Viongozi wasiothamini umuhimu wa umoja wetu, ni janga

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Mabibi na mabwana haipo namna jamii inaweza kupata mafanikio yoyote ya maana bila ya kuwekeza kwenye umoja wa kitaifa kwanza.

Vita dhidi ya ubaguzi wa kikabila, kikanda, kidini, kijinsia, nk, ni mwendelezo wa wenye akili zao katika kusaka maendeleo endelevu katika jamii zao.

Zidumu fikra sahihi za mwalimu Nyerere (rip).

Kutegemea mafanikio tokea katika kuwagawa watu, kukwepa maridhiano ya dhati, kuuwa misingi ya demokrasia, kupalilia chuki nk, kwa namna yoyote ile hakutatuvusha.

Kwamba Zanzibar bwana yule anaonesha kuziba masikio na macho ili kujidanganya kuwa kila kitu ni sawa? Kila kitu si sawa Zanzibar na pasipokuwa na maridhiano ya kweli basi yetu macho.

Kwamba bwana huyu naye ndiyo huyo na maprofesa wake mabingwa wa mipasho? Kwamba uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na kuaminika eti kuwa bora kabisa kuliko huko kuliko wanakoita chaguzi zenye kura za posta?

Kwamba hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawaoni umuhimu wowote wa utangamano wala maridhiano?

Basi na tusubirie majibu kutoka kwa watu waliovunjika nyoyo.
 
Mbona umeandika utopolo, Watanzania hatunaga masiala na wanaojitahidi kuharibu amani ya nchi yetu ikiwa ni sehemu ya kuwafurahisha wanaowatuma kufanya hivyo.

Inajulikana na iko Wazi kuna Watu kule Zanzibar wanafunga na kuomba ili Babu zao Masultani waiteke Zanzibar.
 
Mbona umeandika utopolo, Watanzania hatunaga masiala na wanaojitahidi kuharibu amani ya nchi yetu ikiwa ni sehemu ya kuwafurahisha wanaowatuma kufanya hivyo.
Inajulikana na iko Wazi kuna Watu kule Zanzibar wanafunga na kuomba ili Babu zao Masultani waiteke Zanzibar.
Watanzania wapi unaowaongelea wewe:

Ni:

1. Ma lb7 au mataga?
2. Wapenda haki na uhuru?
3. Wachumia tumbo?
4. Wachumba wa kiume walio tayari kuolewa?
5. Wezi wa chaguzi?
6. Wasaka teuzi?
7. Mamburula wsioelimika wala kujua haki zao?
8. Maprofesa njaa wa majalani?
9. ..

Epuka kutumia neno "watanzania" hilo na sisi wapenda haki tumo. Tafadhali usituongelee kabisa mburula wewe!

Wewe ndiye uliyendika utopolo mtupu.

Habari za kukaririshwa na magenge ya wanyang'anyi hizo si kila mtu anazinunua!
 
Juzi Dodoma kaleta ubaguzi mpya wa umri...”wazee hawawezi kuwa maraisi “ulisikia wapi....
 
Back
Top Bottom