Viongozi wanne Chadema Kilolo wakimbilia CCM

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
618
1,000
1565158835726.png

VIONGOZI wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Ihimbo, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wamefunga ofisi yao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wameeleza kujitoa Chadema wakidai kuridhishwa na utendaji kazi wa mkuu wa wilaya ya Kilolo, mbunge na diwani wao.

Viongozi hao, Katibu Kata, Livingiston Chang’a ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Utengule, Mwenyekiti wa Kata ya Ihimbo, Baton Ndenga, aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Utengule, Pangarasi Mkakatatu na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magangamatitu, Jordan Mkakatu walikabidhi kadi za Chadema kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Erasto Sima jana.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM, Chang’a alisema awali walikuwa wanachama wa chama hicho kabla ya kujiunga upinzani.
Alisema walilazimika kwenda upinzani ili kuwapigania wananchi, lakini tangu wamekuwapo huko hakuna hoja mpya.

Chang’a alisema tangu wamekuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah, amekuwa akifika kwenye kata yao kushiriki shughuli nyingi za maendeleo.

Alisema changamoto zilizokuwapo ambazo wao wakati wanajiunga na upinzani walikuwa wakizisemea, tayari zimefanyiwa kazi na Serikali.

Akiwashukuru wanachama hao, Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto, aliwapongeza kwa kutambua kazi zinazofanywa na CCM katika kata yao.
Kwa upande wake, Sima alisema viongozi hao wameonyesha imani kubwa kwao.
“Binafsi nawapongeza viongozi wa Chadema ambao mmerejea CCM, mmeonyesha imani kubwa kwa Serikali, karibuni,” alisema.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,529
2,000
Kati ya wabunge wa hovyo duniani ni huyo Mwamoto!

Hivi Mwamoto umeahindwa kabisa kutengeneza hiyo barabara ya kilolo inayopitiwa na vijiji muhimu kama Kidabaga, Ng'ang'ange, Boma la ng'ombe, Ng'ingula, Masisiwe, Idegenda, Madege na kuendelea? Angalau hata kwa changalawe ili ipitike kwa mwaka mzima?

Ukitengeza hiyo barabara kuzunguka hivyo vijiji utakuwa Kilolo itakuwa Paradiso sasa wewe umekalia mambo ya uchawi tuu! Shame on you
 
Diason David

Verified Member
Aug 2, 2018
7,554
1,995
Kuwa upinzani sio maslahi wala kutafutwa kupendwa bali moyo na kujitolea popote ka nafasi yako ila wasije wakaona aibu kwa kile kitakacho tokea mbele ya macho yao niwape wafikishe salaam za huko kuwa sisi hatujambo na mapambano yanaendelea
 
cmsuma

JF-Expert Member
Apr 18, 2015
324
250
View attachment 1174262

VIONGOZI wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Ihimbo, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wamefunga ofisi yao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wameeleza kujitoa Chadema wakidai kuridhishwa na utendaji kazi wa mkuu wa wilaya ya Kilolo, mbunge na diwani wao.

Viongozi hao, Katibu Kata, Livingiston Chang’a ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Utengule, Mwenyekiti wa Kata ya Ihimbo, Baton Ndenga, aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Utengule, Pangarasi Mkakatatu na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magangamatitu, Jordan Mkakatu walikabidhi kadi za Chadema kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Erasto Sima jana.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM, Chang’a alisema awali walikuwa wanachama wa chama hicho kabla ya kujiunga upinzani.
Alisema walilazimika kwenda upinzani ili kuwapigania wananchi, lakini tangu wamekuwapo huko hakuna hoja mpya.

Chang’a alisema tangu wamekuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah, amekuwa akifika kwenye kata yao kushiriki shughuli nyingi za maendeleo.

Alisema changamoto zilizokuwapo ambazo wao wakati wanajiunga na upinzani walikuwa wakizisemea, tayari zimefanyiwa kazi na Serikali.

Akiwashukuru wanachama hao, Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto, aliwapongeza kwa kutambua kazi zinazofanywa na CCM katika kata yao.
Kwa upande wake, Sima alisema viongozi hao wameonyesha imani kubwa kwao.
“Binafsi nawapongeza viongozi wa Chadema ambao mmerejea CCM, mmeonyesha imani kubwa kwa Serikali, karibuni,” alisema.
Ok
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom