Viongozi wasiokubali kuwajibika ni madikteta mamboleo!

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
Hivi Mzee Ali Hassan Mwinyi kukubali kuwajibika wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani halikuwa somo kwa taifa????????? Tujifunze nini kwa mtoto wake kutamka kijeuri kwamba hajiuzulu kwa suala nyeti hili la majanga ya kitaifa ya Mbagala na G/Mboto katika uongozi wake??

Jibu la rahisi ni tabia ya UDIKTETA ambao ulianza wakati wa Mkapa na sasa kukuzwa na Kikwete. Huu ndiyo mzizi wa majanga mfululizo maana kama viongozi hawakubali kuwajibika matokeo ni taifa lisiloheshimu sheria!

Ndiyo maana hata bungeni uvunjaji wa sheria ni jambo la kawaida! MATOKEO TUTAMALIZANA jamani; ni utaifa kwisha!!!
 
Wewe kama sehemu ya nguvu ya umma una uwezo wa kumwondoa huyu Mwinyi, hata akisema kuwa hajiuzulu!
Hebu watu waamue kwa siku 2 tu kuingia vichochoroni kama hajakimbia huyu!..Ni dhamira tu!
 
Back
Top Bottom