Viongozi Wetu Na Ndege Huyu Tulikuliku! ( Makala Raia Mwema) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi Wetu Na Ndege Huyu Tulikuliku! ( Makala Raia Mwema)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Mar 15, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,
  JAMBO moja kubwa ni dhahiri, kuwa Watanzania bado tuna safari ndefu sana kufikia hatua ya kuitwa taifa la kisasa.

  Tuyafanyayo mengi bado ni mambo ya hovyo hovyo, na wenye kuongoza kuyafanya hayo ya hovyo hovyo ni viongozi wetu. Lakini hatuna jinsi, hatua tunayopitia sasa ni lazima tuipitie. Hakuna njia nyingine ya kupita na kutufikisha kwa haraka tunakotaka kwenda.
  Tusisahau tu, kutunza kumbukumbu. Tufanye hivyo ili Watanzania wa vizazi vijavyo waje wajifunze kutokana na matendo yetu.

  Tulikuliku ni aina ya ndege. Viongozi wetu wanaweza kujifunza kutoka kwa ndege huyu. Tulikuliku ana kanuni inayomwongoza. Mara tulikuliku anapotaga mayai, basi, hufanya uamuzi mgumu wa kujinyonyoa manyoya yake. Kwa pamoja, tulikuliku dume na jike watafanya tendo hilo.


  Kwa nini?


  Wanajiwekea wenyewe mazingira ya kushindwa kuruka. Wanafanya hivyo ili waatamie mayai yao hata atakapotokea nyoka mpenda mayai wapambane nae hapo hapo. Kwamba wangebaki na manyoya, huenda wangemwogopa nyoka. Hivyo, wangeruka na kuacha mayai yakiliwa na nyoka.

  Kwa kiongozi kujinyonyoa manyoya ina maana ya kukubali kushuka chini kwa watu. Kuyaelewa matatizo ya watu anaowaongoza. Kuwa tayari kupambana kuyatatua matatizo ya watu akiwa na watu.

  Ilivyo kwa viongozi wetu wengi wa leo, ni kuwa, katikati ya dhiki kubwa ya wanaowaongoza, si tu ‘wamefuga manyoya’ mengi, bali, hata pale wananchi wanapokabiliwa na adui maradhi, wao, viongozi, wana mbawa za kuwawezesha kuruka juu angani huku wakiwaimbia watu wao nyimbo za kejeli. Na bado watafanya hila ili kuwachonganisha na kuwagawa watu wao walio kwenye dhahma ya umasikini.

  Na kuna mawili ambayo yaliwezekana kutumiwa na yakafanya kazi miaka ya sitini hadi themanini, na mawili hayo hata yanapotumika sasa, hayafanyi kazi inayotarajiwa. Maana, wakati umebadilika. Ni yepi hayo?

  Naam, ni kwa kiongozi kutumia uongo na kutishia nguvu za mamlaka. Kiongozi anayetaka kufanikiwa katika zama hizi ni yule aliye tayari na kuachama na mambo ya zama hizo; kuwaongopea watu wako na kutishia nguvu za mamlaka.

  Badala yake, kuwa tayari kufanya maongezi hata na wale ambao huko nyuma haikuwezekana kukaa nao meza moja.

  Vinginevyo, Watanzania tungali na safari ndefu sana. Njia ina miba mingi, lakini ni lazima tuipite. Hakuna njia nyingine.
  Nilipata kuandika, kuwa kwenye Uchina ya kale kulikuwa na mwanafalsafa kwa jina la Comfucius. Katika mafundisho yake mengi aliyopata kumpa mwanafunzi wake Tzu Kung, mojawapo linahusu dhana ya utajiri na uhusiano wake na umasikini.

  Comfucius anasema; ukimwona mtu tajiri (aliyefanikiwa kimaisha), basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe.

  Kwa mwanafalsafa Comfucius, dhana ya utajiri haikuwa na maana kuwa na mali pekee, bali, pamoja nazo, ni uwezo wa mtu kuishi maisha adilifu na yenye fadhila (virtues). Na katika fadhila zote, ile ya unyenyekevu na ukweli ndio chanzo cha fadhila nyingine zote.

  Umasikini vile vile, yumkini unaweza kuwa na maana ya kukosa mali na uadilifu. Ndio, mwanadamu waweza kuwa na mali lakini ukakosa uadilifu. Ni dhahiri, katika hali hiyo, hata mwenye mali naye ni masikini sana.

  Kuna kitu kinatokea katika jamii yetu. Wengine wanakiona, wengine hawakioni. Wengine wanakiona lakini hawataki kukiona. Na kuna wanaoonyeshwa, lakini wanashindwa kukiona.

  Tunafanyaje?

