Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?

Apimwe akili,au ni laana ya kuvuruga kuharibu uchaguzi mkuu,au ni laana ya kushadadia kushikia kidede dhuluma ya ishu ya Lisu.
 
1.Anaomba msamaha so kwasababu kakosea bali anajua nguvu ya Rais mfalme anayelindwa na KATIBA mbovu. Japo yeye ni kiongozi wa mhimili wenye nguvu unaopaswa kuisimamia serikali lkn anajua , Rais anaweza fanya lolote. Ukizingatia anaangalia future yake. Tafsir yake Ni kila mwenye nafasi anajitahidi kulinda kitumbua chake hata kwa kujifedhehesha.

2.Hawezi kuwajibika/kujiwajibisha kwa sababu hata kwa kutofanya hivyo pia Hakuna wa kumwajibisha. Hakuna wa kuwajibika na Hakuna wa kumwajibisha. Mwenye mamlaka ya kumwajibisha akijaribu kufanya hivyo anajikuta anajiwajibisha na yeye pia.

Yote haya Ni matokeo ya Katiba mbovu.
Kazi kweli kweli !!
 
TABIA ZA NDUGAI KULINGANA NA MAVAZI:

1. Akivaa Joho la Spika;

"...Huna cha kunifanya. Pambana na kitu kingine lakini sio Ndugai."

2. Akivaa Suti ya Koti na Tai:

"Mhe. Rais sisi Bunge tunakushukuru na kukupongeza kwa kutuletea pesa nyingi...Shilingi Trilioni 1.3 ni nyingi na yote inaenda kutuletea maendeleo."

3. Akivaa Shati la Kitenge;

"Hebu fikiria, juzi mama ameenda kukopa sh.1.3 Trilioni. Miaka 60 ya Uhuru tutembeze bakuli...ipo siku nchi hii itapigwa mnada."

4. Akivaa Suti ya "Kaunda:"

"Nimekosa mimi, nimekosa sana. Nimekosa mimi, Mungu anisamehe, Watanzania nisameheni."

Kwa uzoefu huu, toa Wasifu wa Ndugai.
 
TABIA ZA NDUGAI KULINGANA NA MAVAZI:

1. Akivaa Joho la Spika;

"...Huna cha kunifanya. Pambana na kitu kingine lakini sio Ndugai."

2. Akivaa Suti ya Koti na Tai:

"Mhe. Rais sisi Bunge tunakushukuru na kukupongeza kwa kutuletea pesa nyingi...Shilingi Trilioni 1.3 ni nyingi na yote inaenda kutuletea maendeleo."

3. Akivaa Shati la Kitenge;

"Hebu fikiria, juzi mama ameenda kukopa sh.1.3 Trilioni. Miaka 60 ya Uhuru tutembeze bakuli...ipo siku nchi hii itapigwa mnada."

4. Akivaa Suti ya "Kaunda:"

"Nimekosa mimi, nimekosa sana. Nimekosa mimi, Mungu anisamehe, Watanzania nisameheni."

Kwa uzoefu huu, toa Wasifu wa Ndugai.
Hahahhaa umenichekesha sana sana ulivyomchambua kwa uvaaji na tabia za mavazi
 
Mkuu Pascal mayalla heshma yako,maoni yako ni yapi ili kuweza kutibu swala zima la uadilifu na kuwajibika kwa viongozi wa umma?
Mkuu Emmanuel Mkwama , hili la uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa umma, niliisha shauri sana humu tangu kitambo mfano mzuri ni mabandiko haya matatu
  1. Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
  2. Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?
  3. TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Ukipata muda tembelea pia ujifunze jinsi awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa very seriously na issues za uadilifu na uwajibikaji.

P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali.

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika generation hii iliyopo, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, tuwaache waombe tuu msamaha na life kuendelea as usual, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha?

Paskali
Wanabodi,
Naanzisha updates ya feedback ya baadhi ya mabadiliko yangu, nilishauri nini na hatimaye ushauri huo umesikilizwa?, umefanyiwa kazi?, na matokeo ya ushauri huo.

