Viongozi wote wakitibiwa nje ni nani ataijenga Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wote wakitibiwa nje ni nani ataijenga Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Raia Fulani, Jul 2, 2011.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hili swali watanzania tunajiuliza? Iweje viongozi wote nchi hii wakatibiwe nje ya nchi? Hivi kuwa kiongozi ina maana unakuwa sio raia? Ni mazoea kuwa kila kiongozi wa juu akiumwa anapelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Wanapelekwa India, Uingereza, Ujerumani, Kenya na kwingineko. Siku za karibuni tumesikia Mzee Malechela kapelekwa Uingereza na sasa yuko Marekani mapumzikoni. Muda si mrefu tumeambiwa Prof Lipumba na Mark Mwandosya wako Apollo-India kwa matibabu.

  hatukatai kuwa kwa kuwa ni viongozi ni lazima wapewe treatment ya hali ya juu. Tnajiuliza, hizi treatment tunazowapa (ni kodi zetu) zina tija gani kwetu sisi wananchi? Ni maamzuzi gani wayafanyayo ambayo kweli tunaona wana haki ya kupata hizi huduma?

  Ni kwa nini basi kwa kuona kuna kasoro katika hospitali zetu, serikali kupitia hawa viongozi haioni kuna haja ya kuiboresha sekta ya afya nchini? Wanachojua tu ni kupitisha bajeti na kuchukua posho mbalimbali za makalio.

  Tujiulize kwa mfano, mzee Malecela katika kulitumikia taifa kwake, aliisaidiaje sekta ya afya hapa nchini? Ni ushawishi gani na juhudi zipi alizofanya ili kuhakikisha kuwa sekta ya afya inaboreka. Leo hii anaeda kutibiwa Uingereza na sasa yuko mapumzikoni Marekani. Kwa nini hakutibiwa mathalani Muhimbili ama Agakhani halafu aende marekani kupumzika?

  Hatupendi viongozi wetu wafe kwa maradhi yanayotibika. Wala sisi raia hatupendi kufa. Ila watuambie, kuwa kwao madarakani kuna tija gani kwetu sisi kama hadi leo kila kiongozi anaenda kutibiwa nje ya nchi? Ni nini hasa wanachofanya katika hivyo viti wanavyokalia ikiwa sekta ya afya ni mbovu, nishati mbovu, miundombinu mibovu, kilimo kibovu, elimu mbovu, siasa yenyewe mbovu... karibu kila kitu kibovu. Bahati mbaya karibu kila kitu ni kibovu kwa raia lakini kwa viongozi ni tofauti, ndio maana wanatibiwa nje n.k.

  Kwani imeshindikana kujenga hospitali tatu za maana hapa nchini ambazo viongozi wetu wangeweza kwenda kutibiwa huko? Kila siku wanazungumzia vipaumbele lakini wanakuta wameshaweka vingi hadi wanashindwa kushika kipi ili kukikamilisha kwanza. Na huu usemi wa kusema 'wakati wenzetu wanatembea sisi tukimbie' ndio tatizo jingine. Si kila mbio zina baraka. Na kwa nini tukimbie? Tulikuwa tukifanya nini hadi tukapitwa hivyo? Na waliosema kuwa polepole ndio mwendo walikosea? Tatizo hawa viongozi wakikimbia, pumzi zinawaishia wanabaki kutweta kama samaki aliyebwagwa nchi kavu. Wakitembea, hata kinyonga ana nafuu. Wakikaa wanalala tu! Na huu ndio mwanzo wa matatizo ya taifa hili. Siafiki hawa viongozi kwenda kutibiwa nje kama hatuoni tija yoyote tka kwao. Bora tubanane kwenye hospitali zetu na kama ikishindikana tufe wote tu. Huo ndio uzalendo na kujibainisha na hali halisis ya watanzania wengi-Patriotism and empathy
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  Bila kuipiga chini CCM Tanzania haitajengwa kamwe, wenye mioyo wenyewe wamewsha vunjika mioyo kwa sababu ya uroho na ulafi wa wana magamba
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Na kuendelea kote South Africa, Mandela alipokuwa na matatizo ya macho alienda kutibiwa Saudi Arabia.

  Mimi nimeshaona wageni wengi wa nchi za jirani na hata wa mbali kiasi wakija Tanzania kutibiwa, hususan kwenye tiba za cancer pale ocean road.

  Kwenda kutibiwa nje ya Tanzania si viongozi tu, hata wengine huenda, inategemea ugonjwa gani na huyo bingwa wa ugonjwa ule yuko wapi. Isitoshe, madaktari wetu bingwa wengi tu huchukuliwa nje kutibu.

  Katika fani ya tiba si nchi nyingi duniani zilizojikamilisha kwa kila kitu.
   
 4. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  JSM alipotoka hospitalini London alipumzika 'nymbani kwake' hapo London. Na sasa yuko USA 'nyumbani kwake' pia.
  Ama kweli utumishi wake serikali huyu mzee ulitukuka, no wonder hatukuweza kuwa na mikakati endelevu ya kuwa na hospital za kuwatibu viongozi.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sidhani kama wasauz walilalama Mandela alipoenda kutibiwa huko. Mbona majuzi hapa afya yake ilikuwa gumzo na akatibiwa hapo hapo sauz? Na hao wageni unaosema wanakuja taasisi ya cancer watakuwa ni raia wa kawaida tu huko kwao. Suala ni kwa vipi hawa viongozi wamejenga mazingira mazuri ya kutolea tiba hapa nchini?
   
 6. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  malecela yeye kaelekea new york,alikuwa waziri mkuu miaka mingi tu,alishindwa kuimarisha sekta ya afya
  mtoto wake anaona umaarufu kutangaza baba na mama awako new york
  ndio hivyo
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hata mi nimemsoma wee, naona huko ni kutafuta publicity na kujijenga kisiasa tu. Hakuna cha kujivunia toka kwa hawa viongozi
   
Loading...