Viongozi 'washtakiwa' kwa kutotangaza mali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi 'washtakiwa' kwa kutotangaza mali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Apr 12, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Viongozi 'washtakiwa' kwa kutotangaza mali


  Patricia Kimelemeta na Raymond Kaminyoge

  MBUNGE wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo na Mkuu wa wilaya ya Singida, Pascal Mabiti ni miongoni mwa watumishi wa umma waliofikishwa 'kizimbani' jana kujibu tuhuma za kushindwa kutangaza mali zao na madeni katika kipindi cha mwaka 2007 na 2008.Hatua hiyo imefikiwa, baada ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kutangaza wiki iliyopita kuwa viongozi wa serikali na wanasiasa wataanza kufikishwa kwenye baraza hilo, kujibu tuhuma zinazowakabili.

  Jana Baraza hilo limeanza kusikiliza shauri hilo tangu liteuliwe mwaka jana na Rais Jakaya Kikwete, huku likiongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu, Daniel Lubuva na wajumbe wawili ambao ni Jaji mstaafu Hamis Msumi na Jaji mstaafu Gidious Tibakwatila, chini ya wanasheria kutoka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma.

  Viongozi wengine waliofikishwa katika Baraza hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Simon Mayeye, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda,wakati aliyewahi kuwa Mshauri wa Rais, Rajabu Luhaji, alishindwa kufika kwenye baraza hilo kutokana na udhuru.Ofisa sheria kutoka Tume ya Maadili, Hassan Mayunga alisema viongozi hao wamevunja sheria ya uongozi wa maadili ya umma kifungu cha 9 na namba na 15 kinachowataka kutangaza rasilimali zao, madeni na watoto, chini ya miaka kumi na tano.

  Kutokana na kosa hilo, mwanasheria huyo ameliomba baraza hilo kusikiliza shauri hilo na kutoa maamuzi kwa vigogo hao.Katika utetezi wake Mbunge wa Rorya, Airo alisema hakuwahi kupata fomu za kujaza mali kutokana na mgogoro wa muda mrefu uliokuwepo katika halmashauri ya Rorya.

  “Nikiwa diwani sikuwahi kupewa fomu ambazo zilikuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya kwa kuwa kulikuwa na mgogoro ambao ulitufanya tushindwe hata kusalimiana,” alisema.Alisema kutokana na hali hiyo inawezekana fomu hizo zilifika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rorya, lakini alishindwa kuwapa madiwani .

  “Si kwamba sikuwa tayari kujaza fomu hizo, bali sikuzipata kutoka kwa mkurugenzi,” alisema.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbulu, (Mayeye), alisema alijaza fomu hizo na kumkabidhi mwanasheria wa halmashauri hiyo, aliyepewa kazi ya kukusanya fomu hizo lakini anashangaa kwa nini hazijaifikia tume.

  “Nimekuwa nikijaza fomu kwa miaka yote lakini nashangaa kwanini fomu hizo hazijaifikia Tume ya Maadili, naomba shtaka hilo liondolewe dhidi yangu,” alisema Mayeye.Alipoulizwa na wanasheria wa Tume ya Maadili, ni kwa nini hakufuatilia ili kuhakikisha kama fomu hizo zimeifikia tume, Mayeye alisema kwanini tume nayo haikufanya jitihada zozote kumjulisha kwamba ilikuwa haijapata fomu hizo.

  Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Lubuva alisema kazi ya baraza hilo ni kusikiliza utetezi wa tuhuma za kimaadili zinazowahusu viongozi hao na kutoa uamuzi.“Tunasikiliza mashauri haya na kuyatolea uamuzi, kisha tunampelekea Rais kuhusu kile tulichoamua kwa ajili ya yeye kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria,” alisema Jaji Lubuva.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Lubuva alisema ipo haja kwa viongozi kuendelea kuelimishwa kuhusu maadili ya viongozi.Alisema nchi inayoamini kuwa na utawala bora na wa kisheria, viongozi wake wanatakiwa kufuata maadili ya kazi zao.“ Viongozi kama kioo katika jamii wanapaswa kufuata maadili ya kazi wanazozifanya, kwani hiyo itasaidia kuwa na viongozi bora na waadilifu,” alisema Lubuva.mwisho
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hapa ccm wanatuzuga hamna chochote
   
 3. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  kwanini kusiwe na sheria kwamba baada ya mtu kupewa wadhifa atangaze mali zake ndani ya miezi 6 au mwaka, akishindwa basi moja kwa moja anapoteza wadhifa wake?
   
 4. d

  demokrasia Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii sekretarieti ni chombo muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. nchi haiwezi kuwa na maendeleo kama viongozi wake hawatakuwa na maadili. ni vema chombo hiki kiongezewe uwezo zaidi ili kiweze kusimamia maadili ya viongozi wa umma ipasavyo.
   
 5. d

  demokrasia Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sheria hiyo ipo.kiongozi wa umma anatakiwa atoe tamko lake la mali na madeni ndani ya siku thelethini baada ya uteuzi, kila mwisho wa mwaka, na wakati anapomaliza wadhifa wake.tafuta sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1995 usome.
   
 6. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimelipenda hilo la kutoa timeframe yenye automatic reward - kuwa ikipita muda unaotakiwa kuwa umetimiza mahitaji yote ya sheria hii basi automatically unapoteza sifa za nafasi ile. Kwa Wazo la msingi nafikiri iko vizuri nafikiri ourlearned friends will assit in shaping it as one of the inputs to the coming KATIBA. nafikiri suala la maadili litahitaji kufikiriwa upya katika katiba ili tume/kamati zitakazohusika ziwe na 'meno ya mamba'
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mbona katiba tuliyonayo hailazimishi mtu kutangaza mali? Ibara moja inaanza kwa kusema 'must declare...", inayofuata inasema hawezi kuwa na legal consequence! Ina maana kuna sheria inaipinga katiba? Sasa katiba inazidi kudhihirika kuwa ni mkusanyiko wa makaratasi tu! Isome katiba tuwake sawa kama kuna uwezekano wa kumtia hatiani mtu asiyetangaza mali na madeni yake. Jk aliwahi kutangaza mali zake mara ngapi? Narudi!
   
Loading...