  Hakuna kitu kingine bali ni watu ndio wenye kuifanya nchi. Kuna kitu kimetutokea Watanzania. Kinaendelea kuota mizizi. Na kwa vile kitu ndicho hufanya vitu, basi, mimi naviona vitu vya hovyo hovyo vikitokea katika jamii yetu. Na pengine, kwa vile tumeanza kuwa na hulka za hovyo hovyo, basi, vinavyotokea hatuvioni kuwa ni vya hovyo hovyo.

  Naam, vinatokea kila leo, na kuna wenye kusimama kuvitetea vitu hivyo vya hovyo hovyo. Ni kuanzia namna tunavyouza rasilimali zetu. Na wenye kuuza, ni viongozi wetu waliogeuka ‘madalali’ wa kutanguliza tenipasenti. Hawa wa kundi la pili ndio matajiri wetu wapya . Ni watu waliopungukiwa chembe nyingi za uadilifu, hivyo basi, nao ni masikini.


  Na tumeimbiwa sana, kuwa nchi yetu ni masikini (japo wanamaanisha kipato pekee). Wenye kutuimbisha wanasahau, au labda hawajui, kuwa sisi ni masikini zaidi kwenye maadili.

  Katika wakati huu tunaoenda nao, na tujifunze kutoka kwa mwanafalsafa Comfucius. Kwamba katika umasikini wetu huu kama taifa, basi, walau tujitahidi kujitafakari tulivyo huku tukiwaangalia wenzetu waliopiga na wanaondelea kupiga hatua za mafanikio ya kiuchumi.

  Maana, nasi tutamani kuwa taifa la kisasa. Lakini hatuwezi kuwa taifa la kisasa kwa staili hii tunayoenda nayo. Oneni kule Marekani. Hawa ni matajiri wa kipato. Wanafanya kazi usiku na mchana kutimiza ndoto ya taifa lao. Wamarekani wanaijua ndoto yao na huungana dhidi ya yeyote anayetaka kuikwamisha. Na pengine ni katika kutimiza ndoto hiyo sisi tunalalamika kuwa Marekani ni taifa baya.


  Tujiulize; ni taifa gani litaishi bila kuwa na ndoto na haja ya kuwa na maslahi ya kudumu? Hivi, ni nini ndoto na maslahi ya kudumu ya Tanzania? Je, ni Watanzania wangapi wakiwemo viongozi wanaijua sera ya Tanzania inapohusu uhusiano wake na mataifa mengine?

  Fikiri, tumepeleka majeshi yetu kuzikomboa nchi nyingine, lakini, ni vigumu kuona tumepata nini kiuchumi ukiacha sifa ya kuwa ni taifa karimu.

  Angalia Rwanda. Ni kanchi kadogo sana lakini kameshajua ni nini maana ya kuwa na ndoto na haja ya kuwa na maslahi ya kudumu. Ndio maana hukusikia Rwanda ikitafuna maneno katika kuitambua Serikali ya Mpito ya Libya.

  Leo Rwanda wako ndani ya DRC na wana maslahi ya migodi ya madini ya huko. Wanyarwanda wale wamepenya hadi Uganda na Burundi. Na nani atabisha, kuwa Wanyarwanda wamepenya hata kwenye uchumi wetu.

  Tumekuwa ni watu wa hovyo hovyo. Tupo kama hatupo. Tunayakimbia mambo ya kimsingi kwa taifa letu. Tumejikita zaidi kwenye hoja nyepesi nyepesi ikiwamo fitina na majungu. Ndio, Watanzania tunabaguana kisiasa na kuna ambao, piga ua, watahakikisha tunapata Katiba Mpya ya hovyo hovyo ili tuendelee na mambo yetu ya hovyo hovyo. Nahitimisha.
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
  0788 111 765
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Well said brother Mejngwa,
  Kizazi kijacho huenda kitaleta ukombozi wa kweli kwa watanzani ingawa ukombozi huo huenda ukaambatana na umwagaji damu sioni kama utakuwa ukombozi lelemama, Mpaka hapo ndipo nchi itapoanza kujengwa upya kwa maana ya pato la taifa, mtu mmoja mmoja na miundombinu kwa ujumla. Nimestuka sana nilipoona ile barabara ya Arusha Namanga inayojengwa leo 21 century eti bado si ya njia nne bali njia mbili tu hii ni aibu na uchungu, Nilifikiri nchi kama hii yetu tukijenga barabara basi tumaanishe, Barabara inayotuunganisha na nchi Jirani ilitakiwa kuangalia kesho katika ujenzi, anyway watu wanafanya mambo ya hovyo hovyo again well said.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Barabara ya njia nne kwenye long routes ya nini? ona tafakari , nena. Iko siku utasema barabara za kutoka dar kwenda mikoani nazo ziwe njia nne. Sidhani kama itakuwa na mantiki kweli.
   
