Viongozi wetu (CCM) waliopo madarakani waendelee kutawala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wetu (CCM) waliopo madarakani waendelee kutawala?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mnyakaye, Oct 2, 2012.

 1. m

  mnyakaye Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na nchi yetu Kutamkwa kuwa ni nchi ya amani, nchi iliyopata uhuru miaka 50 iliyopita, nchi ambayo mbali na vita na utawala wa Idd Amin Dada wa Uganda haijawahi kuwa na msukosuko wowote wa kitaifa bado hali ya ustawi wa watu wake ni tete. Maendeleo yaliyopo hadi sasa hayaendani na hali halisi ya matumizi ya Raslimali za Taifa zilivyopotea. Viongozi wetu wameongoza katika kutuibia raslimali za nchi hii kiujanjaujanja. Angalia Afya,Elimu, Miundombinu, Utalii, Bei za bidhaa za matumizi za kila siku n.k

  Leo BBC imetangaza kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JOMO KENYATTA ndio uwanja bora kati ya viwanja vya ndege katika Bara la Afrika. Hawa hawana mlima Kilimanjaro. hawana mbuga za wanyama kama serengeti, hawana KANU n.k.
  Wallah, viongozi wetu ( CCM ) hawajatutendea haki nashauri tuwaondoe kwa njia ya kura katika box.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tatizo sio serikali pekee Watanzania pia wana tatizo kubwa hawajui mfumo wa nchi ambao wanataka. Huwezi kuweka sera nzuri za maendeleo kama hujui mipaka ya serikali. Watanzania wanataka kila kitu kifanywe na serikali halafu tunalalamika utendaji?. Swali hii lazima lijibiwe kabla ya maendeleo Je Watanzania wanataka serikali ya namna gani? Je serikali inatakiwa kufanya vitu gani hasa 1,2,3 bila hili ni porojo tu
   
 3. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania wanapiga kura kama vipofu halafu wanalalama kama vichaa! (Generali Ulimwengu)
   
 4. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Kwa watanzania wengi tuliopigika na "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" tunapomsikia mtu mzima anashabikia na kushanglia CCM (mafisadi sugu) ni sawa na kumwona mzazi wa kiume (baba) wa miaka 50 akimlawiti mwanae wa kiume wa miaka 4 kisha ukawa unamshangilia na kumpongeza mzazi huyo.

  CCM haina tofauti na mzazi wa jinsi hiyo, CCM wameifisidi nchi hii hadi inashindwa kutembea. Na kibaya zaidi mafisadi hao hushangiliwa na kuajabiwa. Nchi yetu imetobolewa kila mahali; kila raslimali zetu zimelawitiwa na hawa mafisadi. Hakuna palipobaki, makampuni ya migodi yameanza kuaga, yameitoboa ardhi yetu; waarabu wameharibu mbuga zetu, wameiba wanyama wetu nk.

  Hebu, tuache kuwaona ni mashujaa watu wanaolawiti watoto wao. Tuwanyongelee mbali 2015.
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  CCM ya Nini?tunataka iondoke.Jeshi letu na Usalama wa Taifa uboreshwe.Waanze kuwa wana produce technologies mablimbali za usalama ambazo tutaweza uza nje.Waanze jenga concrete structures na si hizi camps zinazoitwa "bwalo" kama vile wapo ugenini.Waanze tengeneza hela kwa kutoa training mablimbalia duniani.Waanze kuwa na heshima ya wazi kwa mataifa duniani.


  Waanze ongoza nchi katk michezo,ufundi, shule za urubani, maeneo ya uokoaji etc.pamoja na tafiti nyingine na si kuwalinda CCM na kufanya magwaride hukuwa wakiwa wanafunzi wa technology,wasiwe tena wanatumiamagari ya kisasa toka nje ambayo yanawaweka wazi ktk kuchunguzwa na nchi zinazotoa hizo technology na wanaweza tuzimia siku tunapigana na marafiki zao.
   
 6. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe nae una matatizo gani? mtu anae dhalilisha na kubagua kwa kunyanyapaa walemavu unamfanya kuwa mtu wa kutolea mifano kwenye suala la mstakabali wa taifa?

  Huyo mzee nilikuwa namuheshimu sana, lakini kauli zake zinazo sababishwa na kuzeeka vibaya ndio zinamvunjia heshima na utu kwa watanzania.
   
 7. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  uwanja wa JOMO KENYATTA ndo uwanja bora afrika nzima? upo serious au unatania. nadhani bado hujaenda south africa. unajua kwamba 2010 world cup walitengeneza viwanja vyao vyote. BBC uliyosikia wewe itakua ya kichina.
   
Loading...