Viongozi wetu na mwavuli wa amani

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi bila majibu nini maana ya amani ninavyojua palipo na amani hapakosi upendo imekuwa kama mchezo wa kuigiza watu wakitaka kupatiwa haki viongozi wanakimbilia kudai amani wezi wa epa wananchi wakitaka washtakiwe anasimama kiongozi anakuambia nchi itatikisika tukitaka mabadiliko wanaibuka wakidai amani kama kweli nchi yetu ina amani wangapi wamebambikiwa kesi na wapo magerezani wakitumikia vifungo amani wanaoililia viongozi itatoka wapi kama nchi haisimamii haki watu wanauwawa, wototo wanabakwa, wajane wanadhulumiwa, yatima hawapewi haki zao na hakuna wa kuwasaidia hakuna usawa tabaka ni kubwa ya walionacho na makabwela amani hapa itatoka wapi katika mioyo iliyopondeka namna hii viongozi wetu mtambue uongozi na dhamana tuliyowapa na haki siku zote huinua taifa msikwepe matatizo kwa kutumia mwavuli wa amani hapa hatuna amani bali tuna woga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom