Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Kigwangalla ni msomi akiwa Daktari wa binadamu, jana akiwa awamu ya tano alitueleza kupiga nyungu ni sawa na hakukemea mtambo wa Nyungu kuwekwa Muhimbili. Leo siku 17 tangu Mhe. Rais aondoke madarakani anatoka hadharani nakusema ule mtambo uondolewa na tufuate taratibu za kitaalamu. Huyu mtu anaanzaje kuitwa mzalendo au kukabidhiwa madaraka ya kuongoza watu?
Mrisho Gambo miaka yote mitano ya Magufuli alineemeka na alishiriki siasa zote chafu dhidi ya wakosoaji wa mzee. Leo less than 20 days tangu mzee aondoke anajitokeza hadharani kupingana na sera ya kibiashara na uchumi ya awamu iliyopita. Hivi kweli huyu anafaa kupewa uongozi?
Mwigulu Nchemba amezolea sifa kwenye mitandao za kuchora X kwenye hoja kuntu za wapinzani wa mfumo wa Serikali iliyopita, alisimama kidete kupigia chapuo mfumo wa ukusanyaji Kodi wa mabavu wa Awamu iliyopita, leo anawaambia wafanyabiashara warejeshe imani kwa Serikali na wapeleke fedha benk, simple like that?
Ndugai mtu wa karibu wa Mzee naye anapita kulekule yeye na Naibu wake kukubaliana kwamba mzee alikosea wakati wao ndio walikuwa wapiga makofi na kusifia.
Kabudi aliyekuwa anawaita waliojiweza mabebetu Leo kawa kimya akicheza ngoma kulingana na mfundo. Uprofesa kazi yake nini Kama elimu haiwezi kulipeleka Taifa njia sahihi?
Tukiendelea kuwasifia nakuwaunga mkono watu wa aina hii wataliangamiza Taifa. Tujitokeze nakuwapinga adharani wajue wanakosea. Tuache kuishi kinafiki Kama wanavyotufunza.
Pasaka njema.