• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Viongozi washiriki mazishi ya mke wa mbunge wa jimbo la wawi , Hamad Rashid

A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
858
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
858 0
[h=2]Friday, November 30, 2012[/h][h=3][/h]

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd. Kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Sheikh Abdallah Issa (kushoto), akiongoza dua ya kumuombea marehemu bibi Kisa Mohd nyumbani kwake Mikocheni Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali katika Makaburi ya Kisutu aliposhiriki mazishi ya bibi Kisa Mohd, mke wa Mbunge wa Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiweka mchanga katika kaburi la marehemu bibi Kisa Mohd, mke wa Mbunge wa Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd aliyezikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na Hasssan Hamad OMKR

Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali wameshiriki katika mazishi ya bibi Kisa Mohd ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd.

Mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya kisutu, yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa ADC bw. Said Miraji na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda.Mwili wa marehemu huyo ulisaliwa katika msikiti Maamur ulioko maeneo ya Upanga na baadaye kupelekwa katika makaburi ya Kisutu kwa ajili ya mazishi.

Marehemu bibi Kisa Mohd alifariki Jumanne iliyopita baada ya kusumbuliwa na matatizo ya Presha kwa muda mrefu, na kuzikwa Alkhamis tarehe 29/11/2012.

Akizungumza katika mazishi hayo, msemaji wa familia hiyo amewashukuru viongozi na wananchi waliojitokeza kushirikiana nao katika msiba huo, na kwamba familia imepoteza mtu muhimu ambaye pengo lake haliwezi kuzibika kwa kipindi kifupi.Imewekwa na MAPARA at 9:19 AM
 
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
23,216
Points
2,000
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
23,216 2,000
R.I.P. Mama Hamadi....nilifikiri Hamadi Rashidi anaishi Zanzibar.!
 
P

PYU

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2012
Messages
201
Points
195
P

PYU

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2012
201 195
kumbe wanaishi Dar, huko wawi yuko nani sasa? kweli bongo yote yanawezekana,poleni wafiwa
 
mtotowamjini

mtotowamjini

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
4,534
Points
0
mtotowamjini

mtotowamjini

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
4,534 0
mbunge wa wawi anayeishi mikocheni...sasa mnataka mbunge aishi wawi badala ya mikocheni wapi na wapi...mambo yote yako bongo nyiee
 
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Messages
19,162
Points
1,250
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2011
19,162 1,250
Ungesema tu kuwa ; Maalim Seif ashiriki..........................udaku writing style!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
R

royna

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
479
Points
195
R

royna

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
479 195
what!mbunge wa wawi anaiashi mikocheni! mmmh!my God!
 
S

slufay

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,385
Points
1,195
S

slufay

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,385 1,195
Hata shein hajapiga kura yake mwenywewe wakati wa uchaguzi! Eeeeboooo!
 
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,332
Points
2,000
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,332 2,000
Muungano hawautaki lakini wanataka kuzikwa Kisutu
 
Obama wa Bongo

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
5,245
Points
2,000
Obama wa Bongo

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
5,245 2,000
pole sana hamadi chidi!
poleni sana wana cuf
mbona sijamuona bwana mtatitiro
 
N

Nguto

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
2,943
Points
2,000
N

Nguto

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
2,943 2,000
He! Hamad anaishi Dar!! Hawa wazenj siwaelewi. Karibia wote wanapenda kuishi bara halafu wanataka muungano ufe!! Mh!!! Anyway pole zake kwa kufiwa.
 
mfianchi

mfianchi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
9,455
Points
2,000
mfianchi

mfianchi

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
9,455 2,000
R.I.P. Mama Hamadi....nilifikiri Hamadi Rashidi anaishi Zanzibar.!
Mimi nilifikiri anaishi Wawi na angemzika mke wake Wawi,naamini ana uwezo wa kusafirisha mwili wa marehemu kwa ndege hadi Wawi,udumu muungano
 
Kwetunikwetu

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2007
Messages
1,540
Points
1,225
Kwetunikwetu

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2007
1,540 1,225
Mimi nilifikiri anaishi Wawi na angemzika mke wake Wawi,naamini ana uwezo wa kusafirisha mwili wa marehemu kwa ndege hadi Wawi,udumu muungano
Muungano kwao mbaya mdomoni tu..!
 
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
40,133
Points
2,000
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
40,133 2,000
Unafki wa Wazanzibar ndio utauona hapo, Barubaru upo? hivi Nchini kwenu Zanzibar hakuna makaburi?
 
Last edited by a moderator:
mchumia tumbo

mchumia tumbo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Messages
1,442
Points
1,500
mchumia tumbo

mchumia tumbo

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2012
1,442 1,500
Tanganyika pazuri asikuambie mtu
 
Bee hive

Bee hive

Senior Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
141
Points
225
Bee hive

Bee hive

Senior Member
Joined Feb 22, 2012
141 225
pole kwa wanafamilia.
swala la wapi mb anaishi si sehemu yake ktk thread hii.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,869
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,869 1,225
Friday, November 30, 2012
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Kissa Gwalugano Mohamed,ambaye ni mke wa Mbunge wa Wawi,Zanzibar Bw.Hamad Rashid Mohamed,kwenda msikitini na mazishi kufanyika jana jioni katika makaburi ya Kisutu,Dar es salaam.
Na Goodluck Hongo

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliongoza mamio ya waombelezaji katika mazishi ya Kissa Gwalugano Mohamed ambaye ni mke wa Mbunge wa Wazi, Zanzibar Bw. Hamad Rashid Mohamed.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Pamoja na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. Wiliam Lukuvi, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh.


Wengine ni Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo, viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wabunge.

Katika msiba huo, viongozi wa kisiasa waliweka pembeni tofauti zao na kumfariji Bw. Mohamed ambaye chama hicho kiliwahi kumfukuza uanachama.

Mazishi hayo yalifanyika Dar es Salaam jana katika makaburi ya Kisutu, saa kumi jioni.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Profesa William Matuja aliwashukuru viongozi wote walioshiriki mazishi hayo kwani wamefarijika sana ingawa wamepata pigo kwa kifo hicho.

Marehemu alizaliwa Oktoba 20,1955 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, alisoma katika Shule ya Msingi Azimio, baadaye Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam.

Alisema baadaye alijiunga na masomo ya kompyuta na kuajira THB (iliyokuwa Benki ya Nyumba nchini), lakini alichana kazi na kuamua kujiajiri mwenyewe hadi mauti ilipomkuta.

Alifunga ndoa na Bw. Mohamed mwaka 1984 na walibahatika kupata watoto kati ya hao mmoja wa kiume. Marehemu alikuwa akilalamika kusumbuliwa na mgongo na baada ya kupimwa
iligundulika kuwa na ugonjwa wa mifupa.

Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Novemba 27 mwaka huu, baada ya kuzidiwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kufariki saa tatu usiku.


Majira


 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,869
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,869 1,225
Si Juzi tu Alishindwa KESI MAHAKAMANI kuhusu UBUNGE wake? Sasa Amefiwa na MKEWE... R.I.P Mama HAMAD!!!

Wake wa WABUNGE hawapelekwi INDIA??

**** Unaona NCHI yetu ilivyo diverse??? Mh. Hamad Mkewe alikuwa MKRISTO; Wa BARA...
 

Forum statistics

Threads 1,405,649
Members 532,072
Posts 34,491,930
Top