Viongozi wanaonenepeana, viongozi wanaokwiva madarakani - Taifa linalodidimia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wanaonenepeana, viongozi wanaokwiva madarakani - Taifa linalodidimia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Aug 21, 2010.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wengi tunaweza kuona mwonekano alionao Rais wa Marekani hivi sasa, Obama na kulinganisha jinsi alivyoonekana miaka miwili tu iliyopita. Wengi tunakumbuka jinsi Rais mstaafu Clinton alivyozeeka haraka haraka baada ya kuingia madarakani. Vivyo hivyo kwa PM mstaafu wa Uingereza, Tony Blair. Wote hawa walizeeka ghafla bin vuu baada ya kushika hatamu za uongozi.


  Nimejiuliza swali baada ya kusoma bandiko la NN. Kwanini wabunge wetu wengi na viongozi kwa ujumla wananenepeana baada ya kushika uongozi??!!
  Inatokea thread hii: https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/70521-kikwete-kadondoka-jangwani-4.html#post1039702

  Jibu langu ni kwamba, wengi wa viongozi wetu hawafanyi kazi. Wanaingia madarakani kwenda kujiburudisha, na ndicho hicho kinachowapelekea kukwiva. Kama wangelikuwa wanafanya kazi ipasavyo, kweli Taifa letu lingekuwa na hali hii kimaendeleo??!

  Steve Dii
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Waenda madarakani kutumikiwa na kuneemeka!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Aug 21, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kwao madaraka ni njia mojawapo ya kula 'good time"....

  Kwa hali ya taifa, kiongozi ambaye kweli anafanya kazi katu asingeweza kunawiri. Utanawirije ilhali kuna wajawazito wanajifungulia sakafuni? Utakwivaje wakati watoto wanasoma shule chini ya miti ya miembe? Muda wa kukwiva utautoa wapi?
   
Loading...