Viongozi Wanapoteza Muda

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,662
Jambo hili nimeliona kwa muda mrefu na linakera. Wanapoteza muda sana kwa umati mzima kwenda kumuaga Raisi, na baadaye kumpokea. Kwani akiagwa na maofisa wa wizara ya mambo ya nje kuna ubaya gani?

Vice President, Dr Ali Mohamed Shein and Prime Minister Edward Lowassa and several cabinet ministers, including the Minister for Defence and National Service, Prof Juma Kapuya, turned up at the airport to bid President Kikwete farewell yesterday afternoon. Others present were Minister for Higher Education, Science and Technology, Prof Peter Msolla and the Minister for Energy and Minerals, Dr Ibrahim Msabaha. Ministers for Water Stephen Wassira, Natural Resources and Tourism Anthony Diallo and State Minister in the President’s Office (Political and Social Affairs)Kingunge-Ngombale Mwiru were also present. The President was accompanied by First Lady Salma Kikwete and Minister for Foreign Affairs, Dr Asha-Rose Migiro, among other dignitaries. ·
 
Mnajua kuwa waziri haimaanishi kuwa unaweza kumuona rais muda wowote unaotaka au kumpigia simu hebu jaribu kufikiri mawazi sitini wanataka kum-inform rais juu ya jambo fulani watafanyaje. Na kama tunavyojua rais wetu hakai ofisini sasa njia pekee ya kum-inform kuhusu mambo yao ya kiakazi ni kumfuata aliko. That is the only reason I can think out of it. Kama siyo kweli basi naunga mkono ni upotezaji wa muda.
 
Sam,
Raisi anapata taarifa za utendaji ktk vikao vya baraza la mawaziri, na vilevile kupitia kwa waziri mkuu. kama kuna suala la muhimu linalohitaji attention ya Raisi basi hakuna budi kuwe na appointment rasmi na Raisi.

kama masuala muhimu ya wananchi yanajadiliwa kwenye tarmac pale airport basi nchi yetu ina matatizo makubwa sana. huu utaratibu wa kumuaga na kumpokea Raisi sijauona ktk nchi zilizoendelea.

posted by Filgga
labda na wao wanao responsibilitiy huko..
responsibility ya kumuaga Raisi? lakini wewe upo karibu nao labda unaelewa zaidi.
 
Basi tuu.. wengine wanataka waonekane ni watendaji.. unajaua wengi wanapenda sifa... ndio mana wanataka kujipendekeza pendekeza huko
 
Jokakuu
Baraza la mawaziri ni kikao ambacho kinakuwa na agenda siyo cha kupena brief za utendaji au ufuatiliaji wa kitu. Kwa mfano, rais amekuagiza kufuatilia malalamiko walimu wa shule za msingi mkoa wa Dodoma. Ukipata ufumbuzi si unatakiwa ukamweleze umefikia wapi? Je utamwambia waziri mkuu amwambie mkubwa wake? Labda kama akikuambia uripoti kwa waziri mkuu akikuambia uripoti kwake you have to see him. Kwa ratiba za JK ni lini utapata appointment? Do you need appointment kum brief kitu cha less za a minute? Wakati mwingine unatakiwa kumwambia "Mzee ile kazi uliyonituma nimeshaifanya" That's it. Do you need appointment for that lazima utafute sehemu yoyote umwambie. Au utamwambia El amwambie rais kuwa umemaliza kazi aliyokutuma? Je, mnadhani JK atafurahi kuona mtu amekuja airport na kumpa mkono na kuondoka. Sisemi this is the right way to do things. Ningemshauri rais achukue muda fulani wa ratiba yake kukaa ofisini na kupata brief za watendaji wake. Kwa mfano safari ya kwenda Angola kwa siku mbili ilikuwa haina umuhimu wowote ule. Nasema hivi kutokana na experience ya kitu nilichowahi kukutana nacho, kuna mkuu mmoja wa idara aliagizwa mambo fulani na Mkapa alishindwa kuweka appointment na Mkapa kwa mwezi mzima alikuwa anahitaji kama saa nzima kuongea naye ilibidi afanye juu chini awekwe kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasafiri na Mkapa kwenye ndege ili aweze kuongea naye kwenye ndege kwenda mkoani. Nilimuuliza hivi ni ngumu kiasi hicho kumuona rais? Akaniambia rais akiwa Dar ni vigumu sana kumuona. Hivi unajua ni watu wangapi walifunga safari kwenda Mwanza waliposikia rais yuko huko kwenye mapumziko?
Again, haya ni mambo ninayofikiria mimi ambayo hana excuse kama that is not the situation hilijambo naungana nanyi linatakiwa likemewe.
 
Kuna mtu aliwaho kusema Sirikikali ya JK ina walaji wala si watendaji. Lakini pia ni aibu sana mawaziri hawa hata JK mwenyewe kutokuelewa kwamba ni gharama kubwa kwa misafara kula pesa za umma na pia kuwachelewesha wananchi muda wote kungojea wao wapite ndipo wananchi waendelee na shuguli .JK kwa kuwa anaenda Temeke kupitia Ilala anapashwa kusindikizwa na polisi wa uslama barabarani na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwisha kazi .
 
Joka Kuu,


Hii ni moja ya jambo la kijinga sana na upotevu wa hela za wananchi ! Kwa nini watu wasindikizane kama wanaenda jandoni ? Sam unasema viongozi wengine wanataka kuongea na Rais ! swali ni kuwa Rais hapo airport anakaa kwa muda gani ? i dought hata kama dakika ishirini zinafika !

Utaongea vipi na rais wakati kuna viongozi zaidi ya ishirini ? This B.S has to stop , we can't tolerate it anymore ! The only person who is supposed to there is only Cisco Mtiro....................The rest ....GO BACK TO WORK.
 
Joka Kuu,


Hii ni moja ya jambo la kijinga sana na upotevu wa hela za wananchi ! Kwa nini watu wasindikizane kama wanaenda jandoni ? Sam unasema viongozi wengine wanataka kuongea na Rais ! swali ni kuwa Rais hapo airport anakaa kwa muda gani ? i dought hata kama dakika ishirini zinafika !

Utaongea vipi na rais wakati kuna viongozi zaidi ya ishirini ? This B.S has to stop , we can't tolerate it anymore ! The only person who is supposed to there is only Cisco Mtiro....................The rest ....GO BACK TO WORK.

Bado haujafa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom