Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Polisi mkoa wa Iringa inawashikilia viongozi wawili wa chama cha mpinduzi CCM Mkoa, kwa tuhuma za wizi wa fedha za mradi wa viwanja vya Umoja wa Vijana UVCCM mkoa.Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na uwepo wa tuhuma za Viongozi hao kuhusika kuuza kinyemela eneo la viwanja lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 200.
Sakata la kukamatwa kwa viongozi hawa – limeingia katika sura ya mpya, na hiyo inatokana na shamba la umoja wa Vijana – UVCCM mkoani Iringa, shamba lililokuwa na ukubwa wa zaidi ya ekari 200 kubadilishiwa matumizi na hivyo kuwa ni Viwanja.
ACP John Kauga ni kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa- anazungumzia sakata la kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na biashara hiyo ya Viwanja
Awali Hassan Mtenga katibu wa CCM Mkoa wa Iringa akizungumzia juu ya tuhuma za uuzwaji wa viwanja hivyo vilivyopo katika eneo la Igumbilo mjini Iringa alisema.
Aidha Mtenga aliwashauri wale wote walionunua Viwanja katika eneo hilo la UVCCM na kutoa rai kwa waliohusika katika biashara hiyo ya uuzaji wa viwanja hivyo kinyemela.
Chanzo: StarTV