 4. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  Ukweli mtupu kaka Mjengwa.Tukutane Raia Mwema lijalo...
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu naona msamiati wa leo ni neno "HOVYO"
  Tusijidharau kiasi hicho, kufanya hivyo ni kudhihirisha kwamba kweli watanzania tuko hivyo, jambo ambalo si kweli. Yapo mambo mengi tu ya maendeleo yamefanyika. Zipo changamoto nyingi tu ambazo kwa namna moja au nyinginge ni vikwazo vya kufika huko ulikosema Mkuu. Utandawazi, mabadiliko ya mifumo ya kisiasa, uchumi , kijamii na mengine mengi. Jukumu la kukabiliana na changamoto hizi si la mtu mmoja mmoja, si la viongozi pekee, na si jambo linaloweza kuonekana kwa macho yetu. Madiliko ya kifikra ni muhimu sana katika hili. Tuwe tayari kufanyakazi kwa bidii badala ya kua walalamikaji, tuwe tayari kuona umunimu wa kushirikiana na watangulizi wetu na kuweka kando mawazo ya kujitakia umaarufu wa mtu mmoj mmoja, tuwache kuhujumu jitihada zozote zinazofanywa za kulisogeza taifa katika hatua moja ya maendeleo na mengine mengi.
   
 6. k

  kaka dj Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bravo mkuu, Tafakari ni ya kina na inatoa changamoto kwa kila mzalendo wa kweli.

  Ni ukweli usifochika kuwa mambo ya HOVYO HOVYO katika nchi hii ni mengi, ni wakati wa kila mtu afunge ayaone na tuwe na mikakati chanya ya kukabilana nayo. Mfano mmoja wa mambo ya hovyo na tena ni hatari kwa Taifa letu ni jinsi mfumo wa elimu yetu unapochezewa, tazama walivyo lazima wanafunzi wote/wengi wa shule za msingi hata wasiojua kusoms na kuandika kujiunga na utitiri wa shule za kata zisizo na walimu wenye tija na maslahi duni waliondaliwa kwa mtindo wa zima moto na vitendea kazi haba na matokeo yake ni kuwabwaga nje ya duru la elimu kwa kufeli kwa wingi wakiwa wamepotaz muda wao bure waswe na matumaini tena katika maisha yao ya baadae. Tazama mitaala ya elimu ilivyogeuzwa geuzwa kama vitumbua.
  Tafakari Mtanzania. Mambo ya Hovyo ni mengi.
   
 7. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wewe ni mmojawapo ya watu wanaotetea mambo ya hovyohovyo yanayoendelea hapa tz.uko tayari kutetea kitu ambacho hukiamini ili mradi ushibishe tumbo lako...kama watu wanafanya mambo kwa bidii kuongeza kipato na wanakatwa kodi kubwa ambayo inaishia mifukoni mwa viongozi wa hovyo tutafika kweli?tukiwa na watu kama hawa hatufiki popote
   
 8. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu umejibu mchango wako kwa sababu ya ushabiki au labda hujatembea duniani ukaona bara bara zilivypendeza hugh way zimeachana mbali wanao enda wanapishana mbali na wanao rudi.
  au hujui faida za sasa na baadae kuhusu double way traffic nikusaidie 2 tu
  1. itaepusha sana ajali za uso kwa uso au labda hauna taarifa za ajali nyingi zilizotokea za mabus
  2. itakuwa ni mipango mizuri kwa vizazi vya baadae kimaendeleo ebu ona leo bara bara za miji yetu zilivyo finyu watu wanumiza vichwa kufikiria wafanyeje kuzuia trafic jama ona dar na miji mingine....wangepanga ziku za huko before leo isinge kuwa taaabu

   
 9. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  tupe mifano ni kitu gani viongozi wetu wanatuelekeza au wanajuwa lini tutakuwa wapi au tutafanya nini ,angalia umeme tu umetushinda angalia ahadi za waziri mkuu na mawaziri kwenye bunge la budget ni vichekesho.ahadi nying hazina time frame

   
 10. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Siku zote nitaendelea kusema kuwa tatizo kubwa kuliko yote TZ si sera wala mifumo pekee bali WATU.....watu wa TZ ndio wenye kuleta matatizo ya TZ......hamna kingine.......watu wa TZ ndio wenye kutengeneza na kusimamia mifumo/sera mbovu......watu wa TZ ndio wanaokwenda kwenye sanduku la kura kupiga kura kuwachagua watu wa kuwaongoza.........watu wa TZ ndio wenye kuchakachua matokeo ya kura......adui wa TZ ni mtu wa TZ......period....
   
Loading...