Viongozi wetu na ndoto za Majinamizi. Wanahitaji Maombi zaidi

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Miaka flan ya nyuma nilipokuwa mdogo sikuwa napenda mtu usiku asimulie habari za kutisha au hadith za kutisha. kama ni filamu pia sikupenda kuangalia filamu za kutisha. nlipokua na kukomaa kiakili nilikuja kuona kuwa vile vitu havikuwa na sababu ya kunitisha nikaanza kuishi maisha yangu mwenyewe na kujikuta hata nikiangalia filamu za kutisha nikilala nalala vizuri kabisa. nilifikia hatua ya kuimiliki hofu (to control fear) usipoweza kuimiliki hofu yenyewe inakumiliki.

tumeona matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi wetu. matamko yanayotokana na ndoto za jinamizi wanazoota usiku. utawasikia kabisa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri na manaibu waziri wanatoa matamko yanayaotokana na ndoto aliyoota usiku. akiamka asubuh anatoa tamko.

waswas wangu ikiwa ataota mimi namkaba usiku kesho yake anaweza toa tamko watu flan wakamatwe ili katika hao nami niwepo nikamatwe aridhishe moyo wake. kiongzo akiota kuwa kua kibaka anamwibia kesho atasema polisi wakamate vibaka wote mpaka atakapohakikisha yule aanayefanana na wa kwenye ndoto amekamatwa halafu zoezi litasitishwa na kuwa ndo limekufa.

najiuliza itakuaje ikiwa kiongozi mmoja ataota usiku anafukuzwa na mbwa? kesho atasema mbwa wote wakamatwe na kuuawa ili kwanzia pale kiongozi huyo asiwe na waswas wa kutembea na kukutwa akifukuzwa na mbwa.

tunasikia matamko mbalimbali. kuna ambaye ameota jambo flan.. atatweet au kuandika facebook. naenda kuoga nikirudi nitahakikisha wale wote ambao majina yao yameanzia na X wanakamatwa. kumbe ni kwa kuwa amekosana na X katika ndoto zake za majinamizi.

woga umekuwa ni tatizo kubwa na hili limefanya viongozi wetu waamini ndoto zao zaidi kuliko uhalisia ulivyo. jambo hili mara nyingi limesababisha tuondolewe kwenye reli na kuacha kujadili mambo ya msingi kitaaluma na kujikuta tunajadili kwa mujibu wa ndoto za viongozi wetu.

viongozi hawa hawana maono. wana ndoto za majinamizi. na ndo maana kutwa kucha wanashindana kwa matamko yasiyotekelezeka, na wao wanaona kuwa wana uthubutu.
 
Back
Top Bottom