Viongozi wanaomsifia sana Rais Samia wachunguzwe

Joel Kisoka

Member
Dec 21, 2018
23
31
Tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani kumekua na wimbi kubwa la viongozi wanaomsifia Kwa kila Jambo wakitumia kauli ambayo mm naona imejaa unafki na janjajanja kauli ya kwamba "Mama anaupiga mwingi."

Kila mara ninaposikia kauli hii ikiandikwa mitandaoni au ikitamkwa hasa na wale wenye mamlaka serikalini huwa najawa kicheko na sijui hua kinatoka wapi lakini kuna wazo linanijia akilini mara moja kwamba "Huyu mwamba kashapiga zake na sasa anaficha upigaji wake kwenye kauli ya mama anaupiga mwingi"

Tofauti na miaka mitano iliyopita wakati nchi inaogozwa na hayati Rais John Pombe Magufuli katika awamu ya tano, katika awamu hii kumekuwa na hofu na kutokua na uhakika miongoni mwa wananchi kuhusu matumizi ya fedha ambazo zinatolewa na serikali kuu Kwa ajili ya kuleta maendeleo Kwa wananchi.

Wananchi tumegubikwa na hofu na kuona kwamba kuwa Ile hofu waliokuwa nayo viongozi katika awamu ya tano ya kutokudokoa kama sio kukomba fedha za uma sasa haipo tena ama kama ipo basi ni Kwa wale viongozi "new school" Yani waliokuzwa katika awamu ya tano ambapo uaminifu ulikua kigezo kikubwa cha kutetea ofisi lakini Kwa wale waliopita katika awamu ya nne hasa ndo wanatutia wasiwasi wananchi.

Tunapoona kiongozi aliyekuwepo katika awamu ya nne anateuliwa basi wananchi nywele zinatusimama tukijua kwamba tunaenda kupigwa hapa na mfano hai hapa ni uteuzi wa January Makamba ambaye sikuizi mtaani tunamuita "Ntu ya dili"

Baada ya Makamba kuteuliwa katika wizara ya nishati zile adha za mgao wa umeme na drama katika sekta ya nishati ndo Kwanza season mpya imeanza na tena ni episode za mwanzomwanzo.

Ingawa pia walikuwepo waliomsifia Rais Magufuli katika awamu Ile ya kihistoria lakini hawakututia hofu kama hawa wapambe wa siku hizi ambao wameibuka katika Zama ambayo watu wa hulka hiyo huitwa chawa kwani wanasifia ili wale Yani wanang'ata halafu wanapuliza.

NB; NI MGENI HUMU KAMA KUNA PAHALA NIMEHARIBU MNIVUMILIE!
giphy.gif
 
Ntu ya dili! vipi alipiga dili gani mkuu,tusiofuatilia tuna hamu ya kutaka kujua,maana awamu ya nne hakukuwa na tumbua tumbua,huenda angetumbuliwa wakati huo tungejua nini chanzo mkuu
 
Ntu ya dili! vipi alipiga dili gani mkuu,tusiofuatilia tuna hamu ya kutaka kujua,maana awamu ya nne hakukuwa na tumbua tumbua,huenda angetumbuliwa wakati huo tungejua nini chanzo mkuu
Ntu ya dili Kwa maana ya mtu anayecheza na fursa ndo kizungu huitwa opportunist Kaka.
 
Uchawa umetawala Sana viongozi wetu hasa hao WA old school before Magufuli's reign
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom