Viongozi wetu wa sasa wana muda kweli wa kujisomea?

JOKA55

Senior Member
Nov 1, 2014
110
74
-Katika maktaba ya chuo nilichosoma kuna section ya maandishi mbalimbali ya baba wa taifa, mwalimu jk nyerere hata aliweza kutafsiri injlili katka biblia (commentary) nilipenda sana kusoma kazi za waandishi wa kiafrika na wangi walikua ni viongozi wa juu wa serikali mbalimbali ndani ya bara letu la afrika

-Viongozi hao ni kama

-Leopold sedar senghor na kazi zake kama; la negritude na nyingine nyingi

-Nelson mandela na kazi zake maarufu kama; long walk to freedom nk

-Kwame nkruma na kazi zake kama; africa must unite, i speak of freedom, nk

-Keneth david kaunda na kazi zake kama; zambia shall be free, a humanist in africa, nk

Jomo Kenyatta na wengine wengi. Kwa kawaida uandishi ni kazi ya kiakili ambayo mtu hawezi kuifanya bila kuwa na uelewa mpana na uelewa mpana hupatikana kupitia hasa kusoma mambo mbalimbali, kuongea na watu na kutembea pia

-Kwa sasa ni nadra sana kuona vitabu walivyotunga viongozi wetu wa leo, mi ni mpenzi sana wa kupoteza muda wangu mwingi pale tanganyika library nikiwa na nafasi, kwa sasa ni ngumu sana kukutana na kazi za uandishi za viongozi wetu

-Hawa viongozi wanapata muda kweli wa kujisomea?
 
Back
Top Bottom