Viongozi wanapaswa kulinda vinywa vyao dhidi ya matamko yenye athari kwa Jamii

vicdala55

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
1,009
1,638
"Haka kaugonjwa ni kadogo, tusitishane"

Hii ni kauli ya hatari sana kutolewa na Kiongozi yeyote katika Jamii. Mbaya zaidi kauli hii ilitolewa wakati ambao Mataifa mengi yanapoteza watu wao kwa vifo vitokanavyo na ugonjwa ambao Nchini kwetu tumeambiwa hauna madhara hivyo tuendelee kufanya kazi tusije kufa na njaa.

Ingawa sio leo ama kesho, lkn nina hakika waliotoa kauli kama hii watakuja kujutia hadharani na pengine kuomba wasamehewe kwa kupitiwa kwao.

Ukiangalia takwimu mpya zilizotolewa na Waziri wa Afya kuhusiana maambukizi ya virusi vya COVID 19, unapata picha kwamba kuna mchango mkubwa wa maambukizi uliotokana na zile kauli.

Watu walioambiwa na wataalamu kote Duniani wachukue tahadhali, walibadilishwa misimamo na Viongozi wetu. Pengine walipuuzia na kuanza kujiachia bila tahadhali yoyote.. Inasikitisha sana ingawa hatuna budi kusonga mbele katika kukabiliana na maambukizi mapya.

Kauli nyingine ya kusikitisha ni hii ya Waziri mwenye dhamana ya Afya.. Kwamba sasa inabidi tuseme ukweli, maana yake hapo nyuma ama taarifa za kabla zilikuwa na uongo mwingi!

Tujiulize katika uongo huo watu wangapi tumewasababishia matatizo?

Nina shaka kwamba kama isingekuwa tamko la Marekani kuichunguza China kwa kutoa taarifa za uongo juu ya athari na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Corona Nchini China, bila shaka hata kwetu Taifa lingeendelea kupewa taarifa zisizo sahihi.

China imehofia matokeo ya uchunguzi na pengine adhabu ya Kimataifa, wametangaza vifo zaidi ya 1200 vya ziada. Wanadai vilisahaurika kimakosa! Hii ni ajabu sana.

Je, Serikali yetu imehofia hilo pia?

Nawashauri Viongozi wetu kuchunga ndimi zao, kuzichuja kauli zao kabla hazijafika kwa Umma, na pengine kuwa na utamaduni wa kuomba radhi kutokana na kauli zenye kuleta athari kwa Jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi wa Nchi hatakiwi kuwa mwoga,

Ndio corona ni ugonjwa mdogo sio km Ukimwi na Ebola

Km unamfatilia Trump au Putin hotuba zao utajua

corona inapita haitadumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi wa Nchi hatakiwi kuwa mwoga,

Ndio corona ni ugonjwa mdogo sio km Ukimwi na Ebola

Km unamfatilia Trump au Putin hotuba zao utajua

corona inapita haitadumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ikipita na mumeo au na mama yako mzazi ndio utajua thamani ya uhai wa binadamu na utajua hata uhai mmoja ni wa thamani kiasi gani. We jibu jibu tu kwa kudhania wale inaopita nao hawakuhusu na hawana thamani.
 
Ajabu unaweza kufa kwa kuzidisha bangi kichwani
Punguza bangi Mkuu,
Ikipita na mumeo au na mama yako mzazi ndio utajua thamani ya uhai wa binadamu na utajua hata uhai mmoja ni wa thamani kiasi gani. We jibu jibu tu kwa kudhania wale inaopita nao hawakuhusu na hawana thamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikipita na mumeo au na mama yako mzazi ndio utajua thamani ya uhai wa binadamu na utajua hata uhai mmoja ni wa thamani kiasi gani. We jibu jibu tu kwa kudhania wale inaopita nao hawakuhusu na hawana thamani.
Yaani kwa kweli huyu mtu anayeitwa Bia Yetu sijui amepatwa na nini? Yaani yeye kila kitu anachukulia siasa za CCM na CHADEMA. Na kila mtu anayekuwa tofauti nae basi yeye anamwita CHADEMA. Kweli tutafika? Na kila wakati anaanzisha mada zisizo na kichwa wala miguu. Nafikiri ifike wakati moderator awe anaziondoa mada zisizo na msingi anazoziasha kila wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom