Viongozi wetu wangekua hivi hakika tungekuwa mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wetu wangekua hivi hakika tungekuwa mbali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babalao 2, Aug 10, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Habari Watz, hakika kila jambo linatoa fundisho kwa jambo jingine. Kufuatia sintofahamu ktk mpaka wetu na Malawi tumeshuhudia viongozi wetu wa kada mbalimbali wakitoa ushauri na wengine wakienda mbali na kutoa maamuzi mazito na ya hali ya juu.

  Swali je viongozi hawahawa wenye ushupavu huu linapokuja jambo kama hili la mikataba mibovu, wahujumu uchumi hatuwasikii wakitoa matamko kwa mbwembwe kama hili la mpaka na malawi? Je kwanini masuala ya ndani ya nchi mpaka kulazimishwa kutolea tamko? Jamani shida ni nini kwa viongozi wetu? Suala hili haliko mahakamani jiachieni.
   
 2. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Usikimbile huko. Kumbuka pia vita inatoa mirija mingi sana ya ufisadi. Marekani walitajirika kwa ajili ya vita kuu ya pili. Tenda za aina ya rada zinakuwa nje nje wakati wa vita, na pia ku-supply chakula jeshini, mafuta nk. Wakati wa vita vya kagera wengi "walijitolea" mabasi na malori yao kwa ajili ya vita. Leo hii huwezi kufanya hivyo.

  Ukitaka kuona ufisadi wa hali ya juu, acha nchi kama Tanzania iingie vitani, jeshi litauziwa nyanya moja kwa shs 2000!
   
 3. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  umenifungua macho ndyo maana wenye mitaji ndio wanataka litimie neno wabandike mirija si hawa pia wanataka kile kiti pale juu
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Tamko si issue.

  Mbona Kikwete kashatoa matamko mara kibao, mara wala rushwa anawajua, mara dawa yao inachemka.

  I am not impressed by matamko, tunataka vitendo.

  Na hata hao wanaotoa matamko kuhusu mpaka mi naona wapishi wengi huharibu mchuzi tu.
   
Loading...