Viongozi wengi Duniani wamekuwa wakiishi zaidi ya miaka sabini; Tanzania ni kama vile viongozi wanaanza kuishi chini ya miaka sabini; Tumekosea wapi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
875
4,101
Ukisoma vitabu vitakatifu utabaini viongozi wengi walibarikiwa vipawa, nguvu na maisha marefu. Utabaini viongozi wengi wanaombewa waishi sana; utabaini kwamba viongozi wengi walikuwa wana ulinzi wa Mungu naturally.

Ulinzi huu usionekana ulikuwa unawasiaidia viongozi husika kuyaona maisha ya waliowakabidhi madaraka na kushauri. Hata sasa ukiangalia viongozi wengi waliohudumu na mwalimu bado wapo; waliohudumu na Mwinyi wapo pia. Lakini viongozi wengi waliohudumu na Awamu ya Tatu hadi awamu ya sita hatuwaoni.

Ni kipindi hiki ndipo Taifa lilipoanza kuvuruga amani kwa kukiuka masharti ya uchaguzi na kukataa kabisa kukubaliana na sanduku la kura. Ni kipindi hiki ndicho wanasiasa walipoteza malengo na kuhama vyama kutafuta madaraka. Ni kipindi hiki ndipo watu walilazimishwa kuunga juhudi mkono.

Katika mazingira haya ambayo uaminifu wa jamii kwa kiongozi unashuka ndipo inapozaliwa dhana hasi miyoyoni mwa watu yakutowaombea mema viongozi wao. Ndipo inapozaliwa dhana kwamba viongozi wanalogeka na kuuwawa. Kitu ambacho zamani ilikuwa mara chache.

Nataka kusema nini; TANZANIA VIONGOZI AWATOKANI TENA NA MUNGU, VIONGOZI WANAJISIMAMISHA KWA NGUVU ZAO BINAFSI, NGUVU ZA NDUGU ZAO PAMOJA NA NGUVU YA FEDHA. MATOKEO YAKE WANAKOSA ULINZI WA MUNGU AU MIUNGU KULINGANA NA AINA YA IMANI ZAO.

TUFANYE NINI; Tumrudie Mungu, tumuulize tumekosa wapi? Tusipomrudia Mungu viongozi wengi wataendelea kupata mapigo kwa kiwango kile kile wanachowapa mapigo wananchi. Ogopa sana kuwa na kiongozi ambaye Wananchi wanamwombea Atimuliwe, aondolewe ofisini au hata kuugua aje mwingine......hii siyo hali nzuri. Tunapaswa kuombea taifa liwe na viongozi ambao wanamsada kwa jamii kiasi kwamba kila ukipita wanatajwa kwa wema.

Katika mtizamo huu tujione tulikuwa Taifa Teule na sasa tumejitenga na uteule
 
Kifo ni hatua ya mwisho katika maisha ya mwanadam hivyo hakuna umri maalum wa kifo Cha mtu

RIP viongozi wetu walio jitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa
 
"Watu waliogopa hata kuachiana glasi mezani"; watu wa aina hiyo unategemea nini?
 
Back
Top Bottom