Viongozi wetu wanajifunza nini wakienda mikutanoni Addis? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wetu wanajifunza nini wakienda mikutanoni Addis?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Mar 30, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]ADDIS ABABA,na Jenerali Ulimwengu.[/h] March 26, 2012

  Ningependa sana watawala wetu wafike Addis Ababa wakiwa na macho yaliyofunguka tayari kwa kuona na kujifunza. Kwa siku takriban sita nimekuwa, kwa mara nyingine, nikivinjari jiji hili na kujionea maajabu wanayoyafanya wananchi wa Ethiopia na serikali yao, hususan katika ujenzi wa barabara, nyumba za kuishi na majengo ya ofisi. Ni maajabu matupu kwa mtu aliyeujua mji huu kihistoria.

  Mara ya kwanza kwangu kuliona jiji hili ilikuwa ni Januari 1970. Nilikuwa mwanafunzi wa UDSM, mwaka wa kwanza, na nikapata fursa ya kuwakilisha jumuiya ya wanafunzi katika mkutano wa “UN Decade of Africa’s Development” uliohusisha jumuiya za kiraia na vyama visivyokuwa vya kiserikali. Nilipata nafasi ya kuutembelea mji huu na kujionea jinsi ulivyokuwa mchafu na usdiopenedeza sana. Tangu wakati huo nimekuwa nikirejea Addis mara kwa mara katika kipindi chote cha miaka 40 ‘ushei’.


  Wakati wote mji ulikuwa ukionyesha dalili za maendeleo, lakini hayakuwa ya kasi kubwa. Itakumbukwa kwamba mji huu uliasisiwa na Mfalme Menelik wa Pili mnamo mwaka 1889, na kwa kuwa Ethiopia haijawahi kutawaliwa kikoloni mji huu haujawahi kuwa na maeneo yaliyotenganishwa kufuata rangi ya wakazi wake, kama vile miji yetu ilivyo na ‘Uzunguni,’ ‘Uhindini’ na ‘Uswahilini.’ Hii imekuwa na maana kwamba hakuna Oyster Bay, Upanga na Ilala, kwani sehemu zote za mji zina kila kitu.


  Si ajabu kuwa ghorofa ya kumi ya hoteli kama Sheraton na kuangalia chini ukaona ni soko wanakochinjwa kondoo au ni vibanda vya walalahoi wanaokwenda haja katika choo cha shimo kilichositiriwa kwa pazia la gunia. Lakini katika kipindi kisichozidi miaka saba Addis imeonyesha kasi kubwa ya maendeleo katika ujenzi na upanuzi na uboreshaji wa miundombinu kiasi kwamba inashangaza.


  Kila kona ya jiji, barabara zinapanuliwa, madaraja yanajengwa, njia za kupita juu (flyovers) zinasimikwa na majengo yanainuka. Kwa ujumla, mji huu ukekuwa ni saiti ya ujenzi. Wageni wakazi niliozungumza nao hapa wanasema kwamba hali iko vivyo hivyo maeneo ya shamba, kwamba barabara zinajengwa na kupanuliwa na wananchi wanajengewa nyumba za kuishi kwa bei nafuu.


  Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia, amesimamia kazi zote hizi akifuata falsafa yake inayosisitiza umuhimu wa serikali kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi na siyo kuiachia sekta binafsi kama wanavyohubiri manabii wa injili ya ubinafsishaji na utandawazi.


  Katika mkutano ninaohudhuria hivi sasa Meles amesisitiza falsafa yake hiyo. Akifungua mkutano wa tano wa pamoja kati ya Umoja wa Afrika (AU) na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi wa Afrika (UNECA) maalumu kwa mawaziri wa fedha na uchumi leo tarehe 26 Machi, Meles amedhihirsha kuudhiwa kwake na sera za kiliberali zinazozidumaza nchi za Afrika na kuwanyanyasa watu wake. Mada ya mkutano huo ni, “Kufungulia uwezo wa Afrika na kufanya Nguzo ya Ukuaji wa Uchumi wa Dunia.”


  Meles alisema:


  ” We have to liberate our minds from the neo-liberal ideological shackles that have impoverished our thinking and hindered our progress. This bankrupt ideology insists that the African state should be enfeebled and limits its role to that of a nightwatchman. We are all agreed that we need an effective state that intervenes effectively and selectively wherever there is a market failure that hinders or slows our growth. Such a state can only emerge if we discard the bed-time stories of the ideology such as that of a nightwatchman state.”  Meles aliongeza kusema kwamba kuna umuhimu wa kuwekeza kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu kwa kutumia rasilimali za dola na kuachana na dhana ya kiliberali kwamba jukumu hili zito ni la sekta binafsi:


