Viongozi wetu wanaangalia habari kwenye luninga..?

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,539
9,462
Hivi kweli hawa viongozi wetu wanaangalia taarifa za habari kwenye luninga..? na kama wanaangalia wanajicikiaje wanapoona wagonjwa wakizidiwa na kufikia wengine kufariki..? wanajacikiaje pale wagonjwa wanapolia kwa maumivu na mateso ya kukosa huduma..? wanajicikiaje pale wagonjwa hao pamoja na ndugu zao wanapoiomba serikali kuwanusuru na dhahama hii kwa kuwacikiliza madaktari na kulipatia ufumbuzi..? wanajicikiaje wanapoona mgonjwa akiwaunga mkono madaktari wanapodai haki yao..? na walijicikiaje pale walipoona mtoto mdogo wa miaka isiozidi 12 ambae ni mgonjwa akishauri wagonjwa wote waandamane kwenda kwa waziri mkuu..? na wana jicikiaje pale wanapoona asilimia kubwa ya wananchi wanaohojiwa wakiitupia lawama hawa viongozi wetu..?
 
Changamoto kila mmoja wetu anaona ni tatizo la viongozi, siyo kweli, nitatizo letu sisi wenyewe. Sisi ndo wa kulaumiwa. Umeona jana wananchi wa Maldives walichokifanya, soma hiki kipande:

....... following a month of protests, President Nasheedh stepped down at what his spokesman described as a military coup. Following a confrontation between the president and the judiciary, opposition protests called for the president to step down. Members of the police and army, when called in by the president to subdue the protestors, instead joined them. Protestors seized offices of the national TV station and called for Nasheedh to step down. Nasheedh's vice president, Mohamed Waheed, was sworn in as president immediately following the departure....

Majeshi yetu nayaheshimu sana, Amiri Jeshi Mkuu ni Raisi, this time Waziri Mkuu ameamuru jeshi waende Muhimbili kuhudumia wangonjwa. Wanajeshi wetu (Nikiamini bado ni wanajeshi wetu Nyerere alikuwa akiwaita vijana wetu) wanaenda pale Muhimbili bila kujua kuwa wanasiasa wanawatumia. Wanajeshi 15 kwa Muhimbili, Bugando, Mbeya, KCMC ukiachilia mbali hospitali zingine wapi na wapi jamani?

Umezuka mtindo wa viongozi wetu kutumia vyombo vya usalama kutisha wananchi, kupeleka wanajeshi hospitalini bila kutafuta suluhisho la kudumu ni kuwatisha tu raia. Ni sawa tu na kupeleka polisi kuzui mikutano halali ambayo ni haki ya msingi ya kila raia. Kwa nini wanajeshi wetu wasi-reason na wanasiasa hata tu kuwaambia sawa tutatii lakini hili si sahihi. Wanajeshi ni watu very logical sana hivi hawaku-question kabisa moral ya hii hatua ya Waziri Mkuu? Au tusemeje, kuna maslahi binafsi kwenye hili sakata ambayo yanawasukuma wanajeshi kufanya wanavyofanya. Hivi wanafurahia nini katika jambo hili? Nasukumwa kuamini kuwa wanajeshi walioko pale Muhimbili wako kwa kusudi jingine na si hasa kuwasaidia raia, nadhani wako pale standby kuhudumia ikitokea kiongozi fulani ameanguka ghafla au kapata ajali - yaani kabla ya kumpeleka India wanajeshi wetu wampatie walau huduma ya kwanza. Wananchi tusidhani wako pale kutatua matatizo yetu.
 
Naanza kuamini kuwa kunauwezekano mkumbwa Chadema wakawa na agenda ya siri na CCM hasa kwa hili suala na mgomo wa madaktari mbona hatuoni hatua yoyote wanayochukua hasa kuaandaa maandamano nchi nzima kama walivyo fanya kupingamfumuko wa bei au ndio ile mikutano ya Ikulu inafanya kazi watueleze au hawa wanachi wanaokufa hawawezi kuwapigania tunahitaji majibu ya kina kutoka kwa viongozi wa CDM nasimajibu tu tuone na utekelezaji wake kwani tuliona matunda ya maandamano kipindi kile sasa kigugumizi kinatoka wapi? kutoka kwa CDM kama kuna biashara inaendelea na Ikulu basi hamtufai hasilani mtupishe sisi wenyewe wananchi tufanye maamuzi.
 
Hivi kweli hawa viongozi wetu wanaangalia taarifa za habari kwenye luninga..? na kama wanaangalia wanajicikiaje wanapoona wagonjwa wakizidiwa na kufikia wengine kufariki..? wanajacikiaje pale wagonjwa wanapolia kwa maumivu na mateso ya kukosa huduma..? wanajicikiaje pale wagonjwa hao pamoja na ndugu zao wanapoiomba serikali kuwanusuru na dhahama hii kwa kuwacikiliza madaktari na kulipatia ufumbuzi..? wanajicikiaje wanapoona mgonjwa akiwaunga mkono madaktari wanapodai haki yao..? na walijicikiaje pale walipoona mtoto mdogo wa miaka isiozidi 12 ambae ni mgonjwa akishauri wagonjwa wote waandamane kwenda kwa waziri mkuu..? na wana jicikiaje pale wanapoona asilimia kubwa ya wananchi wanaohojiwa wakiitupia lawama hawa viongozi wetu..?
nafikili ikifika sehemu ya matatizo wanafunga macho wasione.
 
Back
Top Bottom