Viongozi wastaafu, wapinzani wamshauri kwa Rais Kikwete

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,849
Posted Date::2/9/2008
Viongozi wastaafu, wapinzani wamshauri kwa Rais Kikwete
Na Andrew Msechu
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wameshauriwa kuhakikisha kuwa mawaziri na wabunge wanaotajwa hata kwa hisia katika kashfa za ufisadi hawarejei katika Baraza jipya la Mawaziri linalotarajiwa kutangazwa kesho.

Ushauri huo umetolewa katika kipindi cha yaliyotokea bungeni kilichorushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa.

Walioshiriki mjadala huo wakiwamo viongozi wastaafu na baadhi ya wabunge, walipendekeza kwa pamoja kuwa ni vyema baraza hilo liwe dogo ili kupunguza mzigo kwa Watanzania.

Kipindi hicho kiliwajumuisha Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe waliokuwa Dar es Salaam pamoja na wabunge Anne Kilango (Same Mashariki), Lucas Selelii (Nzega) na Kiongozi wa Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.

Katika mjadala huo, Mbowe alisema kutokana na yote yaliyotokea kwa wiki nzima hii, ni vyema mabadiliko makubwa yakafanyika katika kuhakikisha kuwa nchi haitumbukizwi tena katika matatizo ambayo Watanzania wameyashuhudia.

Alisema kwa sasa zipo kashfa nyingine kubwa ambazo zinasubiriwa kushughulikiwa na kuendeleza uwajibikaji, ikiwamo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na mikataba ya madini, hivyo kuwapo haja ya kuangalia uteuzi unaotakiwa kufanywa na rais katika Baraza jipya la Mawaziri.

“Mtiririko wa uwajibikaji unatarajiwa kuendelea punde baada ya kukamilika kwa uchunguzi unaoendelea kwenye kashfa za BoT na mikataba ya Madini, ni vizuri rais asijaribu kuwaingiza waliokuwa mawaziri au wabunge ambao wamekuwa wakitajwa hata kwa hisia katika kashfa zote hizi,” alisema.

Jaji Warioba aliisifu kazi ya kamati ya Mwakyembe na majumuisho yake, lakini aliituhumu kwa kutomtendea haki Waziri Mkuu aliyejiuzulu kutokana na nafasi yake katika utendaji.

Warioba alisema kuwa uzuri wa kazi ya kamati hiyo unatiwa doa na kutaka siku za baadaye hilo liwe funzo, kwa kuwa anaamini suala la Richmond ni sehemu tu ya mtiririko wa matukio makubwa yanayotarajiwa hivi karibuni.

“Ripoti ya kamati ni nzuri sana, ina mtiririko mzuri unaoeleweka, kwa ukweli ni kwamba hata kama wasingemtaja waziri mkuu kwa taarifa ile asingekwepa kuwajibika, lakini wangetenda haki zaidi iwapo wangempa nafasi na kumhoji na yeye,” alisema Warioba, kauli iliyoungwa mkono na Mbowe na Butiku.

Katika mapendekezo yaliyotolewa katika mjadala huo ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuangalia namna ya kukaa na kamati hiyo na kutafuta namna nyingine ya kupata maelezo yake, pia maelezo hayo yawekwe wazi kwa Watanzania iwapo ameonewa au vinginevyo.

Mbunge Anne Kilango Malecela aliyekuwa akizungumza moja kwa moja kutoka Dodoma alisema kuwa, huo ni mwanzo wa ukombozi wa Watanzania kwa kuwa sasa wamechoka kulinda watu ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao ndani ya chama kuwanyamazisha wabunge ili kulinda ufisadi wao.

Alisema hatua iliyofikiwa sasa inatokana na uamuzi waliochukuwa wa kuvunja wigo wa kulinda maslahi ya watu binafsi kwa mwavuli wa chama, baada ya kunyamazishwa kwa muda mrefu na kutowatendea haki Watanzania.

“Tulikuwa tunazuiwa kuzungumza mambo muhimu bungeni, niliwahi kuuliza swali nikaandikiwa barua muda huo huo nikiitwa na kuambiwa nisirudie kuzungumza mambo hayo bungeni bali kwenye chama, lakini baadaye niligundua kuwa suala siyo chama, kumbe tunatakiwa kufanya hivyo kulinda maslahi ya watu wachache na si chama,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa hawatakubali kuwa raba chafu kwa kulinda watu wachafu, bali wataendelea kutetea maslahi ya chama na serikali, akiahidi kufanya mambo makubwa zaidi kwenye suala la BoT na kuibua hoja zaidi katika Bunge hili, ikiwemo kuangalia hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa.

Mjumbe wa kamati teule ya Richmond, Lucas Selelii alisema kuwa kamati hiyo iliyofanya kazi kwa siku 45 iliweza kugundua uozo mkubwa kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kutokana na udhaifu na dalili za kuwepo kwa rushwa na kujuana ndani ya taasisi hiyo na kuamua kuficha ukweli.

“Suala la taarifa ya Takukuru iliyoisafisha Richmond lilitushangaza sana, tulishindwa kuelewa kuwa inakuwaje sisi tuliofanya kazi kwa siku 45 tukaweza kugundua mambo mengi kiasi kile kuliko wao waliofanya kazi kwa miezi sita lakini hawakuweza kutoa kile tulichokisema sisi, hii kama taasisi haikuwatendea haki Watanzania,” alisema Selelii.
 
Posted Date::2/9/2008
Viongozi wastaafu, wapinzani wamshauri kwa Rais Kikwete
Na Andrew Msechu
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wameshauriwa kuhakikisha kuwa mawaziri na wabunge wanaotajwa hata kwa hisia katika kashfa za ufisadi hawarejei katika Baraza jipya la Mawaziri linalotarajiwa kutangazwa kesho.


“Suala la taarifa ya Takukuru iliyoisafisha Richmond lilitushangaza sana, tulishindwa kuelewa kuwa inakuwaje sisi tuliofanya kazi kwa siku 45 tukaweza kugundua mambo mengi kiasi kile kuliko wao waliofanya kazi kwa miezi sita lakini hawakuweza kutoa kile tulichokisema sisi, hii kama taasisi haikuwatendea haki Watanzania,” alisema Selelii.

Tusubiri hiyo jumangapi, kupata suprises.
Naona tukelele twa chura tumeanza kuwasumbua kunywa maji.
Tukaze buti hadi kieleweke.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom