Viongozi wetu Hotuba Zao wawe Wanaandika Maana Awamu Hii Ya Tano Hotuba Nyingi Ni Za Uropokaji.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Nimeshuhudia Awamu Hii ya Tano Ya uongozi wa Nchi Yetu ya Tanzania imepata Viongozi wenye kutoa hotuba za Uropokaji. Nazani wakipitia kusikiliza hotuba zao watakuwa wanajuta matamshi yao na kujiona wajinga wasiofikiri chochote.

Nikikaa na kufikiri nini Chanzo cha kuwa na Hotuba za ajabu zenye kutoa maneno ya hovyo, Ya hovyo na yaliyojaa kejeli kwa wananchi. Nikagundua Hotuba zao haziandikwa ndomana wanaropoka vitu vya hovyo kabisa wakiwa wanaongea.

Uropokaji huu unaanza toka kwa Rais wa Nchi yetu, waziri mkuu na mawaziri wengi wa serikali hii ya magufuli, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu a wilaya, Wakurugenzi nk.

Tunaomba viongozi wetu wawe wanaandika hotuba, waipitie kabla ya kuisoma kwenye hadhira ya watu, maana nimegundua Viongozi wengi wa Awamu hii ya Tano Ama uwezo wao wa kufikiri mdogo sana au wanasema mambo kwa uoga wa kutumbuliwa hivyo hulzimishwa kusema chochote ili kumfurahisha bwana mkubwa.
 
Tena hizo za kuandika ndo zimetufikisha hapa tulipo(vyeti feki, watumishi hewa, mitumba kumbe ndani magari ya kifahari nk.). Hatutakula hotuba
 
Back
Top Bottom