  “We need to make massive investment in infrastructure mostly through public investments. That is how the infrastructure of nearly all of the fast growing countries and regions has been built. The ideology however insists that infrastructure has to be built by the private sector and the state should limit itself to making these lucrative and largely risk free for the private sector. That is the key reason why there has been very limited investment in infrastructure in our continent for the past thirty years. We need to discard to discard the shackles of the ideology and engage in massive public investment in public infrastructure while at the same while at the same time encouraging the private sector to fill in the gaps where it can.”  Vivyo hivyo katika sekta ya elimu, Meles amelaani sera za kiliberali kuhusu dhima ya dola katika elimu, ambayo inataka serikali isimamie selimu ya msingi tu, na kwa kiasi kidogo elimu ya sekondari, lakini elimu ya juu iachwe kama jukumu la sekta binafsi na igharamiwe na familia moja moja.


  Ametoa mwito wa kuikataa dhana hii na kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika elimu ya juu sambamba na uwekezaji katika elimu ya msingi: “We need to discard the neo-liberal prescription and massively invest in tertiary education and technical and vocational training in addition to primary and secondary education and encourage the private sector to fill in the gaps where it can.”


  Alisema kwamba sera hizo hizo zilizoiumiza Afrika na kuziumiza sehemu nyingine duniani ndizo hizo hizo zilizorudi kuziumiza nchi za mahgaribi ambao uchumi wake uligeuzwa uchumi wa ‘casino’ na kusababisha mtikisiko mkubwa wa kiuchumi katika nchi za magharibi na duniani kote:


  “The neo-liberal paradigm which has devastated our economies over the past decades has now come back home to roost…. and transformed the financial sector of many advanced countries into casinos that have played a vital role in the current crisis.”  Kwa upande mwingine, Meles anaona fursa za wazi zikijitokeza kuinufaisha Afrika iwapo nchi za Kiafrika zitazitambua na kuzichangamkia.

  Fursa hizi zinatokana na hali inayojidhidhirisha ya uchovu wa nchi zilizoendelea ambazo hazina nafasi ya kuwekeza tena, na ambazo haziwezi kujinasua pasipo kusaidiwa na nguvu mpya itakayotokana na fursa mpya za uwekezaji zitakazopatikana barani Afrika.

  “Africa, with its over a billion people, massive demand for investment in everything from infrastructure to social services is the only untapped source of global demand that could potentially fill the gap. The massive global saving that has now become part of the problem could become part of the solution if it were directed to investments in Africa,”
  aliongeza Meles.


  Kwa kuzitumia vyema fursa zinazojitokeza, Meles anaamini kwamba laana za miaka ya 1980 zinaweza kugeuka kuwa baraka kwa Waafrika kutumia vyema fursa hizo, rasilimali maridhawa na ukubwa wa nguvukazi ya Waafrika, kujenga misingi imara ya uchumi wa viwanda.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ngumu kumesa kwa viongozi wetu ambao wameshalishwa sumu kuwa binasfisha kila kitu na iachie sekta binafsi kufanya hayo

  Bila wawekezaji tutaishia kufa na kutoendelea. Sera ya elimu ndio hiyo ya kuiacha iende inavyotaka bila kujali ni aina gani ya wasomi wanazalishwa
  Viongozi wetu hjwajifunzi lolote na nafikiri hata wakienda huko hawana lolotye wanalolileta. Hivyo hata hizo hotuba za Meles ni kama porojo tuu kwao. Hawana lolote watakalokuja nalo. Hawaoni lolote lililofanyika na hawajifunzi.
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Lakini waambie wengine hatufurahishwi na namna wanavyoingilia mipaka ya nchi zingine kwenda kufanya fujo. waiache Eltrea itulie na kuendesha shughuli zake za maendeleo kwa amani na utulivu.

  Tukikumbuka kwamba dhana ya maendeleo ni pana, wakumbushe kwamba Binaadamu hata kupata fursa ya kula chakula cha jioni kwa wanafamilia huku wakifurahia mazungumzo na mahusiano yao bila hofu yoyote ile ya milipuko ya mabomu na vita vitavyopelekea familia nzima kuparanganyika na kuanza kurandaranda misituni kutafuta makazi ni maendeleo makubwa sana zaidi ya hayo mabarabara ambako juu yake kuna watu wanapita huku wakiwa hawana uhakika wa kupata japo maji ya kunywa.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..Meles naye amefanya ufisadi mkubwa sana kwa kuwapora wananchi ardhi yao na kuwapa wawekezaji wa kigeni.

  ..nadhani ufisadi wa kuuza ardhi kule Rukwa umefanyika baada ya viongozi wetu kujifunza toka kwa Meles Zenawi.

  ..ila katika masuala ya uwekezaji mkubwa ktk sekta za umeme, reli, barabara, na upanuzi wa elimu haswa ya chuo kikuu, ni lazima tumpe Meles sifa zake.
   
Loading...