Viongozi wetu na misaada kwa jamii iliyo na uhitaji

Makene

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,475
282
Hivi karibuni kiongozi mkuu wa nchi alitoa 10millioni rambirambi kwa ajili ya msiba wa msanii Kanumba.
Kwenye taarifa ya habari ya saa mbili TBC, ameonyeshwa mama mmoja mwenye tatizo la kuvimba mkono, ambao unahitaji kukatwa. Na hii si mara ya kwanza kuonyeshwa kwenye taarifa ya habari.
Maoni yangu, sioni kwa nini mama huyu awekwa kwa taifa zima kwa ajili ya msaada wa millioni 2. Wako wapi viongozi wetu wawakilishi wa serikari; mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na viongozi wengine wa kisiasa kama mbunge wake.
Tumekuwa tukiona harambee mbali mbali za ufahari wa michango ikifanywa. Haingii akilini mama huyu kudai kukosa msaada ilhali viongozi wa wananchi wapo. Sioni kama viongozi wetu wanastahili kuendesha magari ya kifahari ,kuishi kifahari na kushindwa kutoa msaada kwa mama yule mhitaji.
Haiingii akilini hata kidogo kuwa na serikari.
 
AFADHALI KANUMBA ALITUOKOLEA SAFARI MOJA YA ULAYA AMBAYO INGEGARIMI MARA MIA YA HIZO MILIONI 10.huyo mama atajifia tu kwani haki yake aliiuza kwa kanga na pombe.
 
naogopa kusema kwa kuwa kwenye msiba wengi hutoa rambirambi kwa kujionesha na si kwa nia ya kuwatia moyo wafiwa kwa pengo aliloacha aliyetangulia maana ukitafakari kwa undani hata hizo pesa wanazotoa kwa wafiwa hazizibi pengo la mwanadamu husika kwenye familia husika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom