Viongozi wanajeshi huwa hawana mafanikio kisiasa

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
735
191
Heri ya mwaka mpya wana JF.

Uzoefu wetu katika siasa unaonyesha kuwa viongozi wengi wa nchi ambao walikuwa wanajeshi huwa hawana mafanikio ya maana. Nchi nyingi zilizotawaliwa na askari au Wanajeshi zinatawaliwa kiubabe au kwa ubadhilifu mkubwa. Ni askari wachache sana wa kutolea mfano kama Jerry Rawlings ambao wameleta mafanikio kwenye nchi yake ya Ghana. Wengine waliobaki kwa kweli ni maumivu tu. Kuna nini kimejificha?
 
Wengi wao inaonekana hawatumii ufahamu wa kijumla (universal) bali hutumia zaidi ufahamu walionao kijeshi na huona huo kuwa ndiyo uelewa watu wote
 
mtu msomi huwa anatoa mifano na ushahidi, nakushangaa hujaonyesha hata mfano mmoja.
 
fidel castro ruz, rais mstaafu wa cuba,ni komandoo na anakubalika kwa utawala bora na msimamo wake dhidi ya ubepari. Mtoa mada badili kauli yako, huna uhakika na ushahidi wa kutosha, hebu mtazame paul kagame alivyoitoa rwanda kwenye genocide mpaka kuifikisha hapo ilipo. Shabbash!
 
Back
Top Bottom