Viongozi wengi wa Serikali za Mitaa wapiga dili. TAKUKURU wamulikeni

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,786
4,421
Salaam Wakuu,

Leo kijana wenu nimeona niseme kidogo kuhusu kero ya rushwa na kutaka chochote kitu kwa Viongozi wengi wa serikali za Mitaa wakiwemo Wenyeviti, Wajumbe, Watendaji na wengineo wa ngazi hiyo.

Kumekuwa na muendelezo wa tabia ya viongozi hawa kutaka pesa kidogo (rushwa) kila wanapohitajika kutoa huduma mbalimbali kwa Wananchi. Viongozi hawa wakekuwa wakitumia mahitaji na shida mbalimbali za wananchi wa mitaa yao kujipatia pesa ndogondogo. Mfano, Ikitokea labda unahitaji barua ya utambulisho wa serikali ya mtaa wako baadhi yao wanagoma mpaka utoe kiasi fulani cha pesa. Cha kushangaza hapa unakututa huduma hiyo moja kuna mtaa kiongozi anataka 3000, mtaa mwingine 5000 mwingine 10000 n.k. Hii inamaanisha hakuna utaratibu maalumu wa suala hili kinachobaki tu ni uwezo wa kiongozi binafsi kujipangia bei yake ya kuhudumia au kupiga dili lake.

Jambo kubwa nalojiuliza hapa ni je viongozi hawa wa Serikali za Mitaa hawana mishahara? Je, pesa hizi wanazochukua bila kutoa risiti yoyote zinatambulika kisheria na kikanuni?

Nafikiri ipo haja ya Takukuru na Mamlaka nyingine zinazohusika kutupia jicho na kuchukua hatua jambo hili. Pengine kwa wengine pesa hizi zinazotolewa zikawa ndogo na haziwaathiri lakini tutambue kuna Wananchi ambao hawana pesa hizi na wanakwama kupata huduma za msingi kutoka kwa viongozi wao.

Fikiria mtu unapata fursa ya kazi ndogo tu sehemu na wanahitaji utambulisho kutoka mtaa wako halafu unakwama kisa hauna hela ya kumpa kiongozi ili akuandikie barua ya kukutambulisha.

Vipi wewe mtaani kwako yapo haya?
 
Back
Top Bottom