Viongozi wangapi wakistaafu wanategemea kurudi kwao?

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Leo jioni nimetembelea kijiwe cha kahawa, wazee wakawa wanajadiliana mithali inayisema "mkataa kwao ni mtumwa!"

Wazee hao walielezea jinsi ambavyo watu wengi wamekuja mjini wakatelekeza kwao! Mbaya zaidi hata wakifa wanataka wazikwe mjini!

Ndio maana watu wengi wanatoka vijijini kuja mijini (urbanisation). Umewahi kujiuliza kwanini? Mojawapo ni huduma za kijamii na wakati mwingine kuosha macho.

Leo hii Serikali ya Rais Magufuli inafanya mambo makubwa mijini na vijijini kiasi kwamba hata foleni za kuja mijini zinazidi kupunguza. Hayo ndiyo Maendeleo ktk uchumi wa kati. Mwananchi apate huduma zote hapo alipo!

Wengi wa wale wanaopinga Maendeleo Chato ni watu ambao wametoroka kwao hata watoto wao hawataki kuwaonesha kwao na hawana mpango wa kurudi. Tubadilike Ndg zangu. Ndio maana Rais Magufuli aliwahi kusema kuna watu hata Shule za Msingi walikosoma na Sekondari hawajawahi hata kurudi wakachangia hata Ujenzi wa darasa moja.

Wivu wa Maendeleo ni pamoja na kupenda kwenu! Pia Maendeleo Tanzania ni kila kona.

Povu ruksa Ila usinifokee tafadhali. Ukifoka sana najua wewe ni wale jiwe la gizani limewapata. Haahaa!
 
Charity begins at home, lakini siyo kwa kutumia KODI za wananchi.

Mwalimu Nyerere alipostaafu alirudi kwao Butiama pamoja na kwamba wako wanaopadharau kwa kudai hakuna maendeleo.
 
Bado mnahangaika kujibu hoja, ila mnapapasa tu! Kiukweli hili suala la Chato litawatesa sana kwani majibu yake ni magumu kuliko uwezo wenu wa kujenga hoja!Ndio maaana zimeshaanzishwa nyuzi lukuki kujibu lakini bado zimepwaya!

Dunia inakwenda kasi sana, leo hii ni sifa kiongozi kuoendelea eneo alilozaliwa kwa kujaza miradi bila kujali vipaumbele? Nyerere akifufuka atatamani arudi kaburini!
 
Bado mnahangaika kujibu hoja,ila mnapapasa tu!Kiukweli hili suala la Chato litawatesa sana kwani majibu yake ni magumu kuliko uwezo wenu wa kujenga hoja!Ndio maaana zimeshaanzishwa nyuzi lukuki kujibu lakini bado zimepwaya!

Dunia inakwenda kasi sana,leo hii ni sifa kiongozi kuoendelea eneo alilozaliwa kwa kujaza miradi bila kujali vipaumbele?Nyerere akifufuka atatamani arudi kaburini!!

Hebu fikiria uwekezaji ambao Mizengo Pinda ameufanya Dodoma.

Je, nini kinamzuia kufanya uwekezaji kama huo kwao Katavi na kuishi huko?

Na kwa pensheni nono wanayopewa viongozi wakuu wastaafu hivi kuna ulazima gani wa kuwa wezi na waroho wanaopendelea vijiji walikozaliwa?
 
..Charity begins at home, lakini siyo kwa kutumia KODI za wananchi.

..Mwalimu Nyerere alipostaafu alirudi kwao Butiama pamoja na kwamba wako wanaopadharau kwa kudai hakuna maendeleo.
Kwani wananchi wa Chato sio Watanzania?
 
Hebu fikiria uwekezaji ambao Mizengo Pinda ameufanya Dodoma.

Je, nini kinamzuia kufanya uwekezaji kama huo kwao Katavi na kuishi huko?

Na kwa pensheni nono wanayopewa viongozi wakuu wastaafu hivi kuna ulazima gani wa kuwa wezi na waroho wanaopendelea vijiji walikozaliwa?
Maendeleo yamegawanywa nchi nzima. Tatizo una wivu wa kike!
 
Yaani Chato zimewekwa hadi Taa za kuongozea magari wakati hayo magari yenyewe yanahesabika! Miji mikubwa Mingi tu haina taa hizo, ila Chato wanazo!

Funga mwaka itakuwa huo uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu!
 
Bado mnahangaika kujibu hoja,ila mnapapasa tu!Kiukweli hili suala la Chato litawatesa sana kwani majibu yake ni magumu kuliko uwezo wenu wa kujenga hoja!Ndio maaana zimeshaanzishwa nyuzi lukuki kujibu lakini bado zimepwaya!

Dunia inakwenda kasi sana,leo hii ni sifa kiongozi kuoendelea eneo alilozaliwa kwa kujaza miradi bila kujali vipaumbele?Nyerere akifufuka atatamani arudi kaburini!!
Kusingekuwa na vipaumbele usingeona miradi kila kona ya nchi. Sekta zote, Maji, Elimu, Afya, Miundombinu, nk Shida ni wivu wa kike!
 
Kusingekuwa na vipaumbele usingeona miradi kila kona ya nchi. Sekta zote, Maji, Elimu, Afya, Miundombinu, nk Shida ni wivu wa kike!
Bado hujajibu hoja za msingi! Na hilo ndio tatizo! Taja wilaya moja tu yenye miradi mikubwa kama Chato!
 
Yaani Chato zimewekwa hadi Taa za kuongozea magari wakati hayo magari yenyewe yanahesabika!Miji mikubwa Mingi tu haina taa hizo,ila Chato wanazo!
Funga mwaka itakuwa huo uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu!
Wivu tu wa kike! Yaani Chato kuwa na taa za barabarani roho inakuuma! Uliwahi kujiuliza ule Mkoa unapata shs ngapi mapato ya ndani kwenye Halmashauri na Manispaa? Bila kusahau CSR itokanayo na madini na viwanda vya samaki?
 
Hakuna mkoa wa Chato bali kuna mkoa wa Geita!
 
Wivu tu wa kike! Yaani Chato kuwa na taa za barabarani roho inakuuma! Uliwahi kujiuliza ule Mkoa unapata shs ngapi mapato ya ndani kwenye Halmashauri na Manispaa? Bila kusahau CSR itokanayo na madini na viwanda vya samaki?

Sasa kwanini kila mradi wanapeleka Chato badala ya kusambaza miradi ktk maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa?

Hebu tueleze ni jimbo gani ktk kanda ya ziwa limelundikiwa miradi mikubwa mikubwa kama Chato.
 
Maendeleo yamegawanywa nchi nzima. Tatizo una wivu wa kike!

Nimekwambia weka list ya hospitali na vituo vya afya vilivyojengwa vikionyesha mkoa, wilaya, tarafa/kijiji ilipo, ili tujiridhishe na huu utetezi wako. Haya matumizi mabaya ya madaraka ni ngumu sana kuyatetea, na kiongozi muadilifu asingeweza kufanya kwao kwa kiwango hicho.
 
Tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea!

Kijijini Chato kujengwa international airport?
 
Back
Top Bottom