Viongozi wetu sasa hivi wakimung'unya nshale, wakimeza nshale na hata wakitema nshale

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,271
12,568
Nadhani sasa Wamechanganyikiwa, hawana uhakika wa nini wafanye kwenye maeneo yao maana wakikaa kimya wanatumbuliwa, wakiwa wapole kwa wananchi wanatumbuliwa na wakiwa wakali kwa wananchi wanatumbuliwa pia, hadi raha!!. Wako njia panda nadhani, wamejawa hofu, hawana uhakika kama wako sahihi au wanakosea. Unawashauri nini?
 
Hata mimi nimechanganyikiwa. Machinga kwa mfano, (MARCHING GUY!) ni mchuuzi anayefanya biashara yake kwa kutembeza mitaani akiwa ameibeba. Na hawa wapo kwenye miji karibu yote hata Ulaya wapo. Kuchuuza kwa kutembeza sio kosa.

Marching guy hapangi bidhaa zake barabarani, wala hajengi kibanda mbele ya duka la mfanya biashara. Kufanya hivyo ni makosa. Na wanaofanya hivyo lazima waondolewe. Hata kama watatuchukia! Wala Marching guy hatafutiwi eneo rasmi la kufanyia biashara kama gulio vile. Ukifanya hivyo ile dhana ya marching unaiondoa na unatengeneza duka fulani ambapo ni lazima liwe mahali sahihi, lilipiwe kodi na ishuru na pia mchuuzi huyo awe na leseni.

Tukiweka siasa pembeni na hasa ahadi za wagombea ambao walikuwa wanataka kura za kundi hilo wakati wa uchaguzi, ni kwamba utaratibu wa maisha, kufuata sheria na mahusiano lazima vifuatwe ikiwa ni kwa marching guy kutembeza biashara zake na sio kuzipanga barabarani. Kumbuka hawa ni marching guys. If they walk let them walk and sell their goods! Kupanga bidhaa barabarani, kujenga vibanda bila utaratibu katikati ya miji ni jambo ambalo halipaswi kuonewa aibu wala kutumika kisiasa. Kuwaondoa ni lazima. Kule mnakowapeleka ni gulioni na kule sio kwa wamachinga. Mfano mzuri ni majengo waliojengewa pale Ilala yakaitwa ya wamachinga. Wala pale hawapo kwa kuwa dhana yao ni kuuchuuza kwa kutembea! Hiki cha kufurika mjini nakupanga bidhaa ni kitu kingine cha kimakosa kabisa kinachotaka kuchukuliwa hatua.

Hili ni tatizo kubwa la kijamii. Utafiti ufanywe kwamba kwa nini watu wanalundikana mijini bila biashara rasmi zinazolipiwa kodi au kazi zingine rasmi na kwa nini kila kukicha wanaonekana kuongezeka. Tukiwaacha hivyo, kwa woga wa kisiasa, wajae mabarabarani na kupanga bidhaa zao barabarani, hilo ni suluhisho? Waliowatimua kule Mwanza nafikiri walikuwa sahihi! Nimechanganyikiwa!! Tunajenga jamii ya namna gani????
 
Waambie wawe wanafiq tu mpaka 2020 wasirudie tena kufanya ujinga walioufanya 2015!

piga chini mtukufu mungu wa tanzania.
 
Hapo hauhitaji kufanya utafiti wa kujua kwanini watu wanatandika bidhaa zao chini na kutembeza barabarabi, sababu zinafahamika tu wazi kuwa ni:

1. Serikali ilijikita kwenye siasa zaidi kuliko maendeleo ya wananchi- hadi leo hii kusambaza maji ya kunywa ni ahadi za wagombea na kwenye ilani zao za uchanguzi.

2. Maisha vijijini/mikoani yako chini sana hivyo vijana wanakimbilia mijini mara tu ya kumaliza masomo ya darasa la saba, kidato cha nne shule za kata, kidato cha sita na vyuo baada ya kukosa ajira, mitaji na pembejeo. Na mjini viwanda vyote vimekufa hakuna ajira wala mitaji ya biashara, watu hawakopesheki na wanaokopesheka riba ni kubwa sana.

3. Viongozi nao wana njaa na sio wasafi, hivyo wanashindwa kukemea wanaovunja sheria na wenye njaa kama wao pia

4. Serikali inafahamu kuwa hali ya maisha ya wananchi ni mbaya sana hivyo wanaachwa wajitafutie chochote popote wanakokujuwa.

5. Kwakuwa wapiga kura waliopigika kimaisha ni wengi sana hivyo kila mwanasiasa anawania kura zao kwa kuepuka kukosana nao, hata hivyo hii ni solution ya muda tu kwakuwa wanaohamia mijini wanazidi kuongezeka kuliko miundombinu na huduma zilizoko mijini iko siku watawageuka tu wanasiasa pamoja na wale wenye nacho. Itafika siku muda si mwingi wale wenye nacho watanyang'anywa na wasiokuwanacho badala ya kuongezwa.
 
yule wa mwanza bado hajaachia ngazi? kweli njaa mbaya asikwambie mtu, unadhalilishwa lakini umo tu hata kama una Phd. halafu kila siku wanatuambia tujiajili wakati wao wanavumilia matusi na kashfa tena za hadharani ili waendelee na vibarua vyao. Kwa Tanzania hii ukiona mtu kajiajili mpe heshima yake
 
Back
Top Bottom