Huu ni ushauri wa siku nyingi, lakini hatimaye leo angalau umepata sikio la kuusikia na sasa unakwenda kufanyiwa kazi
“Sasa hivi tufumbe macho anayevurunda kazini akae pembeni, hakuna haja ya kumpoza kumpeleka kwenye ubalozi.
Duh....!. Sasa leo ndio nimeelewa!. Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza, imekuwaje kwa mfano tuu ya mtu mwenye level ya DGIS, anateuliwa ubalozi na kupostiwa nchi insignificant tuu?!. Sasa nimeanza kupata majibu!.

Tuliwahi kushauri Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma

Kisha tukashauri tena, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?

Sasa ushauri huu umepata sikio la kuusikia, sasa unakwenda kufanyiwa kazi, kiongozi anayevurunda mahali, hata awe nani, hakuna tena kupoozwa kwa kupewa ubalozi!, atupishe kazi iendelee!.

Ila Mama nae...!, ameanza kuwa mkweli wa type ya JPM, hakopeshi!. Kumbe kuna watu huwa wanavurunda, ila kwa vile post zao ni nyeti sana!, wanaondolewa hapo walipovurunda na kupoozwa kwa kutupwa ubalozini!.

Naunga mkono hoja, wanaovurunda, wasipoozwe na ubalozi, watupishe!.
P
 
Wanabodi,
Naanzisha updates ya feedback ya baadhi ya mabadiliko yangu, nilishauri nini na hatimaye ushauri huo umesikilizwa?, umefanyiwa kazi?, na matokeo ya ushauri huo.

Huu ni ushauri wa siku nyingi, lakini hatimaye leo angalau umepata sikio la kuusikia na sasa unakwenda kufanyiwa kazi

Duh....!. Sasa leo ndio nimeelewa!. Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza, imekuwaje kwa mfano tuu ya mtu mwenye level ya DGIS, anateuliwa ubalozi na kupostiwa nchi insignificant tuu?!. Sasa nimeanza kupata majibu!.

Tuliwahi kushauri Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma

Kisha tukashauri tena, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?

Sasa ushauri huu umepata sikio la kuusikia, sasa unakwenda kufanyiwa kazi, kiongozi anayevurunda mahali, hata awe nani, hakuna tena kupoozwa kwa kupewa ubalozi!, atupishe kazi iendelee!.

Ila Mama nae...!, ameanza kuwa mkweli wa type ya JPM, hakopeshi!. Kumbe kuna watu huwa wanavurunda, ila kwa vile post zao ni nyeti sana!, wanaondolewa hapo walipovurunda na kupoozwa kwa kutupwa ubalozini!.

Naunga mkono hoja, wanaovurunda, wasipoozwe na ubalozi, watupishe!.
P
Angekuwa hivyo saa100 angekuwa kizimkazi siku nyingi
 
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utajibu wewe msomaji.

Naomba kuanza kwa Declaration of Interest.

Kwa vile mimi ni mmoja wa waandishi wa habari, tuliwahi kuitwa mbele ya Kamati ya Bunge na kusulubiwa, naomba bandiko hili, lisichukuliwe kuwa ni hit back. Mimi nimewahi kuandika sana kuhusu uwajibikaji na mambo ya watu kuombana misamaha batili Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity

Hili ni bandiko la swali.

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika generation hii iliyopo, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, tuwaache waombe tuu msamaha na life kuendelea as usual, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha, tena misamaha mingine ni misamaha batili kwa kutoa visingizio, vya eti nilinukuliwa vibaya!, bali msamaha uandamane na barua ya kuwajibika, kama enzi za Nyerere?.

Naomba kwanza niwaonyeshe msamaha wa enzi za Nyerere,
View attachment 2067207
Na kwa msiofahamu kisa hiki, sio Waziri Mwinyi pekee alijiuzulu, Rashidi Kawawa aliondolewa kwenye umakamo wa pili wa rais. Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa alijiuzulu.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emelio Mzena Alistaafishwa, IGP, Samuel Pundugu Alistaafishwa, Kamisha Mkuu wa Magereza Alistaafishwa. Kisha ngoma ikahamia Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alimwaga unga. RPC, RSO, OCD na DSO wa Mwanza sio tuu walimwaga unga, bali walifikishwa kwa Pilato na wote wakala mvua nyingi, isipokuwa mshitakiwa mmoja tuu, aliyekuwa anatetewa na wakili mahiri, Murtaza Lakha, ndie alinusurika.

