Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 262
- 778
Unaweza kushangaa mpaka Leo taifa la Tanzania bado misongomano misikitini na makanisani bado inaruhusiwa. Duu Ni ajabu! Inamaana Hawa viongozi wetu wanaishi visiwani kwamba yote yanayotokea Ulimwenguni hawayasikii Wala kuyaona!
Inajulikana kabisa kwamba msongamano ndio njia rahisi kabisa ya kueneza virus vya COVID-19 lakini kwa Tanzania misongomano kwa baadhi ya maeneo bado inaruhusiwa.
Nchi za ulaya pia zilidhani huo ni ugonjwa wa wachina pekee Kama baadhi ya watanzania wanavyoamini ugonjwa huu Ni wawazungu pekee kitu ambacho Ni kibaya maana madhala yatakuwa makubwa zaidi.
Katika mitandao ya kijamii Kuna kaujumbe kanasambazwa kakimusifu rais wa nchi kutokuzuia misongomano ya ibadani pia mkuu wa mkoa wa dar es salaam hivi juzi ameitisha mkutano wa azara akiongelea suala Hilo Hilo la kutokuzuia misongomano ya ibadani eti kinafiki kwamba Mungu huyo huyo aliyewavusha kwenye majanga ya Ebola, matetemeko ya ardhi, tsunami n.k ndio huyo huyo atawavusha kwenye janga hili la Corona.
Duu! Naduwahaa!
Hivi ni lini mtu muovu, katili, mnafiki na yeye akajitapa kwamba anaamini katika Nguvu ya Mungu?
Ni lini Roho Safi ya Mungu ikaambatana na Roho chafu za wanadamu?
Viongozi hao wanaojionyesha leo Wana hofu ya Mungu ndio hao hao wanaongoza kwa mauaji, visasi, Roho mbaya na matendo yote ya kikatili kwa wanadamu wenzao.
Tafadhali enyi vipofu msimjaribu Bwana Mungu wenu.
ZUIENI MISONGOMANO YA IBADA MAKANISANI NA MISIKITINI kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu hatari kwa wana wa Mungu wasio na hatia.
Mnapozuia misongomano ya ibada makanisani na misikitini sio kwamba mmezuia Imani za watu Bali mnalida afya zao. Maana sio busara kujitumbukiza kwenye shimo na kujifariji kwa kusema Mungu atakuinua kutoka katika shimo Hilo.
Serikali isisitize Watu wazidi kusali na kutubu majumbani mwao (kifamilia) wakimulilia Mungu aiepushe dunia juu ya mipango ovu ya ibilisi na sio kudanganya watu kwamba Corona haiwezi kuwafikia kwa wao kuendelea kujazana makanisani na misikitini.