Msikiti wa Biziredi na kumalizia uwanja wa Lumumba, ambalo ni kosa kwa vile linaweza kuhatarisha amani na utulivu na kuweza kusababisha
  uharibifu wa mali za wananchi wa Zanzibar.
  Mbali ya viongozi hao wanaodaiwa wa Uamsho wengine walijumuisha katika kesi hiyo ni Mbwana Hamadi Juma (50) Mkaazi wa Nyerere, Masoud Hamadi Mohammed (17) Mkaazi wa Mtoni Kidatu, Mohammed Juma Salum (35) Mkaazi wa Kianga na Abdulrahman Simai Khatib (19) Mkaazi wa Mbweni.

  Wengine ni Hashim Juma Issa (54) Mkaazi wa Mbweni Matar Fadhil Issa (54) Mkaazi wa Mbweni, walifikishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu Mdhamini Janet Nora Sekihola kujibu shitaka la uzembe na ukorofi kinyume na kifungu cha 181 (d) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
  Watuhumiwa wengine walifikishwa katika mahakama ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, ambao walishitakiwa chini ya kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
  Mashitaka yote hayo yaliwasilishwa kwa nyakati tofauti na waendesha Mashitaka, Wanasheria wa serikali Mohammed Kassim Hassan, Suleiman Haji Hassan pamoja na Ramadhan Abdallah, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP).
  Katika mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, Mwendesha Mashitaka Mohammed Kassim alidai kuwa watuhumiwa Mbarouk Said na Mussa Juma, bila ya halali walipatikana wakiandamana kupitia katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya mji wa Zanzibar, kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani.
  Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikana makosa hayo na kupewa dhamana ya masharti ya shilingi 300,000 kila mmoja ambapo walitimiza masharti hayo na wapo nje ya dhamana hadi Juni 16 mwaka huu, kwa kesi hiyo kutajwa.
  Awali mahakamani hapo vikosi vya ulinzi na usalama walionekana kujipanga imara na kuhakikisha usalama umedhibitiwa wakati wote wa uendeshaji wa kesi hiyo ambapo maeneo yote ya Mahakama ya Mwanakwerekwe yaliimarishwa ulinzi ndani na nje ya eneo hilo.

  Mamia ya wananchi walifika katika eneo la mahakama hiyo na kuja kusikiliza kesi hiyo lakini waliishia nje ya mahakama hiyo kutokana na ulinzi uliozunguka katika eneo hilo mwanzo hadi mwisho wa kesi hiyo.

  Licha ya watu hao 30 kufikishwa mahakamani leo lakini hali ya amani bado haijatengeneza kutokana na baadhi ya maeneo kurushwa mabomu ya machozi na watu kadhaa kutawanywa katika maeneo ya Mwanakwerekwe, Darajabovu, Amani na Mikunguni muda mfupi baada ya wananchi kutoka katika eneo la mahakama hiyo.
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Hakuna kesi itakayo kwenda na kutiwa nguvuni viongozi wa Muamsho , itaishia uzembe na uzururaji tu, hii nikuwa viongozi wote wa Smz/suk wanajuwa fika kuwa Muamsho siwapumbavu na wachome kanisa na hujuma nyingine.

  Wao walifanya mandamano yao Salama na kumaliza salama na watu kuchawanyika bada ya kupeleka ujumbe wao, na hii ya maandamano hata viongozi wa Smz waliwapa baraka kufanya ni ile geresha tu lakini jumuia ya Muamsho inaungwa mkono na vigogo takribani wengi wa Serekali wavyama tafauti katika madai yao.

  Na hii ya kufanya hujuma hapa kwetu imezoweleka watu hutafuta vishingizio ili kupata mitaji , sio kanisa tu hujuma nyingi hufanya watu ili kupota malipo , Gari,kanisa na maduka wote hao wanategeme posh mwenye gari anajuwa atalipwa na kanisa lita jengwa la horfa mbili au tatu.

  Hii yote ni mitaji ya wakubwa kumwaka pesa na watu wakafanya ufisadi , unambiwa gari lina samani ya million 20 ,Kanisa million 125 watu watakula hela ya Serekali na hakuna litakalo kuwa vitendo hivi ni mitaji ya watu fulani ndani ya Serekali hutafutwa tu vishingizio.
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hao Uamsho hoja yao siyo Muungano. Muungano unatumiwa tu kam geresha. Hawa ni siasa kali mawakala wa Al-Qaida. Lengo lao Muungano ukivunjika watapata mwanya wa kudai taifa la kiislamu linaloendeshwa kwa sharia. Kuanzia hapo itakuwa kilio na kusaga meno. Tujitayarishe kuanza kulipukiwa mabomu Dar es Salaam na Zanzibar kama inavyotokea Nairobi na Mombasa na Nigeria. Sasa nimeelewa kwa nini Nyerere alisema angekuwa na huwezo angevisukumiza visiwa yya Zanzibar mbali baharini ili visiwe karibu na Tanganyika.
   
 4. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dunia nzima ishapata uhakika kuwa sehemu ya Tanzania ina magaidi hatari
   
Loading...