Hivyo jee mnaonaje, huu msamaha ulioombwa leo live kwenye TV, pia uandamane na barua rasmi ya kuomba msamaha wa kweli, ukiandamana na kuwajibika?, au msamaha tuu unatosha?.

Hii Video Clip Inayosambaa

Mimi ni mtu wa Audio Visual, hivyo nikiangalia tuu a video clip, naweza kujua kama imefanyiwa makeke au laa. Hii video clip ni Bonafide Genuine, toka kwa a trusted source, haijafanyiwa makeke yoyote!.

Kwa msiojua mambo ya Audio/Video. Kila ukirekodi video, unapobonyeza kitufe cha record na kuanza ukirekodi, kile unachorekodi kinaitwa shots. Kila ukirekodi pose au ku stop, halafu inaendelea kurekodi unakuwa una change shots. Hivyo mtu ukiitazama video iliofanyiwa makeke, utanotice ama ina kitu kinachoitwa jump cuts, ama inawekewa cuts aways ili kuziba jump cuts. Video yetu hii imepigwa kwa single shot, maana yake anayerekodi alibonyeza record mara moja tuu, hakuchange shot yoyote wala kuingiza cut aways zozote, the video is smooth, simless , hivyo alichozungumza mzungumzaji hayo aliyozungumza ni maneno yake mwenyewe halisi. Hajalishwa maneno yoyote wala hii video, haijafanyiwa makeke yoyote!.

Jee Wajua Kuna Msamaha Batili, Msamaha Batilifu na Msamaha wa Kweli ?.
Sii wengi wanaojua kuna msamaha ya kweli, batili na misamaha batilifu.
Msamaha wa kweli ni pale mtu unakosa, kwanza kwa kukubali kosa, pili kujutia kosa, tatu kuomba msamaha wa dhati na mwisho ku take responsibility kwa kuwajibika kwa kubeba the consequences ya matokeo ya makosa yako, kwa kupisha ofisi ya umma kupunguza embarasment caused.

Msamaha batili ni pale mtu umekosa, badala ya kukiri kosa, unatafuta visingizio kwa kutafuta the scapegoat to shift the blame kwa wengine kwa kudai au umenukuliwa vibaya au video clip imefanyiwa maujanja!.
Msamaha Batilifu ni msamaha batili ambao ule ubatili unaweza kuondosheka na kugeuka ni msamaha wa kweli. Ule msamaha uliombwa na Spika, ni msamaha batilifu, wenye ubatili wa kusingizia kuwa Ile video inayosaamba, imetengenezwa kwa kuunga unga, kitu ambacho sio kweli!.
Ile video ni bonafide genuine, haijafanyiwa maujanja yoyote, hivyo hayo matamshi, ni matamshi halisi ya mhusika. Kuomba msamaha kwa kutafuta kusingizio chochote, ni kuomba msamaha batili wenye ubatilifu.

Ubatili kwenye msamaha huu unaweza kuondosheka kwa Spika kuchutama tuu na kukiri ni kweli ni yeye na aliyasema hayo kwa kughafilika tuu, na asitafute visingizio.

Kwa mlioisikiliza hiyo video, jee kuomba tuu msamaha kunatosha, au pia awajibike?.

Paskali

Pascal Mayalla ulimwonea bure Ndugai wa watu, maana kumbe alikuwa anasema ukweli. Sasa kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria, basi kila anayebainika kakosea iwe kwa kujua au kwa kuingizwa mkenge basi awajibike ikiwemo kujiuzulu kama ambavyo walifanya uliowaweka kwenye bandiko lako regardless nafasi ya mtu.
 
Back
Top Bottom